Miezi saba mawaziri waponda raha hotelini,angalia uongozi wa kikwete ulivyo

nyamagaro

JF-Expert Member
Feb 25, 2010
394
225
6th June 2011Hakuna nyumba za kuwapaNahodha%2816%29.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha.


Ule ukwapuaji wa nyumba za serikali zilizokuwa rasmi kwa makazi ya watumishi wa umma bado unaendelea kuigharimu serikali kwa maofisa wake kukaa hotelini kwa kipindi kirefu kutokana na kukosa nyumba za kuishi kulingana na stahili zao.
Miongoni mwa maofisa wake ambao wanaigharimu kwa sasa ni pamoja na mawaziri kadhaa, wakiwamo wawili ambao NIPASHE imethibitisha pasi na shaka kwamba bado wanakaa hotelini tangu wateuliwe Novemba mwaka jana.
Miongoni mwa mawaziri hao ambaye amekumbwa na tatizo la kukosa nyumba ya kuishi hivyo kupanga hotelini tangu alipoteuliwa Novemba mwaka jana ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha.
Uchunguzi wa NIAPSHE umebaini kwamba tangu kuteuliwa kwake, Nahodha amekuwa akiishi katika Hoteli ya New Afrika iliyoko jijini Dar es Salaam kutokana na kutopatiwa nyumba ya kuishi na serikali.
Mwandishi wa gazeti hili alithibitishiwa na vyanzo kutoka ndani ya hoteli hiyo kuwa Waziri Nahodha anaishi katika hoteli hiyo kwa muda mrefu sasa.
Gharama za chumba kwa siku katika hoteli hiyo ni kati ya dola za Marekani 140 na dola 160, kwa vyumba vyenye hadhi ya kawaida (standard) wakati vyumba vyenye hadhi ya juu (executive suite), ni dola za Marekani 280 kwa usiku mmoja.
Msemaji wa Wizara hiyo, Isaac Nantanga, alipoulizwa na NIPASHE ni kwa nini Waziri Nahodha bado yuko hotelini mpaka sasa na lini atapatiwa nyumba ya kuishi alisema kuwa: " Sisi katika wizara tunaletewa waziri na kuambiwa kwamba waziri wenu huyo basi, lakini mambo ya nyumba ya kuishi au kwa nini anaendelea kuishi hotelini hilo si suala la Wizara ya Mambo ya Ndani.”
Nantanga, alisema wizara inayoweza kueleza kwa nini Waziri Nahodha bado yuko hotelini au kwa nini hajapata nyumba ya kuishi mpaka sasa ni Ujenzi inayomiliki nyumba zote za serikali kwani inawajibika kuwapangia nyumba za kuishi mawaziri.


Aidha alisema kwamba hata Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma pia inaweza kuwa kwenye nafasi ya kulizungumzia suala hilo.
Hata hivyo, Msemaji wa Wizara ya Ujenzi, Martin Ntemo, alipoulizwa alisema kwamba Mawaziri wote waliokuwa wakiishi hotelini wameshapatiwa nyumba.
Mbali na Nohadha ambaye pia ni Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) akiwa ametumikia nafasi hiyo kwa miaka 10 chini ya Rais Mstaafu Amani Abeid Karume, ni Waziri mmoja ambaye amekuwa akihamishwa kutoka hoteli moja hadi nyingine.
Baadhi ya mawaziri na naibu mawaziri walikuwa wakiishi katika hoteli za Court Yard na Ubungo Plaza.
Mbali na mawaziri, pia kuna majaji wengi wamekuwa wakikaa hotelini kwa muda mrefu baada ya kuteuliwa kutokana na kukosa nyumba za serikali ambazo ni stahili yao.
Serikali ilikuwa na nyumba zake zilizokuwa maalumu kwa ajili ya makazi ya mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu, wakuu wa vyombo vya usalama, mashirika ya umma, idara ya mahakama na taasisi nyingine mbalimbali za serikali ambazo zilikuwa zikitumiwa na maofisa wote kila wanapoteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali.
Hata hivyo, serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ilipitisha sera za kuwauzia watumishi wake nyumba za serikali kwa bei ya kutupa kwa kisingizio cha kuwasaidia watumishi hao kwa madai kwamba hawakuwa na uwezo wa kumiliki makazi yao binafsi.
Kadhalika, serikali ilijenga hoja kwamba ilikuwa inauza nyumba hizo ili kupata mtaji wa kujenga nyumba nyingine mpya na nyingi zaidi ambazo pia zingeuzwa kwa watumishi wa umma.
Ingawa serikali ilijenga baadhi ya nyumba hasa katika Jiji la Dar es Salaam ambazo sasa zinakaliwa na mawaziri, nyumba hizo zimekuwa zikiangaliwa kwa kuteuliwa na baadhi ya watumishi wa umma zikifananishwa na makambi, huku baadhi wakigoma kuhamia huko.
Hata hivyo, hoja ya serikali ya kuuza nyumba kwa bei ya kutupa ilikosa nguvu kwani muda mfupi baadaye zilibomolewa na wamiliki wapya (watumishi wa umma) kisha zikaporomoshwa majumba mapya ya kisasa na ya bei kubwa.
Mifano halisi inaonekana jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Oysterbay, Mikocheni na Masaki.CHANZO: NIPASHE
 

Aza

JF-Expert Member
Feb 23, 2010
1,701
1,250
mumuwajibishe mkapa wenu,sasa kama hawana nyumba je?
lol what a joke? $ 200+
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom