Mifugo ya wahamiaji haramu yapigwa chapa kwa magendo Biharamulo

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
chapa(1).jpg

Siku chache baada ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kuhimiza operesheni ya kuondoa mifugo kwenye misitu ya hifadhi na mapori ya akiba hapa nchini imeibuka biashara haramu ya kupiga chapa mifugo ya wahamiaji haramu kwa njia ya magendo hali iliyosababisha migogoro kati ya wafugaji na watendaji wa serikali ya kijiji cha nyabugombe kata ya nyakahula wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera.

Mgogoro huo umeibuka katika zoezi la kitaifa la kupiga chapa mifugo kwa kila wilaya ambapo wilaya ya Biharamulo kata ya Nyakahula zoezi hilo limefanyika katika kijiji cha Nyabugombe ambapo wafugaji wamelalamikia utendaji kazi wa maafisa wa serikali wakidaiwa kupiga chapa mifugo ya wahamiaji haramu kutoka nje ya nchi kwa njia za magendo kutokana na mianya ya rushwa.

Akijibu tuhuma za kupokea rushwa katika zoezi la upigaji chapa mifugo mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nyabugomba Bw.Williamson Mugasa amekanusha vikali kuhusishwa na rushwa huku akishindwa kubainisha uhalali wa mifugo iliyotoka nje ya kijiji chake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo Bi.Wende Ng,ahala amesema kuwa ofisi yake imelenga kupiga chapa mifugo aina ya ng,ombe 132,900 na kusema kwamba wilaya ya Biharamulo haina mifugo ya wahamiaji haramu.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom