Miezi sita bila Dkt Magufuli: Watanzania waliisoma na kuielewa dhamira ya Rais Magufuli iliyotiririka kama maji

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
932
2,803
MIEZI SITA BILA JPM: WATANZANIA WALIISOMA NA KUIELEWA DHAMIRA YA RAIS MAGUFULI ILIYOTIRIRIKA KAMA MAJI.

Leo 10:15hrs 19/09/2021

Rais John Magufuli, alikuwa Mzalendo mwenye mapenzi ya kweli kwa Nchi yake,hakuijua China,Marekani wala Ulaya toka achaguliwe, yeye ni Morogoro, Arusha, Iringa, Tanga, Mbeya, Songea, Mtwara, Lindi, Rukwa, Sumbawanga anarudi Moshi,Singida anaingia Dodoma kamaliza,yaani yeye alidili kwa ukaribu Sana na watu wake, alitaka kujua kila tatizo la mtu ili atatue hapo hapo,alitamani yeye akinywa chai asubuhi kila Mtanzania anywe chai, yeye akila mchana kila Mtanzania ale chakula mchana,yeye akila chakula usiku basi kila Mtanzania ale chakula usiku, alikuwa msikivu, mvumilivu, mwenye huruma, upendo, rafiki wa wanyonge na wanaoonewa. Alisimama kwa waliovunjika moyo ili kuwapa tumaini jipya,hakuona shida kutoa mpaka senti ya mwisho kuwapa wenye uhitaji,yeye aliishi ufukara kama sisi kujua shida zetu,

Japokuwa alikuwa mwenye mamlaka ya juu kuliko Mtanzania yeyote lakini alishuka kwa unyenyekevu na kula na Wananchi chakula wanacho kula wao,hakuwasahau alipotoka,vijana wa enzi yake aliocheza nao akanywa nao kahawa,kila alipopita alitenda mema,akawafuta walioonewa machozi yao,akawafungua wafugwa wao,aliingia magerezani kuwasalimu wafugwa,ubinadamu ndio hisia zake,akawasamehe waliokosea,Wimbo wa upendo uliibwa machoni pake,rohoni na kwenye utumishi uliotukuka,hakujilimbikizia mali,alijua tulikuja tupu tutaondoka tupu,alikuwa mwenye utani,matani kidogo, masihara kidogo ili tu kuwaonyesha ni Mimi yule yule sikubadilika,Usingizi hakupata akiiwazia Tanzania,asubuhi aliamka na saa mbili asubuhi alianza kuzindua miradi aliyoagiza ijengwe kwa manufaa ya Watanzania wa leo,kesho na kesho kutwa,alikuwa Baba mwema sana.

-Rais Magufuli alikuwa kiongozi mwenye akili nyingi haijawai kutokea katika taifa la Tanzania.

1. Rais John Magufuli alikuwa na shahada ya elimu ya sayansi yaani Bachelor katika somo la namba na kemia kwa kizungu tunasema Bachelor of Science of Education in Mathematics and chemistry,kwa hiyo unapozungumzia suala la namba yaani hesabu kwa Rais Magufuli zililala yaani, kemia hii ya kuchanganya madawa na makemikali ndio huwezi kumdanganya kitu,hilo tuliona alipoongelea suala la Ukimwi kutokuwa na njano,aliongea suala hilo akiwa kijijini Chato lakini walijibu wazungu wakiwa London,New York na Washington,na haikutosha Serikali ya Washington ikapanda kwenye mimbali ya hard talk na cnn kujibu sentence moja tu ya Rais John Magufuli aliyoitoa kijijini Chato,hii ndio akili tunayoitaka kwa Watanzania kuchalenge Mambo makubwa ya dunia na tumeona tokeo,leo chanjo ya Ukimwi imekuja baada ya Rais Magufuli kuwachalenji.

2. Rais Magufuli alikuwa na shahada ya uzamili katika fani ya kemia kwa kizungu wanaita masters of science in chemistry,kwa hiyo unapozungumzia wakemia duniani basi lazima umzungumzie na huyu mwamba.Pia ana shahada ya uzamivu katika fani ya kemia tena,kwa kizungu wanaita PhD in Chemistry,basi unapo zungumzia kuhusiana na sayansi ya kemia kwa kizungu chemistry yoyote hapo ndio imelala kwa Rais John Magufuli.

3. Sasa basi Rais John Magufuli ukimwangalia vizuri na kutafakari kwa kina utakuja kugundua kwamba alikuwa na akili nyingi mno za kuzaliwa nazo,utakuja kugundua alikuwa na kipaji cha uongozi yaani karama ya uongozi,alikuwa na kipaji cha kusimamia,alikuwa na kipaji cha kuyaelewa mambo kwa uharaka kwa speed ya 5G na kuyachukulia hatua stahiki,alikuwa na hekima,Hekima ndio inabeba mazagazaga yote,ndani ya hekima kuna kila kitu,ndani ya hekima kuna akili za kupambanua na kutafakari mambo,ndani ya hekima kuna akili za kutatua matatizo mbalimbali,ndani ya hekima kuna ucha Mungu,ndani ya hekima ndimo kuna akili za kutambua kwamba hakuna jambo linaloshindikana mbele za Mungu,ndani ya hekima kuna ujuzi na Maarifa mbalimbali,ndani ya hekima kuna busara,ndani ya hekima kuna akili za kuyaelewa mambo ambayo hujasomea darasani au popote,Rais John Magufuli alitumia hekima hiyo kumwomba Mungu na kuwasihi Watanzania tumwombe Mungu ili majanga yaondoke katika uso wa Tanzania.

4. Nasema hivyo kwa sababu Rais John Magufuli hakusomea masomo ya sanaa,wala siasa wala Uongozi,lakini alijua vitu vingi mnoo,hauwezi kumdanganya,alijua na kuielewa historia,alijua na kuielewa sheria na ipo kichwani,mambo ya utalii ndio usiseme alijua vilivyo,alijua kuongoza,aliijua geographia ya dunia nzima,alijua kusimamia majukumu,alijua na kuuelewa uchumi,alijua na kuilewa vilivyo elimu ya fedha,alijua na kuyaelewa mambo ya kodi,alijua na kuzielewa vizuri mbinu zote na janja janja za mafisadi,alijua na kuzielewa vilivyo mbinu zote za mebeberu laghai na makwepa kodi,alijua na kuelewa vizuri janjajanja zote za mafisadi, watakatishaji wa fedha, majizi,alijua na kuyaelewa mambo ya mapato na matumizi,Mambo ya kubajeti hapo ndio kabisa Rais Magufuli alikuwa makini mnooooo.

5.Rais John Magufuli alikuwa kiongozi anayeweza kuongoza (lead), kufuatilia (monitoring) na kusimamia (manage) viongozi wa kila wizara kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu na kwa kujituma bila kuchoka.

6.Wizara ya afya yumo, wizara ya ujenzi yumo, wizara ya elimu yumo, wizara ya kilimo yumo, wizara ya ulinzi yumo, Kwenye Maliasili yumo, TRA yumo, Bandarini yumo, TAZARA yumo, Michezo yumo, wizara ya fedha yumo, kwenye miradi yumo, kwenye dini yumo, kwenye hekima yumo, kwenye umeme yumo, kwenye sheria yumo, kwenye lugha yumo, kwenye chemistry yumo, kwenye mathematics yumo, kwenye madawa yumo. Kuishinda corona yumo.

7.Kuyazidi kete mabeberu yumo, kugundua mbinu wanazotumia watu wanaokwepa kodi yumo, kuweka mbinu bora za kuzuia wakwepa kodi yumo, kuyashinda mabeberu kupambana na corona yumo,kuzungumza lugha za kila aina na makabila yote yumo na alifanya hivi kila alivyosimama kuhutubia au kusalimia Wananchi alisalimu kwa lugha zote na dini zote.

8.Kukusanya kodi za kuendeshea serikali kwa ufanisi yumo, kutafuta fedha za kuendeshea serikali bila kutegemea mabeberu wala tozo yumo,Kusimamia miradi kwa ufanisi na kuzuia ubadhilifu na ufisadi wa pesa za miradi yumo.

9. Kuboresha viwanja vyetu vya ndege kama ulaya yumo, kuwaza jinsi ya kufanya watanzania wote watibiwe hapahapa Tanzania yumo,Kuyazidi mabeberu kete yumo,Kupiga stori za maendeleo na wananchi yumo.

10.Kugundua janja janja za mabeberu na mafilisi katika kuiba rasilimali za nchi yumo,kuyapa displine mabeberu ambayo yanakwepa kodi na kufanya unyonyaji wa rasilimali zetu yumo.

11.Kutokuyaogopa mabeberu yumo,Kugundua matakatishaji ya fedha za miradi za serikali yumo, kugundua majitu yanayotaka kupata au kutoa rushwa yumo, kutoa elimu bure yumo, kujenga hosteli vyuoni yumo, kujenga babara za juu na za rami yumo.

12.Kugundua mbinu wanazotumia majizi kutuibia mapato bandarini yumo. Kuyazuia majizi yasituibie mapato bandarini yumo, Kugundua mbinu wanazotumia majizi kutuibia madini yumo, kuyazuia majizi yasituibie madini yetu yumo.

-Tathmini ya wapiga kura Mwaka 2020 walisema wanampigia kura Rais Dk Magufuli kutokana na mambo yafuatayo :

1.Uchapakazi wake na ufuatiliaji uliotukuka

2.Ubunifu wa mifumo mbalimbali i.e malipo serikalini

3. Ujasiri wa utekelezaji wa maamuzi i.e miradi mikubwa kufufua shirika la ndege etc

4.Maono yake wakirejea suala la korona,

5.Uwezo mkubwa wa kushughulikia masuala ya kimaadili serikalini

6. Miradi ya kitaifa aliyoianzisha akamilishe yeye

7.Nsimamo wake usioyumba kwenye masuala mazito ya kitaifa.

8. Maamuzi ya papo kwa papo kwenye field i.e ziara za kutatua kero

9.Muwazi na Mkweli

10. Amejenga ushawishi wa kimataifa kama Rais mwenye kujiamini na wa kipekee mzalendo wa nchi yake na Afrika. Hivi ni baadhi ya vigezo walivyotumia baadhi ya wananchi kumpigia kura Dk.Magufuli,lakini wananchi walikiri pia kuwepo na changamoto kadhaa za uongozi,kiuchumi na kijamii wanazoamini kipindi kijacho angeweza kuzikabili kutokana na misingi ya kiuchumi aliyoijenga mfano Bwawa la Umeme la Rufiji(Julius Nyerere) ambalo litakuja kushusha bei ya Umeme,na urahisi wa mawasiliano baada ya kuikamilisha reli ya Umeme ya SGR.

Wananchi wengi waliohojiwa kuhusu upinzani walikuwa na hofu na vyama vya upinzani kuhusu uwezo wao wa kioganaizeni kuongoza nchi na exposure kuhusu mambo ya kiserkali na utayari wa kushika madaraka makubwa ya nchi na hasa kuyapinga wao wenyewe mambo waliyopigania kwa miaka 20 ambayo Rais John Magufuli aliyafanya yote kwa asilimia 98% Haya ni maoni ya wananchi siyo conclusive.niliyawakilisha na watu waliyajadili kwa hoja.

-Mafanikio ya Rais Magufuli kwa miaka mitano ya Awamu ya tano.

1.Miaka mitano ya Magufuli, Serikali iliongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za afya 1,769, zikiwemo zahanati 1,198, vituo vya afya 487, hospitali za wilaya 71, hospitali za mikoa 10, ikiwemo Hospitali ya Mkoa wa Mara, (Mwalimu Nyerere Memorial Hospital) ambayo ujenzi wake ulikwama tangu miaka ya 1970.

2.Miaka mitano ya Magufuli, Serikali ilijenga hospitali za rufaa za kanda 3. Hii ilifanya vituo vya kutolea huduma za afya kuongezeka kutoka 7,014 mwaka 2015 hadi kufikia 8,783 hivi sasa.

3.Miaka mitano ya Magufuli, Serikali iliajiri watumishi wapya wa afya wapatao 14,479, wakiwemo madaktari wapya 1,000 walioajiriwa hivi karibuni. Hii imeongeza idadi ya watumishi wa afya nchini kutoka 86,152 mwaka 2015 hadi 100,631 mwaka 2020.

4.Miaka mitano ya Magufuli, Serikali iliimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, ambapo iliongeza bajeti yake kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 270 hivi sasa na pia imenunua na kusambaza magari ya kubeba wagonjwa (Ambulances) 117.

5.Miaka mitano ya Magufuli, Serikali ilifanikiwa kusomesha madaktari bingwa 301 ambao wamewezesha kuimarisha matibabu ya kibingwa nchini, hususan kwa magonjwa ya moyo, masikio, figo, mifupa, ubongo, kansa, na kadhalika.

6.Kutokana na hatua hizo, Miaka mitano ya Magufuli, Tanzania iliongeza idadi ya akina mama waliojifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kutoka asilimia 64 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 83 hivi sasa.

7.Miaka mitano ya Magufuli, vifo vya watoto wachanga (wenye chini ya siku 28) vilipungua kutoka wastani wa vifo 25 hadi vifo 7 kwa kila vizazi hai 1,000; na idadi ya rufaa za kwenda nje ya nchi zimepungua kwa asilimia 95.

8.Kutokana na kuimarishwa kwa matibabu ya kibingwa, Miaka mitano ya Magufuli, Tanzania iliweza kupokea baadhi ya wagonjwa kutoka mataifa jirani ambao wameanza kuja kutibiwa nchini, hususan magonjwa ya moyo.

-Mafanikio katika kilimo kwa miaka mitano.

Aliongeza pato la Taifa linalotokana na Kilimo kwa 17% toka trilioni 25.2(2015) mpaka trilioni 29.5(2019).
#JPM Alifanya sekta ya Kilimo sasa ichangie 28.2% ya pato la Taifa na kuajiri 58% ya watanzania.

#JPM Alifanya nchi ijitosheleze kwa Chakula kwa 121%.
#JPM Aliongeza uzalishaji wa mazao makuu ya biashara Pamba, Korosho, Kahawa, Chai, Pareto,Tumbaku, Mkonge toka Tani 796,502(2015) mpaka 1,144,631(2019).

#JPM Aliongeza upatikanaji wa Pembejeo toka Tani 36,614,28(2015) mpaka 76,725,52 mwaka 2015 ongezeko la 110%
#JPM Aliongeza uzalishaji wa ndani wa mbegu bora toka tani 2,060,497(2015) mpaka tani 6,917,317(2020) ongezeko la 53%.

#JPM Aliongeza thamani ya mauzo ya mazao ya bustani(Horticulture) toka dola milioni 412(2015) mpaka dola milioni 779(2019) na kuchangia 38% ya pesa zetu za kigeni.
(Tumeanza kupeleka bidhaa za mboga na maua katika soko la ulaya moja kwa moja).

#JPM Aliimarisha upatikanaji wa Mbolea kwa pamoja(Bulk Procurement System) unaosaidia kupata mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu.
#JPM Aliongeza Idadi ya Viwanda vya mbolea nchini toka 4(2015) mpaka 13(2019).
#JPM Alianzisha jumla ya Viwanda 189 vya kuchakata mazao ya Kilimo.

#JPM Alifuta ushuru wa tozo za ada 105 kupunguza nyingine 4 Kati ya 146.
#JPM Alitekeleza kikamilifu mkakati wa Taifa wa vijana kushiriki katika kilimo(NSYIA) toka uliozinenduliwa 2016 ili kuwavutia vijana kushiriki katika kilimo, mikoa 12 na halmashauri 81 zinatekeleza mpango huu.

#JPM Aliongeza eneo la kilimo Cha umwagiliaji toka hekta 461,326(2015) hadi 694,715(2020)
#JPM Alirejesha mali za ushirika ndani ya miaka mitano zilizoporwa na kuuzwa kinyume na utaratibu.
Kutoka NCU(Mwanza),SHIRECU 1984(Shinyanga),KNCU(Kilimanjaro).

#JPM Kupitia wakala wa taifa wa kuhifadhia chakula alijenga maghala ya kisasa na vihenge na Kuongeza uwezo wa nchi wa kuhifadhia chakula toka tani 251,000 hadi Tani 501000.

-Tumuenzi Rais John Magufuli kwa mema yake.

Ninatambua kuwa unapokuwa Rais kuna sifa za ziada zinazotarajiwa kwako lakini pamoja nazo bado hazikuondolei ule uasili wa ubinadamu wako.

Rais John Magufuli alikuwa nao udhaifu wake kama mwanadamu lakini tupime zaidi uimara wake hasa kwenye taasisi hiyo ya urais na pale tunapoona madhaifu, basi tumkosoe kistaarabu.

Rais Magufuli alijitahidi mno na nadhani aliwashinda marais wote waliomtangulia kwa kigezo cha mambo aliyoyafanya kimaendeleo katika kipindi chake cha miaka mitano.

Kwanza alikuza sana makusanyo ya Kodi. Udhaifu katika makusanyo ya kodi kilikuwa kilio cha wengi hasa wapinzani,aliongeza kasi kwenye ujenzi wa barabara na madaraja.Serikali ya awamu ya tano ilinunua meli na vivuko vipya.

Kwenye Kilimo mikopo ilitolewa kwa wakulima,alipambana na watu wa kati wanaowadhulumu wakulima,njaa sasa imekuwa historia nchini kwetu,nidhamu imeimarika sana serikalini hivyo kuboresha huduma. Rushwa imedhibitiwa kwa kiwango kizuri.

Tuliongeza ndege na kufufua shirika la ndege. Mgawo wa umeme ulibaki kuwa historia,Umeme ulisambazwa maeneo mbalimbali ya nchi mpaka vijijini. Maji yameendelea kusambazwa.

Elimu bila malipo ambayo iliongeza udahili. Shule zote kongwe zilikarabatiwa kwa kiwango kizuri na kurejesha kiwango chake elimu cha awali. Shule za umma sasa zinaanza kurudi kwenye kumi bora. Zahanati na hospitali nyingi zilijengwa, bajeti ya dawa iliongezwa sana. Sera yetu ya mambo ya nje imehuishwa na kuwa inaingalia Tanzania kwanza.

Mambo ni mengi na takwimu zipo. Ukiangalia vizuri utaona Rais Magufuli aligusa kila nyanja na hii ndio maana tuliingia kwenye uchumi wa kati. Ukiwa na jicho la kuangalia baya ni lipi kwenye kila jema basi huwezi kuona kazi kubwa iliyofanyika.

-Rai yangu ni kuwa Rais Magufuli ni mchapakazi na mtu mkweli.Magufuli amekuwa Rais wa mfano.

Wananchi wengi walikiri kuwa Rais John Magufuli ndiye rais waliyemsubiri kwa miaka mingi sana,Awamu ya tano kuna jamaa yangu alikuwa anafanya kazi pale halmashauri ya manispaa ya kinondoni sikumuona tena.

Yaani yeye alikuwa anatembelea maeneo mawili tu,kwenye ATM na BAR. Alikuwa anajifanya eti yuko serikalini ndo maana hafanyi kazi,Awamu ya tano alikuwa mpole sana akipigiwa simu anasema yuko busy,

Vibe la JPM nadhani liliwapitia awa mission town wote,vibe lilimtembelea na kumfinya kidogo,kwa miaka mitano atakuwa alijifunza kuishi kwa jasho lako kuliko kwenda bandarini asubuhi na nauli na kurudi jioni na Milioni mbili.

Tulichoka dharau kutoka kwa vijinchi vidogovidigo mh. Raisi John Pombe Magufuli aliturudisha kwenye chati ya Afrika na kuturudishia heshima,we are a big nation a Great Tanzania.

Wale waliokuwa wameweka vibanzi kwenye macho Huku wakitetea debate yenye ubishi na utata kwamba urban area is better than rural Area, sasa DK. Magufuli kavibadilisha vijiji kuwa na kila kitu. Maji, umeme, Barabara za lami, mahospitali, shule kila Kata.

Wale wabishi wa zamani wameanza kukubali wenyewe kurudi kijijini kwa hiari baada ya maisha kuwa magumu mjini. Mission town wote wameondoka, sasa hivi ukikutana nao utawasikia wakikubaliana na hoja kuwa kwa sasa rural area is better than urban area.

Ukimwambia mzungu, Rais Magufuli anasomesha watoto wa kitanzania bure hawalipi ada hawawezi kukuamini wanasema hilo hadi ulaya limeshindikana, ukiwaambia wazungu Rais John Magufuli alipeleka umeme kila kijiji Tanzania wanaduwaa wanasema kwao vijijini wanatumia solar.

Dr John Pombe Magufuli ndio Kiongozi pekee tunayeweza kujivunia kwa kulisuka upya Taifa ambalo siku za nyuma lilipoteza mwelekeo Kabisa

Watanzania wanaitaji maendeleo na Kiongozi mahiri ambaye amebeba maono lukuki kuhakisha Nchi inasonga mbele kwenye Medani zote,

Jukwaa la Uchumi duniani ( World Economic Forum- WEF- 2019) imeitaja Serikali ya Tanzania kuwa ya 28 duniani kwa usimamizi madhubuti wa Fedha za Umma na kuziacha nyuma zaidi ya Serikali 150 zikiwemo Botswana 37, Msumbiji 69, Kenya70, Uganda100, Malawi106.

Magufuli stands out in his humility and self-deprecation. He shuns wealth, and fame. In a country where thieves are celebrated, and murderers elevated — Dr Magufuli is the one public servant who forsook worldly possessions. Mark 8:38 asks: “For what shall it profit a man, if he shall gain the whole world and lose his own soul?” Methinks the author in the good book must have had Dr Magufuli in mind.

The simplicity of this Societal and moral giant is the one thing that remains an enigma to me and many. He always roots for the little guy. He abhors hierarchy and disdains flamboyance,he’s ruthlessly self-critical. He always puts himself last. He’s a rare breed.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effect of micro-financing on Poverty Reduction.
 
Nasema watanzania wataishi kama mashetani, nasema uongo ndugu zangu!!

Nitawapiga mpaka na mashangazi zenu si kweli ndugu zangu!

Kwani mm ndo nilioleta tetemeko,, hakuna misaada hapa,,

Usiponipigia kura sikuletei maendeleo,, na kodi utatoa,,
 
Magu was genius.

Ni aina ya viongozi nadra kupatikana Afrika. Alijua nini hasa kinakwamisha maendeleo yetu.
Ukiacha mengine, lile la kuhakikisha rasilimali zinamnufaisha mwananchi ni jambo la maono na ushujaa sana.

Afrika ni maskini sababu tunanyonywa sana na wazungu. Na wanahakikisha tunakuwa na viongozi mabwana yes na kucheka cheka. Na watahakikisha viongozi dizaini ya Magu wanaondoka ili wasiwe mfano kwa nchi nyingine. Kama walivyomwondoa Gadafi.
 
Tujipe miaka/miezi michache tuanze tena kulia lia tukiomba rais kama JPM. Tatizo watu wana ubinafsi na tamaa sana bila kujua lazima kila reformation ije na maumivu makubwa na inabidi kuvumilia kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Huwezi kupata mtu kamilifu lakini unaweza pata someone who will get the job done. Afrika imekua in vicious circle kwa miaka mingi na marais sampuli za JPM ndo walihitajika kuturudisha kwenye ramani ya dunia, wengine ni vibaraka tu walio wavivu na wenye udhaifu wa fikra
 
Wewe Leslie Mbena bado upo?! Umesahau pia kuzungumzia watu wasiojulikana wakati wa Magufuli! Zungumzia utajiri na uporaji wa Paulo Makonda wakati wa Magufuli!

Vipi kuhusu vifo vya Ben Saa nane, Azory Gwanda, Leopold Lwajabe n.k.

Magufulia acha kumpampu tatizo lake lilikuwa kwenye lugha (kimalkia)ndo maana hakusafiri nje!! Mengine ni kujipendekeza tu!
 
Kwa uzi wako kutokana na tafsiri ya wanaotoa maamuzi leo na juzi wamepiga mikwara mitandao huoni kama unafitinisha uongozi uliopo kwa wananchi kwa kulinganisha utendaji bora wa Hayati JPM. Hizi ndio mama aliziita chokochoko,gilba na ufitini.

Unataka kuainisha kwamba Jemedari akiondoka kwenye nafasi basi watendaji wanabadili utendaji, wazee wa mjini wamerudi kwenye kila sekta sio, nidhamu kazini kwa watumishi imeondoka baada ya kayafa go meet his maker.

Yaani Tanesco utendaji umepungua na ukataji umeme hovyo umeongezeka sababu chuma cha pua kimeondoka sio. Watu hawaunganishi umeme kisa waziri alileta punguzo. Chuma angekuwepo hizi stori zingekuwepo sio.

Ina maana hawa Tarura wamebuni mfumo ambao kila aliyepark anaona bora pesa ampe dada lakini risiti isiwekwe sababu ya kulipia kwa simu na tozo juu sio. Yaani wadada wa parking wanapiga milo 3 na bia juu jioni hela zinavyowazidia siku hizi.
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom