Midlife Crisis: Life Begins at 40

Miaka ya sabini ilitoka series moja nchini Uingereza iitwayo The Fall and Rise of Reginald Perrin.
View attachment 1855833

Reginald (au Reggy) alikuwa na umri wa miaka 46. Alikuwa na mke na watoto wawili ambao walishaondoka nyumbani. Reggy alikuwa meneja kwenye kampuni anayofanyia kazi.

Kadri siku zilivyoenda Reggy alikosa raha kabisa na alianza tabia za ajabu ajabu. Alianza kuchelewa kufika kazini na kila siku sababu mpya. Alianza kujibu wateja vibaya. Bosi wake naye alikuwa anamtia wazimu!

Alianza kuchepuka na sekretari wake. Alianza tabia hatarishi, kwa mfano siku moja walienda kwenye mbuga za wanyama akatoka nje ya gari kwenye eneo lenye simba.
View attachment 1855854
Nyumbani nako mahusiano na baadhi ya ndugu zake hayakuwa mazuri na pamoja na kuwa alikuwa alikuwa na uhusiano mzuri na mkewe, alikuwa na matatizo ya nguvu.

Kuna siku aliamua kuchukua boksi lenye kumbukumbu zake za ujana na kulichoma moto.

Siku moja aliamua kuwa hawezi kuendelea kuishi namna hii.

Alichofanya ni kwenda baharini, akavua nguo zote na kuingia baharini, kisha akaibuka akavaa nguo nyingine na wigi na meno bandia, huyo akaenda kuishi kwenye mji mwingine kwa jina lingine ambako alipata kazi ya kusafisha mitaro na kutunza nguruwe.
View attachment 1855852

Stori ni ndefu....

Wanasaikolojia wanasema kuwa huwa inafika kipindi (miaka 35 - 45) ambapo binadamu hupitia hali fulani waliyoiita Midlife Crisis, kwa Kiswahili huitwaje hii, Mgogoro wa Maisha Kuelekea Uzeeni?
View attachment 1855834

Inafika wakati kwenye "graph" ya maisha, pale kwenye kilele pale, baada ya kufanya mambo mengi na kutimiza mengi, ambapo kitu pekee anachoona mtu ni kifo ndo kilichobaki.

Inafika wakati mtu huona mabadiliko yanayoashiria uzee ndo huo unapiga hodi, naye katika kukabiliana na hali hiyo huanza kufanya mambo ya ajabu ili kujihakikishia kuwa yeye bado ni kijana.
View attachment 1855835

Mabadiliko anayoweza kuona ni kama Uzito wa misuli kuanza kupungua, nywele huanza kuwa nyeupe, matatizo ya nguvu za kiume, kuanza kuchokachoka na kuumwa umwa hapa na pale n.k.

Tabia anazoweza kuanza ni kama kuanza kuhangaikia kupita kiasi afya na muonekano wake, kuanza kuchepuka chepuka ili kuthibitisha kuwa yeye bado kijana, na kukosa tu furaha maishani mwake.

Wanasaikolojia wakati huo waliona kuwa chimbuko la hii Midlife Crisis ni la kisaikolojia na la kibaiolojia.

Kisaikolojia, waliona kuwa Midlife Crisis ni "Identity Crisis", Yani ni kipindi cha mpito cha ukuzi wa binadamu ambapo anajaribu kutambua yeye ni nani na nafasi yake humu duniani ni ipi. Binadamu hupitia vipindi hivi kadhaa, ikiwemo kile anachopitia wakati wa balehe.
View attachment 1855837

Ijulikane kuwa hizi hazikuwa nadharia tu, bali zilikuwa ni principle zilizotumiwa hata na taasisi na kliniki zinazotoa ushauri tiba kwa wanandoa.

Kibaiolojia, waliona kuwa Midlife Crisis inakuja baada ya mtu kutambua kuwa sasa nguvu za ujana zimeanza kuisha.
View attachment 1855838

Kwa wakati huo, ilikuwa ikiongelewa Midlife Crisis mara nyingi walikuwa wakiongelea wanaume.

