Tetesi: Mifuko ya hifadhi ya jamii kwa Watumishi kubakizwa miwili

Mimi binafsi nitafurahi sana ikiunganishwa, kuna watu wangu wa karibu nawajua wanateseka sana kwa manyanyaso ya mfuko mmoja siutaji ila ni jambo jema.
Katika mifuko hii pia imekuwa km kichaka cha kujificha....
Probably itakuwa ni ppf! Huu mfuko umekaa kihuni mno! Kuna kampuni moja kubwa huko arusha ambayo wafanyakazi wake wanalazimishwa kujiunga ppf tu! Halafu sasa fedha wanazokatwa zinatumika kuwakopesha kwa riba kubwa ya 30%! Dhamana ni akiba yako ya ppf, na unapoacha au kuachishwa kazi basi tajiri ana uwezo wa kukukata direct kutoka kwenye hifadhi yako maana pia yeye ndiye anayekulipa ppf yako! Yaani hadi penalties nyingine kama za low performance zinakatwa kwenye ppf yako! Sasa unashindwa kujua kama huo mfuko ni wa tajiri(mmiliki wa kampuni) au serikali?
 
TANGU KITAMBO HZ TETESI, HATA JUZI KALIZUNGUMZIA KAGERA.

ILA ITALETA SHDA NA HUDUMA ZA HFADH ZTAKUWA MBOVU, LABDA ANGESEMA MIFUKO IWE MIWILI ILA IWE NA UHURU WA WA KUSAJILI MEMBERS. IWE PRIVATE AU GVT.

HATA HVYO, HUU MFUMO ANAOLETA NI WA KIZAMANI, NI SAWA NA KWENDA MBELE HATUA 5 UNARUD HATUA 7

KWA MUJIBU WA TETESI NI KWAMBA NSSF, GEPF NA PPF ITAUNGANISHWA KUWA MFUKO MMOJA (NSSF) HALAFU LAPF+PSPF NI PSPF
Nawezaje kukopa pesa walau kidogo pspf, mimi ni daktari nina miezi 6 kazin
 
Hakuna haja ya kua na utitiri wa mifuko ya hifadhi ya jamii wakati yao kazi ni ile ile ya kutoa mafao mbali mbali na pensheni, hata hii mifuko ya afya ya jamii yote ijumuishwe kwenye huo mfuko mmoja mkubwa, tuokoe mishahara kwa kulipa utitiri wa wakurugenzi
 
kwa mawazo yangu naona ni sawa ili kupunguza gharama nyingi za uendeshaji bora kuwe na mifuko michache yenye tija
 
Ushindani ni muhimu sana, sasa serikali itakusanya pesa vizuri ila huduma kwa wafanyakazi na vile vibonus sijui mafao ya uzazi na mikopo ya kuanzia maisha wasahau.
Hivi uliwaza nini hadi ukachagua hiyo avatar, thought shapes reality, hiyo avatar inaakisi jinsi ubongo wako unavyofanya kazi
 
Itaua ufanisi pamoja na uendeshaji wa mifuko kwa ubora kuunganusha mifuko kuwa mmoja ni ishara ya kuifanya kuwa kama wizara kitu ambacho kitatufanya turud tulikotoka! Last suala la kuunganisha linahitaji critical negotiations especially kwa maeneo na mikataba ilivyoingia!
 
Itaongeza ufanisi na punguza garama.Tuangalie mashirika mengine pia yaunganishwe kupunguza dublication na garama.
 
ila ni njia ya ku create emplyment mkuu tuangalie wana familia
Watu hawajui tu. Kuajiri watu wengi kunafanya mzunguko wa pesa uwe mkubwa na kukuza uchumi. Serikali ikiiajiri watu wachache ni mbaya kwa uchumi tofauti na shirika binafsi.
 
Hizo tetesi ni za kweli kabisa.
Ni suala la muda tu, kuna mswaada wa dharula wa marekebisho sheria ya mifuko ya jamii utapekwa bungeni wakati wowote ili kukidhi hilo takwa la rais.

Hatua hiyo itakuwa ni nafuu kwa serikali ili kupunguza gharama za uendeshaji LAKINI ni hasara kubwa kwa wafanyakazi na ni janga kwa taifa.
 
Kuna tetesi nmezipata mahali ingawa sijathibitisha kama ni kweli. Jumomosi nilikuwa nmekaa na mchumi mmoja mahali fulani(jina la sehemu na mhusika nahifadhi).

Inasemekana bwana mkubwa amepanga kuunganisha kama sio kuvunja mashirika yote ya hifadhi ya jamii na kubakiza moja la serikali na moja la binafsi, pia inasemekana wakurugenzi wa haya mashirika yote ya hifadhi walishaitwa na kupewa huo utaratibu na kuambiwa kuwa hiyo ni amri na ole wao waje kulopoka huku mtaani.

Watumishi wote wa serikali watalazimika kuhifadhi fedha zao kwenye mfuko wa hifadhi wa serikali(ni lazima) na watumishi wa sekta binafsi wanaweza kuchagua ni mfuko gani wahifadhi hela zao.

Kuna miradi iliyokuwa inatekelezwa na mashirika hayo miingine inaonekana kusimama, mkulu kasema hata serikali inaweza kuiendesha. Kama ni kweli hili swala linaweza kuathiri uchumi?
Umbea wa kiwango cha makinikia
 
Back
Top Bottom