Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 8,937
- 25,279
Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru amesema kabla mifuko ya hifadhi ya jamii haijaanza kujenga viwanda, wataalamu wanapaswa kutengeneza mpango mkakati ili kutoathiri malipo kwa wanachama.
Mafuru alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kutoa tuzo za Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), akifafanua mapendekezo ya Rais John Magufuli kwa mifuko hiyo kuacha kujielekeza kwenye ujenzi wa majengo, badala yake ifanye hivyo kwa viwanda.
Akizindua jengo la PPF Mjini Arusha Mei, Rais Magufuli aliwataka viongozi na wataalamu wa mifuko hiyo kuanza kujenga viwanda ambavyo vitakuwa na manufaa kwa Watanzania hasa ajira kwa vijana.
Muda mfupi baada ya pendekezo hilo, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulitoa mkopo wa Dola 2.1 milioni za Marekani kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa kiwanda cha viuatilifu Kibaha mkoani Pwani. Kiwanda hicho kinamilikiwa na Shirika la Maendeleo Taifa (NDC).
Chanzo: Mwananchi