Kwa wanawake ilijulikana kuwa wao huwa wanapitia "crisis" yao kabla, wakati na baada ya ukomo wa hedhi (menopause). Kwahiyo Midlife Crisis kwa wanawake ilidhaniwa kuwa ilisababishwa tu na uwezo wake wa uzazi.
View attachment 1855839

Ni mwandishi mmoja miaka ya 80 ndio alianzisha msemo wa "biological clock" na "the clock is ticking" wakati akiongelea menopause.

Hadi kuna baadhi ya wanaume waliokuwa wanapitia crisis yao nao wakawa wasema inasababishwa na menopause za wake zao!
View attachment 1855840

Lakini je hizo pekee ndizo sababu/chimbuko la Midlife Crisis?

Jamii na mtindo wetu wa maisha siku hizi ina mchango mkubwa katika kuleta Midlife Crisis.

Ni kweli kuwa baiolojia Ina mchango katika kuogoza maisha yetu. Lakini si kweli kuwa mtindo wetu wa maisha leo hii unaongozwa na baiolojia. Jamii imetupangia mpangilio wa matukio maishani mwetu.
View attachment 1855841

Umri fulani uwe na kazi! Umri fulani uwe umeoa! Umri fulani uwe unalea watoto! Umri fulani uwe umestaafu!

Hii imefanya watu wawe na matarajio makubwa maishani, na wasipoyafikia au wakichelewa huvunjika moyo au kutoridhika na waliyoweza kufanikisha.

Kuna msemo ulitokea nchini Marekani "keeping up with the Joneses" uliotokana na katuni yenye jina hilo (1913), yani tuko kwenye wakati ambapo unaangalia maisha ya jirani na anavyomiliki ndo unajua uko wapi kimaendeleo na unafeli wapi! Jirani ana TV inch 100 wewe yako inch 30! Jirani ana vioo vya aluminium wewe huna!
View attachment 1855842

Turudi kwa jamaa Reggy. Ni wazi kuwa Crisis aliyokuwa anapitia ilikuwa mzigo mzito sana kwake. Lakini je kukimbilia kwingine kungemsaidiaje?

Msemo wa "life begins at 40" ulitoka kwa mwanamama Theodore Persons (1917) mjane aliyekuwa mwalimu wa mazoezi. Alisema, "ni kitendawili maishani kwamba hatuanzi kuishi mpaka tuanze kufa. Kifo huanza ukiwa na miaka 30, yani seli za mwili wako huanza kuzeeka. Uzee wa watu wengi huanza mapema mno. Watu wakila vizuri na kufanya mazoezi wanaweza kuishi maisha marefu mno kuliko wanayoishi leo. Maisha bora ya mwanamke huanza akiwa na miaka 40".

Mwanamama huyu alikuwa akiongea kuwapa hamasa wamama waliokata tamaa na kujiachia, ambao wengi waume zao walikuwa wameenda vitani, ili waendendelee kutunza familia zao vizuri na jamii kwa ujumla.
View attachment 1855843

Tangu wakati huo msemo huu hutumika kama njia ya kutufanya tuwe wapya (personal renewal) hasa kipindi cha middle age tunapohisi uzee unaingia, ili kutupa mtazamo chanya wa maisha na kutukumbusha kuwa bado kuna muda mrefu wa kuishi na kuna mengi tunayoweza kutimiza na kufurahia.

LAKINI, Mwandishi mmoja Edmund Bergler kwenye kitabu chake The Revolt Of A Middle Aged Man (1954), alikuwa na maoni kwamba siku hizi, hasa baada ya huu msemo "life begins at 40", watu wamekuwa wakitaka wapate furaha kwa haraka!

Yani wakati mtu kafika umri fulani, anahisi kuwa sasa anazeeka, amefeli, hajatimiza hiki na kile, huku anaambiwa life begins at 40 na mambo yanapaswa kuanza kuwa mazuri, basi haoni njia nyingine ya kupata furaha yake zaidi ya kutafuta raha za kibinafsi bila kufikiria wengine (selfish persuit of pleasure).
View attachment 1855845

Yaani, aina ya watu we Reggy, ni watu ambao huwa wanawaza hivi
"Nahitaji furaha, upendo, kukubaliwa, "tendo", na ujana. Haya yote nayakosa kwenye hii ndoa mfu na mwanamke mzee, mgonjwa mgonjwa na mlalamishi. Nitamuacha nianze maisha mapya na mwanamke mwingine. Huduma kwa watoto na mke wa kwanza nitatoa. Nasikitika hii ndoa kuvunjika. Lakini lazima nijihami kwanza! Lazima nijiokoe!"

Kwa muhtasari, Midlife Crisis sio hali ya kibaiolojia isiyoepukika. Tuelewe kuwa hali hii pia hujengwa na jamii zetu kupitia mtindo wa maisha wa jamii zetu.

- - - - - - - - - - - - -
Picha Kwa hisani ya Google.

Binafsi, naamini life begins when you Wake Up.
View attachment 1855846
Binafsi, naamini life begins when you Wake Up.

I hope hii sentensi ina maana zaidi ya moja mimi naamini life begins when you ask why yaani why zikishakuwa nyingi lazima kielewekee!
 
I'm approaching 40, kitu kinachonishangaza ni muda kwenda fast,, honestly miaka 20 iliyopita imeenda kasi Sana, miaka 20 ijayo nitakua kibibi,I hope haitakwenda fast nijiandae vizuri kuwa bibi
Kwa kawaida ukiwa busy lazima utaona muda unakimbia sana kwa sababu ya majukumu lakini ulivyokuwa mdada ulikuwa upo tayari kupoteza muda makusudi ili ufike muda fulani ufanye Jambo unalolipenda lakini twende mbele turudi nyuma ukiwa kwenye matatizo utaona muda hauendi kabisa!
 
Kwa kawaida ukiwa busy lazima utaona muda unakimbia sana kwa sababu ya majukumu lakini ulivyokuwa mdada ulikuwa upo tayari kupoteza muda makusudi ili ufike muda fulani ufanye Jambo unalolipenda lakini twende mbele turudi nyuma ukiwa kwenye matatizo utaona muda hauendi kabisa!
Hauko sahihi mkuu, ukiwa na matatizo muda unaenda fast kabla hujayatatua😊😊
 
Wewe hujawahi kumbwa na balaa zito katika maisha yako unapokuwa na matatizo unakuwa na msongo wa mawazo kama let's say umehukumiwa miaka 30 jela muda uraendaje fast ili utatue hilo tatizo?
Mnhhhh mfano wako na midlife crisis wapi na wapi? Lol
 
Hivi ni kawaida mfano kufikisha miaka 30 na bado haina chochote cha kueleweka ulichofanya ..hii hali huwa unaweza vipi kupambana nayo? Labda unakuta nyuma una deni kubwa umebeba labda la wazazi, wadogo zako labda au ndugu zako wengine wanàkuangalia wewe na hapo unakuta ni bila bila..
 
I'm approaching 40, kitu kinachonishangaza ni muda kwenda fast,, honestly miaka 20 iliyopita imeenda kasi Sana, miaka 20 ijayo nitakua kibibi,I hope haitakwenda fast nijiandae vizuri kuwa bibi
natamani nibaki hivi, nisiongezeke umri, actually 40 is perfect age, not young not old...upo kati hapo, akili imetulia.....
...bad thing is, 20yrs to come hamna kitu tena...babu WTF maisha haya!!!
 
nikifikisha miaka 40 nikiwa sina kitu siwezi kumlaumu yeyote hata nafsi yangu nishahidi...kusoma nimesoma japo kiasi..kazi zote za kipumbavu nimefanya..jela nimewahi kuishi kwa kesi ya kupewa ..Tamisemi wanaendelea kuninyoosha na umri unanitupa mkono.
Wanakunyoosha kivipi? Ajira au?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom