"Middle income country" ni Mbinu nyingine ya Wazungu!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,782
Huwa nashindwa kuelewa ni kwa nini nchi karibia zote za Kiafrika sasa imekuwa kama fasheni kila mtu anasema mwaka fulani tutakuwa ,,middle income country" au nchi ya kipato cha kati, sasa nashindwa kuelewa logic ya huu msemo, tuchukulie kwa mfano TanZania yetu tunaambiwa kwamba 2025 tutakuwa nchi ya kipato cha kati au middle income country, sasa hapo ni nini kitabadilika?

Kwa maana sasa hivi tunaambiwa sisi ni moja kati ya nchi masikini Duniani lkn tunaambiwa kwamba 2025 tutatoka hapa na kuwa pato la kati (middle income country) lkn si ni bado tutakuwa ni moja kati ya nchi masikini kuliko zote Duniani kama tulivyo sasa kwani wale walio hiyo middle income ambayo sisi tutaifikia si watakuwa wamepiga hatua na kwenda mbele zaidi?
Sasa logic iko wapi?

Au nchi zote zitasimama na kuwa na minus mpaka 0% economic growth mpaka sisi tuwakute hiyo 2025?

Kwangu mimi naona huku kupeana majina ni mbinu ya Wazungu kuendelea kututawala, na kutubakiza nyuma, unajua maneno yanaumba wametuita masikini na sisi tumekubali sasa wanatupa jina la middle income ikumbukwe kwamba haya majina yanaendana na sera ambazo hao hao Wazungu ndiyo wanatupa za Uchumi wetu kwa mfano sasa hivi ni masikini na sera wanazotupa ni za kuuza Malighafi kama Kahawa, Chai, dhahabu ghafi n.k., baadaye wakituita middle income watatuwekea sera ya kuwa na semi finished goods hivyo hivyo lengo ni kuendelea kutuweka chini yao milele na sisi tunakubali ningeshauri tuache huu ujinga wa kujiita masikini au sijui middle income na hilo lisiwe lengo letu bali lengo letu liwe kuzipita nchi zilizo mbele yetu Kiuchumi tusema tunataka kuifikia Ujapani, Ujerumani au USA na siyo sijui 2025 tutakuwa middle income tukifika huko watatupa tena kigezo kingine kwamba 2050 tutakuwa sijui lower middle income n.k. hivyo binafsi sioni mantiki ya hizi label isipokuwa kuendelea kutufanya tubakie kuwa nyuma tu na Mzungu daima mbele yetu!
 
Umesahau kile nilichokujibu kule? Naona Umenielewa umeamua kuja kuanzisha thread huku! Si unataka Tanzania ya Viwanda vya vibarua??
 
Jibu langu refu sana mkuu lakini naomba ulisome lote

Uko sawa kwa mtazamo mmoja ilhali tena Kuna penye umepotokwa pakubwa.

The rankings are surely to deride and degrade most countries in the Asian, African and South American continents. Nchi kama Brazil for instance Wana urbanization rate ya 90%, zaidi ya kina USA, France, UK, Germany etc. Ukitazama miundo msingi kama barabara, maji Safi ya bomba, stima zipo kila mahali, lakini waitwa upper middle income nation, hawawezi kuwa kwa vyama vikubwa kama OECD, UNSC nkd. Hio kwangu ni kuwadhulumisha tu.

Lakini ukitazama kimaendeleo, Tanzania ii mbali Sana ikilinganishwa na taifa kama uingereza, ufaransa au ujerumani. Ukisema wataka kuwafikia hao lazima uwe na mipango dhabiti ya kufika hapo. You need a very big vision that can be subdivided into small achievable short term objectives kama vile tuseme ikifika mwaka 2020, Tanzania yafaa iweze kukimu mahitaji yake ya plastiki bila kununua toka nje. If you manage to meet this need by then, hamtakua mmewafikia hao mababe lakini tofauti kati yenu itapungua. Hela zilizokua zatumiwa kuingiza bidhaa za plastiki zawezatumika kujenga barabara hadi mashinani na hii itawezesha mkulima kuuza mazao yake jijini na kuongeza pato. By doing that, you have increased your country's per capita income from very low down to somewhere in the middle hence a middle income nation.

Shida ni viongozi wanaweka malengo ya karibu tu (middle-income) huku wakijitajirisha badala ya kuiga taifa kama Korea kusini, Taiwan, Singapore nkd walioapa kuwafikia wajiitao the developed world na wakaweka mipango short, middle na long term. Hivi Sasa Singapore ishawapita hao wafaransa, waingereza, wajerumani na wamerika. Korea kusini nao washawapita wahispania na waitalia na tuzungumzapo Hivi, washawakodolea macho wafaransa na kuwakaribia kwa vishindo. Mataifa haya mawili mnamo 1960s yalikua sawa na Tanzania na Kenya kimaendeleo.

