Upo sahihi kabisa lakini hata hilo la viwanja... ni vile tu watu hatutaki kuelewa evaluation ya land for equity! Hapa nishasema sana, unapoingia ubia na mwenye ardhi halafu percentage share yake ikafika angalau 10% wakati jengo linalojengwa ni la gharama; hapo ukifanya land evaluation LAZIMA itakuwa above market value kwa hata mara 5 na zaidi!!!Dau kajitahidi sana huo ndio ukweli ....kuna mambo kama ununuzi wa ardhi ya miradi ya arusha city na dege ......yanahitaji marekebisho ili kurekebisha bei za ardhi na mengine ,
kuna wakati huku tulikua tunawashindanisha DAU na KIMEI ..ilikuwa katika kuchagiza tu.sidhani kama kutatokea pair nyingine kama hiyo kwa sasa ....wote hao wameyatoa mashirika mbali na Magu angetakiwa awaweke karibu wamshauri.
NSSF aliyoipokea DAU toka kwa Mustapha Mkullo ....ilikuwa na assets chache sana ....sawa na CRDB aliyoipokea Kimei late 90s ilikuwa imebakisha branch hazizidi NNE nchi nzima na walikuwa mbioni kufunga bank kwa kufilisika ...leo hii wako kila wilaya na ndio bank kubwa ....
Mradi kama wa Dege city kwa stage uliokwishafikia nitamshangaa sana KIHUHIRA na huyo bosi wake kama watauzira.
Kwahiyo kimsingi, issue wala sio "bei" ya hiyo ardhi bali percentage ownership ya jengo na total value ya jengo husika!
Mbaya zaidi, wanaomiliki hizi ardhi ni real estate developers ambao piga ua hawezi kukubali kukuuzia kwavile anafahamu mambo yanaendaje kwenye real estate industry na anafahamu akikuuzia ina maana atafanya hivyo kwa kuangalia market value!! By the way, kwanini akuuzie ikiwa na yeye ni real estate developer!!!
Kwavile wanafahamu, mara zote atakutaka muingie ubia... so, is up to ukubali kuingia ubia na mimi or tafuta ardhi somewwhere else!! Na hili suala hata watu wa kawaida hivi sasa wanajua kama wanamiliki prime areas! Kwa mfano, zamani ilikuwa rahisi sana kuhamisha watu pale Kariakoo... lakini siku hizi hawakubali na badala yake wanakuambia jenga na yeye ummilikishe sehemu ya jengo husika... very brilliant!
Na kwa kutokana na hilo, Dau pale hata akipelekwa mahakamani kwa tuhuma za "kununua" ardhi ekari moja kwa 800 Million hawezi kukutwa na hatia kwa sababu hazikukunuliwa kwa hiyo bei bali zimethaminishwa to that value... thamani iliyochangiwa sana na %age ownership na thamani ya mradi!!
Wakitaka kumtia hatiani, labda waangalie ikiwa hapakuwa na ujanja ujanja... kwamba, ilikuwa very possible kwa mbia kupata 5% ownership lakini akapewa 20%... hapo ndipo unaweza kujenga kesi ngumu!