Miembe imetoa maua mengi lakini yanapukutika yote, nini shida?

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,174
73,616
Miti ya miembe imetoa maua mengi sana, la jabau ni kuwa maua yote yanapukutika na vijiti vilivyoyabeba maua vinadondoka. Tatizo ni nini na nini kifanyike in case miti inatoa maua mengine yasipukutike?
 
tafuta wataalamu wa kilimo au wauza madawa watakushauri aina gani ya dawa ya kupiga. Hiyo ni dalili ya kuwepo wadudu/fungus wanaokula vikonyi vinavyoshikilia maua.
 
Miti ya miembe imetoa maua mengi sana, la jabau ni kuwa maua yote yanapukutika na vijiti vilivyoyabeba maua vinadondoka. Tatizo ni nini na nini kifanyike in case miti inatoa maua mengine yasipukutike?
Mkuu nadhni shida ikawa ni umwagiliaji au upungufu wa virutubisho ( K au Ca) maana kipindi mmea unatoa mauwa huwa ukimwagiliwa Maji unapata stress ambazo zinapelekea flowers abortion pia upungufu wa virutubisho unaweza pelekea ilo jambo
 
Asante Sana. Ila sijamwagilia. Madini kweli inawezekana màna siweki mbolea Kanisa. Siyo kwangu tu Ni wote wenye miembe Tabia Ni moja
 
Plant stress....inasababishwa na upungufu wa madini muhimu ktk kipindi hicho...kama mmea haupati maji anza kuupatia.
 
Nikama sperms za mwanaume, zinatoka mamillion lakin moja tu ndio inafanya kaz, ata maembe pia maua ni mengi ila maembe ya wastani tu
 
A common sign your plant is stressed is if it's dropping leaves and flowers.
Stressors can include lack of water, over watering, Temperature change, less light – you name it. If the problem isn't too little or too much water, or something else easy to identify, have patience
 
Ukame, uchavushaji duni, upungufu wa boron au virutubisho vingine, magonjwa ya ukungu au fungi. Embe za kisasa zinahitaji uangalizi wa karibu kwa mwaka mzima sababu zinapendwa sana na wadudu na magonjwa ya kila aina. Kuna wadudu huwa wanaingia kipindi cha maua madhara yanakuja kuonekana wakati tunda limekomaa kwahiyo kama hukupiga dawa hatua fulani huvuni tunda hata moja. Tafuta mtaalamu akushauri huwenda ukawahi msimu
 
Mkuu sijajua kwa miembe ya kisasa ila mm na hii miembe ya kienyeji km ikianza tu kutoa maua hua naparua goma kwa kutumia panga sehem kidogo tu hii inasaidia sana mmea kutunza maua jaribu mkuu inaweza saidia.Maana mm miti yangu ilikua inatoa maua mengi sana ila yakianza viembe yanapukutika kwa wingi sana ndo nikapewa elim hii kwa kweli imenisaidia sana.
 
Chief unaweza elezea kwanini kuparua gome tu kunatosha?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom