Mifuko ya kijamii (NSSF, PPF) na kuifadhili CCM tena uchaguzi wa 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mifuko ya kijamii (NSSF, PPF) na kuifadhili CCM tena uchaguzi wa 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TajiriMutoto, Jul 25, 2012.

 1. TajiriMutoto

  TajiriMutoto Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kama upo makini utakuwa umeshaliona hili au japo kuliskia,
  Kwa kifupi mifuko ya kijamii NSSF na PPF itatumika tena kuifadhili CCM kwenye uchaguzi wa 2015. Ndio maana tumeambiwa No mafao mpaka umri wa miaka 55. Serikali ya CCM inataka kucheza na akili zetu lakini kwa hili halivumiliki.
  Hii ni serikali sio dhaifu tu bali pia ni wezi na wadhulumaji wa kubwa kwa wananchi wa kawaida kwa kile kidogo walichonacho.
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna kaukweli Ndani yake, Make hawa jamaa wana haha kusaka Mabilioni ya Kuhonga wakati wa Kampeni, na Michango yetu ndo itaenda kufanya hiyo kazi, Ila mimi tiyali nimefikia mwafaka na Mwajiri wangu hakuna tena Kupeleka makato yangu huko NSSF na badala yake nitakuwa nikiichukua mwenyewe,
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Yaani natamani mtu aanzishe topic ya NINI KIFAYIKE kuhusu hii dhuluma lakini ajabu topic zote ni za kulalamika tuu.
   
 4. m

  muchetz JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Saa ingine inabidi uwe na kichaa kutokuelewa haya mambo ambayo Chama Cha Majambazi kinafanya. Ukiangalia takwimu mbali mbali (hata za hao majambazi wenyewe) life expectancy (mtakaopata tafsiri ya kiswahili nzuri mtanisaidia) ya mtanzania ni chini ya miaka 55. Kimsingi pensheni ni kwa ajili ya kumsaidia mstaafu pale ambapo anakosa uwezo wa kuendelea kufanya kazi kutokana na uzee/ulemavu e.t.c (na hapa nisisitize sio kusaidia anao waacha anapokufa hii inakuwa secondary objective katika mazingira fulani).

  Kwa kuangalia madhumuni ya pensheni utaona serikali yenu sikivu ina inataka kufanya hiyo secondary objective kuwa ndio main objective ya pensheni. Lakini ukweli wanaouficha ni kuwa wamechukua hizo pesa za pensheni (kukidhi kiu ya anasa zao) na mashirika hayawezi tena kulipa pensheni kwa misingi yake. Sasa sababu pesa hazipo ndo wakaona waje na kisheria kandamizi ili ionekane wanakujali sana utakapo kufa(sio kuzeeka maana life expectancy inatoa facts tofauti) ili waendelee na starehe zao.

  Wafanyakazi amkeni. CCM haiko kwaajili yenu wala watoto, wajukuu zenu e.t.c. Spending spree ya serikali siyo sustainable hata wakipewa hiyo 1 bilion dollars a month(kama rais wenu alivyonukuliwa akisema), itaishia kumkamua ng'ombe damu......
  Rise your voices!!!!! Strike and strike effectively. Peaneni elimu kwanini mnafanya mgomo, then mfanye mgomo wenye malengo.

  Things are so obvious. What are you waiting for?????
   
 5. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Huu ni uwizi wa wazi wa mchana kweupe! Hatukubali
   
 6. mikonomiwili

  mikonomiwili JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wana hubiri tujiajiri sasa tutawezaje kama hata hiki wanakizuia?
  unajua mtu ukifanya kazi kama miaaka kumi naukawa namshahara mzuri ukiachakazi unawezakua nafungu lakuwezesha kujiajiri mwenyewe na kuajiri watu wengine

  lakini serikali haioni hilo inafikiria kutunyonyatu , wafanyakazi tunaonewa sana huku wafanya biashara wakiachwa huru hukukodizaozikishushwa lakini mfanyakazi ni shamba labibi la serikali

  sioni kam aserikali inanisaidia kitu chochote , hela zangu nimekatwa kwenye mshahara wangu bado unanipangia mashari ?
  huku nikilipakodi nyingi sana kuliko hata bilionea mfanyabishara

  ukipokeamshahara unalimwakodi
  ukichukua kamshaharakako kwenye ATM unalimwa kodi
  ukiendanunua vyakula , namahitaji mengine unalimwakodi
  ukiumwa unalipia hospitali ela inaenda serikalini
  ukisafiri unalipa kodi

  kilakitu mfanyakazi analipa kodi , lakini wafanyabiashara hakuna anaye wagusa
  na sasa wameleta tena hii . Na walaaniwe
   
 7. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Mungu atupe nini Jamani Watanzania sie, Wafanyakazi , Mmelogwa, hebu lianzishen Bwana na sie Wakulima Tuje Nyuma yenu Kuliondoshelea Mbali Zoga CCM
   
 8. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mahali pengi sana wafanyakazi ndo nguzo ya ukombozi wa nchi, hali hii imechukuliwa kwa miongo na miongo sasa kiasa kwamba ktk nchi zetu hizi za daraja la tatu, mtu kuwa mfanyakazi tena wa serikali ni kitu cha kujivunia, ni kama kila mtu anataka nafasi ya kuajiriwa tena na serikali yake.

  Wafanyakazi ni watu waelewa sana, japo kwa bahati mbaya ktk mazingira ya TZ inakuwa kama kwamba wafanyabiashara ndo waelewa sana kuliko wafanyakazi. Wafanyakazi wamekuwa wakifanyakazi ili mradi walipwe chao na kisha waondoke muda wa kustaafu ukifika. Wameshindwa kuchagiza mabadiliko ya uongozi ktk nchi na wamekuwa ndo washutumiwa wakubwa ktk masuala ya wizi wa mali ya umma na ufisadi, imekwenda mbali hata kuona kuwa wao kwa sasa ndo wameridhika na mfumo mbaya, maana pengine unanufaisha. Wafanyakazi wakitumiwa na wafanyabishara kweli wamemnyomnga mkulima na raia wa Tza kiaina na kinamna.

  Sasa limekuja suala la mifuko ya hifadhi ya jamii, kupitia CCM, kisha serikali na baadae bunge kupitisha mufumo ambao haukubaliki kabisa, kukaa na mafao ya wanachama hadi wafikishe miaka 55, ni uhalamia. Viongozi wa CCM ambao ndo wenye sera Nape na wenzako tuambieni hili limetoka wapi???

  Hivi kijana atasubiri afike miaka 55 ndo achukue fedha yake ambayo angefanya biashara na kujiajiri ingemtoa??? achukue akiwa mzee ili iweje??? kulifanyika kosa chini ya CCM la kuongeza umri wa kustafu huku kiwango cha maisha ya Mtazania kimeshuka, wafanyakazi kama kawaida yao walinyamaza kama hawaoni vijana wanakosa ajira huko wao wanajirudisha kwenye ajira hizo hizo za vijana kwa milango ya nyuma. Wakati umri wa kuishi umepungua hadi miaka 47, CCM chini ya Mkapa ikabandisha umri wa kustaafu hado miaka 60, aibu. Sasa kijana hana ajira harafu mafao yake aliyopata kwenye kiajria cha miaka 2 au 3 inabidi asubiri kwa zaidi ya miaka 25-30 ili aje kukipata. Suala ni kwamba inawezekana kweli??? je atalipwa mfano 200,000/- yake ya leo baada ya miaka 25-30 kama 200,000/- au itakuwa imepanda thamani hadi kuwa milioni 200 baada ya miaka hiyo???

  Mheshimiwa Mwenyekiti, Muswada pia unapendekeza kuongeza kifungu kipya cha 27(a) ili kumwezesha mwajiliwa ambaye baada ya kufikia umri wa kustaafu kwa lazima na bado anaendelea kutoa michango yake katika Mfuko kuwa ana stahili ya kulipwa bonus-- Huyu anatoka wapi???? Vijana kazi watapata lini? na wapi? CCM JAMANI KUWENI NA UTU​

  Suala hili halikwahusisha wadau na halikuwa wazi kama inavyostahili, tusije ambiwa wadau ni fulani na fulani watu 100 kuwakilisha wafanyakazi zaidi ya milioni 3 kwa serikali na sekta binafsi.


  Wafanyakazi kwa sheria hii dhalimu ya CCM na serikali yake, tunapaswa tupinge kwa nguvu zote sheria hii ili iondolewe mara moja, tusisubiri eti haki mwaka kesho au kesho kutwa, hawa wezi watakuwa wamefanikiwa kuiba haki yetu kwa miaka 2 au 3, ambayo pia haikubaliki. Kwanza tunaomba wabunge wa wananchi waanze kulifanyika kazi bunge hili hili la bajeti.

  Vijana tunahitaji mitaji na hela zetu ndo mitaaji sahihi kujikwamua kimaisha, sio lazima tumkopeshe NSSF na wenzake kufanya mambo ambayo hatukukubaliana wakati wa kuingia mkataba, hata faida ya uwekezaji wao haiji kwa wadau, ni kulipana mishahara wao sio kumpatia mwanachama kipato.