Lakini kabla wafike hapo walipitia eneo la middle income nation, wakawapata wakolombia, Venezuela na Mexico hapo na wakawapita na kuwaacha papo hapo juu ya kuwa na na kufuatilia mipango yao mifupi, ya kati na mirefu. Hii yamaanisha zipo taifa zilizonaswa na "the middle income trap" na kwa karne kadhaa hazijakua. Therefore with proper long term visions, well stated medium term goals and achievable short term objectives, Tanzania can come from behind, find several nations in the middle income trap and leap frog these stagnant nations as the far Eastern Asian countries did. Yawezekana.
 
Ulitaka usiwekewe viwango ili mbweteke?

Fanyeni kazi kuwafikia hao.
 
Nakubaliana na wewe kwamba ni lazima tuweke malengo kwani hatuwezi kuruka ktk hapa tulipo na kuwa kuwa nchi iliyoendelea lkn tatizo langu ni kwamba haya malengo hatuyaweki sisi bali Wazungu ndiyo wanaotuwekea hiyo ndiyo hoja yangu hasa!

Waliokuja na agenda 2025 au 2030 siyo sisi Waafrika bali ni Wazungu halafu wanatuambia sisi tutekeleze.
Kama sisi ndiyo tungekuwa tunajiwekea hayo malengo ni sawa kwa mfano Uchina walikuwa first five year plan, baada ya hapo ikaja great leap forward wao ndiyo waliopanga na kuweka hayo malengo na kulikuwa hakuna maneno kama sijui lower middle income au upper lower income ila kwetu sisi tunaletewa plans na Wazungu na kuambiwa 2025 tunatakiwa tuwe middle income country na ili tufanikishe tufanye abc sijui sasa sasa hivi wanasema (Wazungu) ,,Agenda 2030, 2063 and beyond the Africa we want" ina maana wao (Wazungu) ndiyo wanatengeneza hiyo blue print na kutupa sisi Waafrika tuifwate na siyo sisi kujiwekea malengo kulingana na uwezo wetu na jinsi tunavyoona iinafaa kama vile Uchina walivyofanya!

Hivyo ukiangalia utaona kwamba sisi ni kama watoto wa Wazungu na wao wanatuambia nini cha kufanya na njia gani tupite hivyo basi tutaendelea kwa jinsi wanavyotaka wao na kamwe hatuwezi kuwafikia kwani wao ndiyo wanaopanga tuendelee vipi lkn nchi kama Korea Kusini, Uchina, Singapore, Taiwani na hata Malaysia walikuwa na blueprints zao wenyewe na siyo ktk kwa Wazungu na ndiyo maana walitoka, angalia Afrika hakuna nchi inayopeleka kwa mfano wanafunzi kwa wingi kwenda kujifunza nchi za nje na kuwarudisha baada ya kuhitimu kuja kujenga nchi kama walivyofanya Korea, Singapore au hata Uchina, kama kweli tulikuwa serious sasa hivi ningetegemea tuwe tunasomesha Wanafunzi Dunia nzima ili wapate skills ambazo sisi hatuna na baada ya kuhitimu kuwarudisha nyumbani ili kufanya knowledge transfer lkn sijaona mpango kama huo, wanaokwenda nje ni kwa jitihada zao binafsi na huishia huko hawarudi nyumbani ...
 
Unachonena ni ukweli mtupu, ukifuatilia mipangilio yao, haswa île ya IMF na world bank, utaishia kuwauzia raw materials tu nao wakikuuzia finished goods. Hii ni kwa sababu hii mipango mara nyingi huhimiza mataifa ya fungulie soko ushindani toka nje ili viwanda vya nyumbani viweze kua world class lakini lengo ni kupanua soko ya bidhaa za viwanda zao.

Lakini ukitazama vyema, hii mipango hulenga nchi zilizolalia sikio na hakuna jitihada zifanyazo kujiwezesha kiuchumi. I'll give you an example of my country, kenya. Mpaka hapo 1998, wakati wa moi na kenyatta, tulikua twafwata kidete zile MDGs, SDGs na hazikutusaidia kamwe. Benki kubwa zilikua Barclay's na Standard, processed food zilikua za kampuni kama finlays kwa majani Chai, Unilever kwa edible oils, mabati ilitoka uingereza na simiti ilikua ya Lafarge from France. Gdp ya Kenya ilitoka 13bn in 1960s to just 20bn in 1998, takriban nusu tu kwa karibu karne nne. In short, walikua wametukalia chapati.

Baada ya kibaki kuchukua urais na wadau wakaketi chini kubuni vision 2030, benki kubwa kabisa Kenya ni KCB na equity ambazo zimekita mizizi Kanda lote, BIDCO ndio kampuni kubwa zaidi ya edible oils ikiuza as far south as Angola na as far west as Ghana na hata imenunua shares za Unilever, Chai ni ya ketepa, kakuzi, kiptagich etc, mabati rolling mills na Dumu Zas zauza mabati hadi Sudan kaskazini. Simiti twajua ilivyo sasa. Gdp iliongezeka zaidi ya mara tatu toka hio 20bn hadi 65bn hivi Sasa chini ya Karne mbili.

Ninachosema ni mipango yao mbovu mno, tukifwata twaumia lakini si wote wazifwata, wale waliozipuuza washaanza kuona mwanga kwa umbali.
 
Asante kwa maelezo mazuri!
 
Upo uwanja wa mapambano, halafu mpinxani wako anakupa jinsi gani ya kuweza kumfunga, ni kweli au danganya toto ? Tusiwaamini hawa bila ya kuchambua na kufikiria kile ambacho sisi kama tz (Afrika) tunakihitaji zaidi, au watatupelekesha sana ili tusipige hatua (wakishirikiana na baadhi ya viongozi wetu). Akili vichwani mwetu !!!!
 
Tatizo Watanzania hamna mipango endelevu, mnaishia kukurupuka na maamuzi bila kuwaza na kudadavua. Mnafanya mambo kwa kushtukiza na kubabaisha. Mara Big Results Now mara sijui nini.
Hadi muige Kenya na kukaa chini na kutafakari kwa muda, mtaendelea kuonekana kwenye hizo takwimu za LDC wakati mna kila aina ya raslimali.

Nchi ya Kenya ilikusanya wataalam wa kila nyanja, wachumi, wana sheria, wajenzi n.k. Wakakaa wote pamoja na kuandika dira ya nchi ambayo inaitwa vision 2030. Halafu Wakenya wengi tukapewa darasa kuhusu hii dira, ikawa taifa lote tunafuata mwendo mmoja ili kuifanikisha.

Kwamba kila uongozi unaoingia, lazima ujitahidi kufanikisha. Leo hii hata kwenye kampeni, wagombea urais wote wanajinadi jinsi watabuni mikakati ya kufanikisha hiyo dira. Kwa kifupi, kila mtu anajua tunakokwenda ndani ya miaka ingine kumi. Hata kwenye mahojiano ya ajira (job interview), huwa kuna maswali sana yanayohusiana na hii dira ya taifa.

Ni baada ya hapo ndio tumeona nchi inapiga hatua kwa kasi maana leo hii tunajua tunakwenda wapi kama taifa. Na hatutegemei maamuzi ya rais, kwamba hujui ataamka vipi kesho au na lipi. Atamfuta nani na kumwajiri nani, atazuia wapi na kufungulia wapi, nchi inaishi kwa taharuki. Nimeona sehemu eti mkuu wa mkoa Dar es Salaam kaibuka ghafla na kuagiza watu wote wasiokua na ajira wahesabiwe, kwamba wakuu wa mitaa wazunguke nyumba kwa nyumba na kuhesabu, sasa hajatoa hata taarifa kwanini anafanya hivyo, anawaweka watu katika hali ya taharuki na kubabaisha. Haifahamiki analenga kufanikisha nini hamna malengo yaliyowekwa wazi, hamna mwelekeo ni full mkurupuko na ubabaishaji.

Mnasema haitokuja siku muige Kenya, lakini itafika siku mtaelewa tu. Leo hii mna jazba sana na Wakenya, mkimkamata Mkenya anaiba inakua taarifa za habari nchi yote kwenye runinga na redio zote na mitandao ya jamii yote. Inadhihirisha jinsi tumewatamausha kwa kushindwa kutufikia.
 
Hizo ndo sifa za KIKE.

Kuna sehemu imeandikwa Kenya na Tanzania.

Unajibu swali usiloulizwa.
 
Upo uwanja wa mapambano, halafu mpinxani wako anakupa jinsi gani ya kuweza kumfunga, ni kweli au danganya toto ? Tusiwaamini hawa bila ya kuchambua na kufikiria kile ambacho sisi kama tz (Afrika) tunakihitaji zaidi, au watatupelekesha sana ili tusipige hatua (wakishirikiana na baadhi ya viongozi wetu). Akili vichwani mwetu !!!!
Kabisaaa, tusipoamini vichwa vyetu, tutahadaiwa tu siku nenda siku rudi. Nafurahi jinsi nchi kadhaa Bara hili zajiwekea mikakati. Tazama uhabeshi, Rwanda nkd
 
Tatizo Watanzania hamna mipango endelevu, mnaishia kukurupuka na maamuzi bila kuwaza na kudadavua. Mnafanya mambo kwa kushtukiza na kubabaisha. Mara Big Results Now mara sijui nini.
Hadi muige Kenya na kukaa chini na kutafakari kwa muda, mtaendelea kuonekana kwenye hizo takwimu za LDC wakati mna kila aina ya raslimali.

