AbasMzeEgyptian
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 407
- 312
Magazeti haya haya yalisema NSSF imefilisika na kwamba Mkurugenzi Mkuu mpya kaachiwa fupa
Ina maana kuondoka kwa Dr Dau NSSF miezi 9 ndio mafanikio makubwa Kiasi hiki? Kutoka kuwa Fupa Hadi kuwa Imara kifedha na balance ya TRILLION 7 Kwa mpaka 2085?
Kwa miradi gani mpya iliyoanzishwa na yenye tija kiasi hicho?
Maana huyu Mkurugenzi mpya amesimamisha miradi yote na akalalamika miezi 3 iliyopita alisema hakuna mradi mbaya, wa hovyo na usio na manufaa kwa taifa na wenye kutia hasara kama Daraja la Kigamboni ambalo ni mmoja ya legacy kubwa ya Dr Dau
lakini wiki iliyopita kabadilika na kanukuliwa akisifia kuwa Daraja Kigamboni lina print pesa kuliko BOT na ni mradi bora zaidi kuliko miradi yote iliyofanywa na pension funds za nchi hii
Mwenyezi Mungu Ni Mjuzi