Midomo sasa kufichua siri za watu

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Midomo sasa kufichua siri za watu

160325094246_lip_640x360_reuters_nocredit.jpg


Wataalamu nchini Uingereza wanasema wamevumbua teknolojia ya kusoma midomo ya watu ambayo inaweza kubaini wanasema nini bila kusikia wanachosema.

Teknolojia hiyo inaweza kusaidia sana kufahamu watu wanaonaswa kwenye kamera za siri za CCTV wanasema nini.

Wataalamu hao katika chuo kikuu cha East Anglia wanasema teknolojia hiyo inaweza kutumiwa kukabiliana na uhalifu na ugaidi.

160325104920_lip_reading_640x360_universityofeastanglia_nocredit.jpg


Teknolojia hiyo inaweza kutumiwa kukabiliana na uhalifu na ugaidi. Lakini pia inaweza kutumiwa na wanahabari wanaofuatilia habari za wasanii na watu mashuhuri.

Watu ambao wamekuwa wakitumiwa kujaribu kusoma midomo ya watu wamekuwa wakitatizika sana kutofautisha sauti kama vile P na B.

Lakini wanasayansi hao wanasema teknolojia hiyo mpya inaweza kutofautisha sauti hizo.

Wataalamu hao wanasema pia kwamba teknolojia hiyo mpya itasaidia sana katika mifumo ya kukusanya habari kwa kutumia kompyuta.

Chanzo: BBC Swahili
 
Wanahangaika sana hawa watu, lakini bado kila kukicha wanalipuliwa tu.

Wakimaliza hili, watakuja na macho, na maneno yao yatakuwa hayo hayo, kukabiliana na ugaidi.

Ahsante!
 
Nakumbuka jamaa wa lip reading walikuwa wamekaa mbali sana na Prince Charles na late Diana enzi hizo wanafunga ndoa na walitafsiri maneno ya Charles "I LOVE YOU" na mengine.

Walete jipya
 
Back
Top Bottom