Nchi ya Kenya ilikusanya wataalam wa kila nyanja, wachumi, wana sheria, wajenzi n.k. Wakakaa wote pamoja na kuandika dira ya nchi ambayo inaitwa vision 2030. Halafu Wakenya wengi tukapewa darasa kuhusu hii dira, ikawa taifa lote tunafuata mwendo mmoja ili kuifanikisha.

Kwamba kila uongozi unaoingia, lazima ujitahidi kufanikisha. Leo hii hata kwenye kampeni, wagombea urais wote wanajinadi jinsi watabuni mikakati ya kufanikisha hiyo dira. Kwa kifupi, kila mtu anajua tunakokwenda ndani ya miaka ingine kumi. Hata kwenye mahojiano ya ajira (job interview), huwa kuna maswali sana yanayohusiana na hii dira ya taifa.

Ni baada ya hapo ndio tumeona nchi inapiga hatua kwa kasi maana leo hii tunajua tunakwenda wapi kama taifa. Na hatutegemei maamuzi ya rais, kwamba hujui ataamka vipi kesho au na lipi. Atamfuta nani na kumwajiri nani, atazuia wapi na kufungulia wapi, nchi inaishi kwa taharuki. Nimeona sehemu eti mkuu wa mkoa Dar es Salaam kaibuka ghafla na kuagiza watu wote wasiokua na ajira wahesabiwe, kwamba wakuu wa mitaa wazunguke nyumba kwa nyumba na kuhesabu, sasa hajatoa hata taarifa kwanini anafanya hivyo, anawaweka watu katika hali ya taharuki na kubabaisha. Haifahamiki analenga kufanikisha nini hamna malengo yaliyowekwa wazi, hamna mwelekeo ni full mkurupuko na ubabaishaji.

Mnasema haitokuja siku muige Kenya, lakini itafika siku mtaelewa tu. Leo hii mna jazba sana na Wakenya, mkimkamata Mkenya anaiba inakua taarifa za habari nchi yote kwenye runinga na redio zote na mitandao ya jamii yote. Inadhihirisha jinsi tumewatamausha kwa kushindwa kutufikia.

Hauelewi unachokiandika, Agenda 2030 siyo mpango wa Kenya bali ni mpango wa UN chini ya 2030 Agenda for sustainable development ambapo kama Kenya kama zilivyo nchi nyingine masikini walipewa na kuambiwa nini cha kufanya kufikia hayo malengo, hivyo wacha kupotosha Kenya haijatayarisha agenda 2030 bali Wazungu ndiyo waliotengeneza agenda 2030!
 
Mkuu, tofauti ipo kati ya agenda 2030 ya UN na vision 2030 ya Kenya

Agenda 2030 ya UN came to action in a historic UN summit in 2015 and it had 17 SDGs. These were to be implemented in the next 15 years after the summit hence 2030 was the end year. This is under the sustainable development goal of the UN.

Vision 2030 of Kenya was passed much earlier, 1st conceptualized in 2000 and commissioned in 10th June 2008 as a blue print and guide for the nation's quest to become a newly industrialized (upper) middle income economy exceeding $10,000 per capita. This was hence to provide high quality life to its citizens by 2030.
 
Hauelewi unachokiandika, Agenda 2030 siyo mpango wa Kenya bali ni mpango wa UN chini ya 2030 Agenda for sustainable development ambapo kama Kenya kama zilivyo nchi nyingine masikini walipewa na kuambiwa nini cha kufanya kufikia hayo malengo, hivyo wacha kupotosha Kenya haijatayarisha agenda 2030 bali Wazungu ndiyo waliotengeneza agenda 2030!

Makada wa CCM ni mfupa uliomshinda fisi, huwa nafuatilia jinsi mnavyobisha kwenye hoja zenu hadi nawaonea huruma. Hata kama mnalipwa, mnafaa kutumia akili na kutafiti kabla ya kujibu hoja. Agenda ya UN 2030 kitu cha hivi majuzi utalinganisha vipi na dira yetu tuliobuni enzi za rais Kibaki.

Unatia huruma, kwaheri sitapoteza muda zaidi nawe.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom