Mifuko laini ya plastiki kupigwa marufuku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mifuko laini ya plastiki kupigwa marufuku

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagwell, Oct 3, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zaina Malongo
  SERIKALI inafikiria kupiga marufuku matumizi ya mifuko laini ya plastiki Tanzania bara .
  Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira), Dk Terezya Huvisa wakati alipozungumza kwenye Kituo cha Radio Clouds jijini Dar es Salaam juzi.

  Terezya alisema wadau wa kujadili suala hilo ni wa kutoka ofisi yake, Wizara ya Fedha na Uchumi na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira nchini (Nemc).
  “Wenzetu Zanzibar wameweza kupiga marufuku kwa sababu hawana viwanda, lakini Tanzania bara ina viwanda ambavyo vimeanzishwa kisheria,”alisema na kuongeza
  “Sisi tuna viwanda ambavyo vimeanzishwa kabla ya sheria ya mazingira,hivyo lazima tukae tujadili tujue tunaanzia wapi”, alisema.

  Alisema watatekeleza bila kuathiri mambo mengine, kwani Tanzania bara mifuko hiyo inatumika katika matumizi mbalimbali kama hospitali pamoja na vifungashio.

  Upande wa Msemaji wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(NEMC),Geogre Adrian aliwataka wananchi kuwa na ushirikiano wakati wanapotumia mifuko hiyo kwa kuangali wenye viwango .

  Alisema kanuni za mazingira nchini, zimeshaandaliwa na tayari imewasilishwa kwa waziri husika kwa ajili ya kusainiwa ili iweze kutumika.

  “Waziri alipozungumza bungeni kuhusu suala la mifuko ya plastiki, tuliandaa muswada na kupeleka katika wizara inayosimamia mazingira,”alisema

  Kauli ya kukatazwa kwa mifuko ya plastiki Tanzania bara imekuja baada ya Zanziabar kuzuia mifuko ya plastiki kutoka bara.  Hata bado naona tutazuia vingi tu kutoka bara
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Badala ya kupiga marufuku, serikali ingetoza kodi kubwa!
   
 3. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Mbona hii mifuko ilishapigwa marufuku muda mrefu tu! Usanii TZ hauwezi kwisha kama kwa vazi la Taifa.
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Nashangaa kwa kweli....ipigwe marufuku mara ngapi??
   
 5. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Porojo tu kama za wenzake! Amuulize Tibaijuka etc
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Inapigwa marufuku mara ya ngapi? Somebody somewhere has christmas plans in their heads. Kuwatia joto wenye kutengeneza ya plastic watoe hela na wenye ya karatasi nao watoe hela ya kyongezea nguvu agizo.
  Welcome to season 2 kwa hisani ya vpo na nemc.
   
 7. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kila kitu ni upepo...
  Nakumbuka walipopiga marufuku walikuja na strategi nzuri sana....viwanda marufuku kuzalisha (japo waliruhusu uzalishaji wa mifuko hiyo lakini iwe na microns kubwa). Viwanda vya wadosi viliendelea tu kuzalisha hizi takataka. Jamaa wa Nemc walipokuwa wakijaribu kutembelea viwanda husika walivurumishwa vibaya mno, tena na waswahili tu na wala si wadosi. Na biashara ndo ikaishia hapo.

  Kama "watapiga marufuku" sasa basi itakuwa ni utekelezaji wa marufuku iliyopigwa takribani miaka saba iliyopita.
   
 8. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,098
  Likes Received: 11,241
  Trophy Points: 280
  Wazuie na vumbi kutimka, nalo ni kero kweli kweli.
   
 9. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  dhaifu alipiga marufuku mara tu alipoapishwa kuwa rais dhaifu
   
 10. peri

  peri JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  umenena vyema mkuu, waongeze kodi na wafute kodi mifuko mingine isiyo haribu mazingira.
   
 11. m

  muchetz JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Umeona ehee. Mi nasema usanii full hapa. Yaani haka kanchi bana. Kuanzia raisi mpaka mjumbe wa nyumba kumi, mpaka mwananchi ni usaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii mtupu. Liwalo na liwe. Kanyaga twende!!!
   
 12. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,968
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Shangaa na wewe bwana hakimu. Hii mifuko ilishapigwa stop longi, sasa ipigwe marufuku mara ngapi? Ubabaishaji bongo hautakwisha.
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mifuko ya plastic ilishapigwa marufuku wakati Prod Mwandosya akiwa waziri wa mazingira, lakini bado ipo. Huwezi kusema unapiga marufuku kitu wakati huo huo unachokuwa kodi itakanayo na mauzo ya hicho unachopiga marufuku. Hapa serikali na hasa huyo waziri wa mazingira should come up with a practicle solution na sio hizi cheap headlines. Alianza kubomoa nyumba zimemshinda sasa anarukia kwenye mifuko ya plastic kichwa kichwa.

  Atoze kodi kubwa kwenye plastic bags, na afute kodi kwenye paper bags. Hela watakazopata kutokana na tax increament wanaweza kutumia kwa kukuza mazingira - mpango utajitegemea wenye bila kuzungusha bakuli kwa wafadhili.
   
 14. Gedeli

  Gedeli JF Gold Member

  #14
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 452
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Tanzania sina hamu nayo kabisa hii mifuko ilipigwa marufuku haukuisha mwezi wakaja na jibu kuwa viwanda vimebolesha uegenezaji wa hiyo mifuko lakini ukweli ni kuwa hakuna kilichobadilika
   
 15. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mbona ilishapigwa marufuku siku nyingi.Ni usanii mtupu unaoendelea.Serikali hii haiwezi kusimamia lolote likafanikiwa.
   
Loading...