Mifano ya uongozi na maendeleo anayoitoa Lissu kutoka Ulaya ni kujitoa fahamu au ni ushamba

Mchimwachimego

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
358
271
Tokea kampeni zimeanza nimekuwa nikisikiliza sera za mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu tundulisu lakini mara nyingi akitoa hoja zake lazima aseme "NDIVYO ULAYA WANAFANYA" amekuwa akiyasema akitolea mfano wa bima ya afya na utawala wa majimbo, NK: Nimewaza sana ni ushamba, ujinga au limbukeni ya kutaka urais hivyo anataka kuwaaminisha watu kuwa bila kuiga alichokifanya mzungu hakuna uongozi wala hakuna maendeleo Afrika.

Ubaya mkubwa anaoufanya ni kutolea mifano ile tu inayoiona kwake ni bora anaacha ile mibaya ambayo nako ipo, mfano: Kwenye nchi aliyokwenda kupata msaada wa ukimbizi inaongozwa na "MFALME" wote tunajua utawala wa kifalme urithiwa na hakuna demokrasia ya kupata mfalme,inamaana nchi yote ya Ubelgiji haina mtu anayefaa kuwa mfalme kwanini hasitueleze na madhara ya utawala huu na ikumbukwe mfalme leopard wa Belgium aliua malaki ya wakongomani haya hayaoni.

Sisi kama taiga tunaitaji kiongozi atakayezalisha maendeleo kwa kuibua mawazo miongoni mwetu na ndio njia pekee itakayotutoa kutoka kuwa tegemezi wa tecnolojia na mawazo kutoka ulaya ni lini tutaunda vitu vyetu wenyewe kama nchi Uhuru anaohubiri hauwezi kuwa wa kweli kama tutamtegemea mzungu kwa kila jambo.

Namalizia kwa kuwashauri watanzania kwamba mataifa yote duniani yaliyoendelea yalipata viongozi majasiri na imara wasiokubali kuyumbishwa na wale wasiowatakia maendeleo kama MAO wa China,FIDEL CASTO wa quba na wengine wengi.

Tuachane na ushabiki wa kisiasa "NO PAIN NO GAIN" MUNGU aliamua kuturudishia heshima kwa kutuletea JPM rais mwnye misimamo isiyoyumbishwa. Lissu ni wakili daima watu hawa utetea MTU wa aina yoyote awe amefanya kosa au lah yeye anachotaka ni ushindi na WAZUNGU hupenda watu hawa kwa sababu wana tabia ya kuheshimu kila lililopo kwenye mikataba hata kama uwe wa kinyonyaji huyu hatufai ataturudisha nyuma kwa kufuata mikataba ambayo ni ya kinyonyaji na kutetea kuwa tuliisaini wenyewe.

Mikataba yote ya kimataifa tuliundiwa waafrika hivyo kosa hili watanzania muliepuke , Tumchague MAGUFULI amejitoa na kuonyesha kuwa sio kila anachokileta mzungu ni chakumeza "THERE IS NO FREE FOOD FROM ANYONE" amekataa sheria zao za mazingira anatujengea bwawa la umeme, amekataa kila mladi ufanywe na wakandarasi kutoka nje,amekataa kufungia ndani watu kisa korona ,amekataa kwenda ulaya kujipendekeza "BINADAMU WOTE NI SAWA" hata wao wanatuitaji sisi,amekataa kuaminisha umma kuwa jeshi letu ni imara limejenga ukuta melelani na ikulu, amekataa kwamba watanzania hawawezi kufanya vitu vya maendeleo wenyewe, asanteni na karibuni.
 
Sema tu una chuki binafsi na Lissu! Huna hoja hapo mbona hata kabla Lissu hajaitaja Ulaya tayari mgombea wenu wa CCM alishatangaza kuwa ataifanya Tanzania kuwa kama Ulaya! Je huyo nae ni mshamba na Limbukeni? Je huyo nae kajitoa ufahamu?? After all, lazima tukubali sisi watu wa nchi zinazoendelea hatuna ujanja wa kutoiga au kuchukuwa mifano toka nchi zilizoendelea! Tunaomba huko mpaka misaada ya madawa na elimu sembuse mifumo ya kiuongozi!? Acha kuvizia watu hoja za Lissu hata CCM tu wameshindwa, wamebaki kuvurumisha vijembe na kejeli. Mwaka huu tutasikia mengi mpaka mmejikuta mnajitukana wenyewe mkizani mnamtukana Lissu!
 
Kwani Magufuli anaposema anataka kuifanya Tanzania kuwa ulaya ni ushamba au ni ulimbukeni?
 
Mfano wa maendeleo tunyofanya yameanzia wapi?

Madege, Mameli, madaraja, mabarabara, makompyuta nk. Mifumo ya utawala vyote hivyo vimeanzia wapi?
Kusema tuwe kama ulaya shida ni nini labda tuseme kama Somalia ungefurahi!
 
Back
Top Bottom