Middle East Political Unrest: Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje wanatoa tamko gani juu ya usalama wa raia wa Tanzania waishio Mashariki ya Kati?

Yapaswa iwe hivyo ila kwa Tanzania sidhani km kitu hicho kinafanyika, nakumbuka suala la Msumbiji....kuna watanzania wenzetu walikuwa wanakimbia huko wengine wakawa wadhubutu kuvuka mito na wakafia humo...wengine walipoteza mali zao...kumbuka suala la S. Africa,....nilianza kuhisi baba hana huruma na watoto wake....."serikali haikuleta tetemeko""....Huko Kagera... Rwanda ilichangia, Kenya ilichangia, Uingereza ilichangia, Watanzania walichangia, kanisani tulichangia , misikitini tulichangia nk...raia wa Kagera waliopatwa na majanga walipewa pakti za biscut... nakumbuka baba alikuja kumeshakucha kabisa majirani walikuwa wameshatufariji kadri ya uwezo wao....baba alifika anawaambia kuwa si yeye aliyeleta tetemeko......Sembuse ndugu zetu walioko Ughaibuni.....nahisi hatuna bahati kwa kipindi hiki juu ya masuala ya utu.

Sent using Jamii Forums mobile app
If this statement is true, then something must be wrong somewhere
 
Kwahiyo US alivyotoa tamko juu ya raia wake waishio nje walitoa kiwehu wehu? Je hawakuangalia impact zitakazotokea kwenye hizo nchi?
Balozi za USA ziko kwa ajili ya maslahi ya wananchi wake, balozi zetu ziko kwa ajili ya uhusiano wa kiserikali tu na ndicho kisa wengi huzilalamikia kwa kutowajali.

Serikali ya Marekani ni ya wananchi na kwa ajili ya wananchi, serikali ya Tanzania ni ya CCM kwa ajili ya wanaccm hii ndiyo tofauti kubwa.
 
mmmmh. Haya mimi simo
Nchi hujengwa na wananchi bila kujali dini, vyama na makabila yao, sisi tunalazimishwa kubaguana kivyama tukiaminishwa kuwa Tanzania ina wenyewe na wenyewe ni wanaccm na ndicho kisa cha kuambiwa CCM itakomboa majimbo yote yaliyochukuliwa na wapinzani (hawa si wananchi)!
 
"Mimi sikumtuma mtu aende huko mashariki ya kati,halafu mbona mnapenda kuniongezea frustration kila kitu mnataka nizungumze kwanza nimetoka likizo juzi tu bado sijawa tayari kuropoka ropoka,"amesikika kiongozi mmoja nzito
Msumbiji watanzania walifanyiwa kitu mbaya sana lakini kauli za mkuu ziliniacha hoi. Kwa hali hiyo unataka watu bado wawe wazalendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tamko linatakiwa kutolewa na nch husika kuwa Kuna Hali ya hatari .

kwenye mahusiano ya kimataifa ukijitamkia tu waweza leta mgogoro mkubwa Kati yako na hiyo nchi unayoiyoitamkia tamko sababu mfano utalii kwenye hiyo nchi waweza poromoka,uwekezaji ukaporomoka ,investors wakaondoka ,biashara yake ya nje ikaanguka sababu watu watakataa kuingia mikataba ya Kibiashara nao kea ku base kwenye tamko lako.

Matamko.hayatolewi kiwehu wehu tu kisa Kuna mtanzania Yuko nje ya nchi anafanya kazi za kuosha matako vizee vya kizungu au vya kiirani
Mbona Uingereza imeonya Raia wake wajihadhari. Ina maana itasababisha mgogoro mkubwa? Au hufuatilii vyombo vya habari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cc Infantry Soldier take care mimi ni mromboo sio mnyakyusa it's better if you will mind your business dharau za kijinga sizitaki
 
Back
Top Bottom