  Nawasilisha
   
 9. stineriga

  stineriga JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 2,033
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  yule kiongozi wa shirikisho wa chama cha wafanyakazi, mbona amepiga plasta mdomo kwenye hili???
   
 10. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Nashangaa, Tunataka Muongozo tulizanzishe...
  I hope tungepewa Nyoyo za Wa France
   
 11. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nani akupe muongozo ni kukaa barabarani tu mkuu sisi wenyewe ndio wakupeana muongozo ili tukakae tahiriri squire viwanja vya NBC pale posta.
   
 12. d

  da50v1 Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wabunge ndio waliopitisha wakishirikiana na wadau mbalimbali,
  so wakulaumiwa ni wabunge wetu kwakupitisha sheria mbovu kama hii, wote wa CCM na upinzani walipitisha
  na Raisi amekwisha saini.
  Jitihada zaidi zinahitajika ili kudai haki yetu kwasababu miaka 60 ni mingi sana
   
 13. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  mi nilishatoa hela yangu yote.Nashangaa hili ndilo lilikuwa marketing strategy ya NSSF na PPF, kupatikana hela kwa haraka.Sasa kwa vile wameshaingia katika miradi hovyo, na kuleta hasara, wameshajua kuwa rate ya kutoka watu inazidi ile ya kuingia sasa wanaweweseka.

  Nadhani mfanyakazi anaweza ingia mkataba na mwajiri apewe hela kamili ikiwa na hiyo ya pension halafu akaweke katika saccos, au Bank.Mkataba uwe wa muda mfupi au hata kama kibarua.

  Dunia nzima huwa serikai hutumia mfuko huo kuchezea hela,ila hali huwa mbaya zaidi fedha nyingi zikishindikana kupatikana, huku idadi ya wastaafu ikizidi kuwa kubwa ukilinganisha na matumizi na michango ya wanachama.Ni full Pyramid wanachofanya sehemu nyingi duniani.

  Cha kushangaza ni kwamba kuna hela nyingi sana ambazo huwa wanachama hawajadai wala hawatakuja dai kwa vile ni kidogo na wanachama hawaoni sababu za kuzifuata.Wapow atu ambao hawawezi fuata waajiri wao ambao kampunizao zimekufa au waliibiana ili wakawajazie fomu.wapo wengine wamekufa bila kuwa na chochote cha kuweza wasaidia warithi wao kufuatilia hizo mafao.Kwa vile hawa jamaa hawaja invest katika statistics ambazo zinaongozwa kwa live data, wameishiwa huku wakiwa na hela kibao zitakazobaki forever.Kweli serikali iliyoo ilijiandaa kwa kila nyanja kuikamata hii nchi na kuifanya ilivyo.Juzi tuu dau katangaza kuwa wana hela ya kutosha lipa wanachama wote mara wahitajipo hela,huku wakiwa na serikali katika deal la kuja ziba baada ya watu kujisahau na kukimbilia kujiunga.


  pamoja na wao kudhnai kuwa waasave ila zozi zima wanaloliendesha halina sana tofauti na upatu ambao hutegemea walioingia kuwapa waliotangaulia.Ni kwmaba wameahamisha deni tuu ,huku wakijua kuwa kuna kipindi kitafika umri wa taifa ukibadilika basi kila kitu kita collapse. Kipindi kinachofuatiwa na vijana wengi kuweka hela zaidi ya wazee kutoka then wazee watapata kila kitu vizuri,sasa kiazazi kifuatacho kitakuwa ,vijana hao watakuwa wazee na wanao wanaweza kuwa achache kutoakana na uzazi wa mpango, kujiajiri zaidi, kuchagua mifuko etc then huku pakiw ana matumizi kama haya mfumo unacolapse.
   
 14. a

  artorius JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 758
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Now its the time to dramatise this shameful condition instead of complaining.What should be the way forward?
   
 15. ruhi

  ruhi JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 1,409
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Kwa hili lazima serikali atashindwa tuu,naombeni mabomu niende bungeni mie,mnachelewa sana
   
 16. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Anzisha basi wewe.
   
 17. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Wala usiwe na shaka mkuu. najipanga muda si mrefu utanisikia na nita ku'tagg.
   
 18. ruhi

  ruhi JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 1,409
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Mwenye wazo anipigie kwa namba 0758497937
   
 19. denyol

  denyol Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ndio maana naamini mpango huu utafanikiwa, mpaka sasa hakuna wayforward yoyote zaidi ya malalamiko yasiyokuwa na ushirikiano -un-centered- kazi ipo
   
 20. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  anzisha weye basi
   
Loading...