Nini maana ya uwekezaji kukua kwa asilimia 400.Tafsiri yake ni nini kwa Mtanzania.Kwa tafsiri yangu ndogo sana nafikiri, uwekezaji ukikua kwani kuna ulazima wa kuwa na tazo? Kuna ulazima wa kupandisha petroli kila kukicha kwa kuongeza kodi za kumgandamiza Mtanzania maskini,kwa kisingizio cha kujenga madispensari na mabarabara? mara makodi ya majengo tena yanayotozwa kwa lazima kila mwezi ukinunua umeme bila kujua ukomo wake, na makodi mengine lukuki.Kwanini unateseka nchi yako kupata maendeleo,
Wewe unatokea nchi gani?
Hii miradi itamwajiri hata ndg yako kama sio wewe
Kama huna ndugu hata jirani yako ataajiriwa pia,
Why can't you positive to your country?
Mimi nilitegemea kwa hiyo asilimia kubwa hivyo,uwekezaji huo uweze kuwanufaisha wananchi kwa kuwaondolea makodi na matozo yanayobebwa na watanzania wengi walio maskini kwa maumivu makali, angalau basi hali ya maisha yashuke na unafuu uonekane sio kwa nadharia bali kwa uhalisia.
Nafikiri tufike mahali viongozi wetu watuambie hakuna tena kukatwa matozo kwenye miamala ya simu, matozo unaponunua umeme, mafuta ya kula yameshushwa kodi kwa sababu uwekezaji umechukua nafasi hiyo kutokana na uchumi kupandishwa na wawekezaji.
Mimi ukiniambia uwekezaji umepanda kwa 400% wakati hali tunayoishi nayo ya shida iko palepale statement yako hiyo sitakaa nikuelewe milele.Nitakuelewa tu utakaponiambia makodi,matozo na makodi mengine ya petroli yameondolewa au yameshushwa sana na serikali kutokana na uwekezaji mkubwa.
Nilimsikia mbunge mmoja akisema,kwenye petroli peke yake kuna kodi sio chini ya 19.Hesabu kuanzia 1,2,3,mpaka 19.Hizi ni kodi mwananchi analipa.Halafu unasimama unasema uwekezaji umepanda kwa hiyo asilimia uliyosema mleta mada.Bado sijakuelewa una maanisha nini.