MIFUKO YA JAMII IMARA KIFEDHA HADI 2085.

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,221
2,000
Katika gazeti la Habari leo , lililo toka leo kuna habari ya mifuko ya jamii kuwa iko Imara kifedha hadi 2085.

Hii inadhihirisha watu kuwa kina Dr Dau na wenzake walikuwa wanafanya kazi zao vizuri sana, na mengi yaliyosemwa tena hasa kuhusu Dau, inadhihirisha yalikuwa maneno ya uzushi na unafiki, zilizokuwa na hisia za kumharibia jina kiongozi mwenye uzoefu mzuri na mtanzania anayeipenda nchi yake.

La kushangaza ni kuwa miezi minane iliyopita , magazeti yalim kashifu kuwa kaacha FUPA NSSF. Leo tunaona lile fupa kube limeja minofu tena minono sana.

Nina imani NSSF itaendelea kuwa na sifa nzuri ya kikazi na uwekezaji, kwani aliyepokea usukani hapo nssf , yuko mbioni kulisoma vizuri taasisi na kujitayarisha kuendelea kulipaza kimaendeleo. Japokuwa katika hii miezi 9 toka aondoke ndugu Dau, hakuna miradi mipya bali wanaedelea kuisimamia vizuri miradi aliyoicha ndugu Dau.

IMG-20161221-WA0001.jpg
IMG-20161221-WA0003.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom