Mifuko ya Plastiki na Mazingira: Marufuku zisizo na mwongozo unaoeleweka!

Monie

Member
Sep 22, 2007
26
6
Ni zaidi ya mwaka sasa tangu serikali na bunge letu tukufu kupiga marufuka mifuko ya plastiki inayotumika kwa shughuli mbalimbali hapa nchini, kama vile kufungia bidhaa madukani, sokoni hata kufungia vyakula kama chips,n.k

Kama kawaida serikali ilitangaza muda wa matumizi ya mifuko hii kutumika kwa kuzuia viwanda vinavyotengeneza visitengeneze tena na wale wanaoagiza kutoka nje wasiagize tena.

Mimi nilifikiria baada ya muda uliotolewa kwisha serikali ingechukua hatua madhubuti kuhakikishia mifuko hii haitumiki tena kwani inachafua sana mazingira na kama wataalamu walivyosema hata ikichomwa bado moshi wake unakuwa na madhara kwa viumbe hai ikiwa ni pamoja na binadamu.

Serikali ilitoa aina ya mifuko ambayo inaruhusiwa kutumika lakini sidhani kama wanachi wanaelewa ni mifuko ya ubora gani ambayo siyo mizuri na gani ambayo ni mibaya. Bora wangeweka wazi jambo hili ili kuepusha usumbufu kwa wananchi.

Majuzi serikali ilizinduka na kuanza kuwakamata vijana Wamachinga wanouza mifuko hiyo mitaani na kuwatishia kuwapeleka mahakamani huku askari wanaowakamata wakitokomea na mifuko yao. Kinachonishangaza ni kwamba kwanini wasikamate chanzo cha mifuko hiyo? Kwanini wasishitaki viwanda vinavyotengeneza mifuko hiyi? Kwanini wasiwakamate wale wanaoingiza mifuko hiyo kutoka nje? Hawa wamachinga mnawaonea bure kateni shina na siyo matawi.

Lakushangaza zaidi wakati wamachinaga wanapambana na miganmbo wa serikali mifuko hiyo inaendelea kutumika kwenye supermarkets kama kawaida na bila kubugudhiwa na mtu yeyote. Mfano supermakets za Shoprite wanaingiza tani nyingi sana za mifuko hiyo ya plastiki, Je serikali inataka kutuambia kuwa mifuko hiyo iko kwenye kiwango kinachohitajika?

Na kama sivyo kwanini wasikamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria? Shoprite ni mfano tuu zipo supermarkets nyingi sana hapa mjini wanatumia mifuko ya plastic. Ingekuwa vyema basi serikali na nyie watu wa mazingira mkaanza na hao ndio mgeukie wamachinga, vinginevyo zoezi hili halitafanikiwa kwa kuwaonea wadogo wanouza mifuko 20 na kuwaachia wale wanaoingiza kwa makontenna.

Igeni mfano mzuri wanchi jirani yetu Kenya wamefanikiwa sana kwa hili kwani walianza kuiziua kwenye supermarkets zote, wakafuatia wauzaji wadogo, mwisho watuumiaji wenyewe na sasa huwezi kumkuta mtu mjini Nairobi kabeba mfuko wa plastiki haijalishi ni wakiwango gani wanakamatwa.

Sasa sisi Tanzania inatushinda nini, serikali amka! Wizara husika amka, na nyie watu wa mazingira fanyeni kazi yenu. Wenye viwanda tengenezeni mifuko ya karaasi na katani isiyochafua mazingira.

Natumaini nimesikika Mkereketwa wa Mazingira.

Naona uchungu sana serikali inaposhindwa kusimamamia na kutekeleza sheria iliyojiwekea yenyewe!!! WHyyyy kwaniniiiiiiiii?
 
Umetoa mifano mizuri ya hatua za haraka za kuchukuliwa ili kuondoa tatizo la mifuko ya plastic. Marufuku iliyopigwa ni kwa ile mifuko laini ya plastic, hiivyo bado utaendelea kuiona mifuko ya plastic ambayo sio laini na yenye ukubwa wa kati na mikubwa.

Zaidi ni wakati mwingine kwa sisi wananchi kuonyesha kukereka na mifuko hiyo, kwa kurudia utamaduni wetu wa zamani wa kwenda madukani na sokoni na vikapu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom