Midaharo ya Uchaguzi wa Tanzania 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Midaharo ya Uchaguzi wa Tanzania 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Paul J, Oct 28, 2010.

 1. P

  Paul J Senior Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zikiwa zimebakia siku tatu tunazidi kuona ni kwa jinsi gani watawala wetu wanazidi kukosa mwelekeo na kubaki kutapatapa tu. Watanzania wenzangu nani asiyejua kuwa hapo awali midaharo ya kisiasa iliombwa na wenzetu wanaoitwa wachochezi lakini ikakataliwa na CCM kuwa midaharo hiyo haina tija wala maslahi ya chama? Nyinyi nyote ni mashahidi. Anayepinga hili basi hayuko Tanzania hii wala dunia hii labda kafufuka leo toka kuzimu. Ni jambo la kushangaza kuona watu walewale waliokataa mdaharo leo wanajitokeza kuwa nao wanataka mdaharo. Hiki ni kipimo tosha cha kukosa dira na mwelekeo kwa watu kama hao na hii inadhihirisha wazi kabisa kuwa hata yale yote ambayo yameishasemwa na kuhahidiwa kwa watanzania ni usanii mtupu!!!!!!!!.

  Katika hali ya kawaida nilitegemea chama tawala hata kama hakikuwa na uwezo wa kuendesha midaharo kipindi hicho basi wangetumia hekima walizonazo na si kukana hadharani na hasa katika vyombo vya habari kuwa hakuna mgombea wao atakayejishughulisha na midaharo. Baada ya Dr. Slaa kuendesha mdahro na ITV tarehe 23/10/2010 na kujibu hoja zote kwa ufasaha akatoa changamoto kwa CCM waliokataa midaharo na leo hii wanasema eti mgombea wao naye atafanya mdaharo kupitia chombo hichohicho? Swali Mbona CCM ilikataa katakata wagombea wake kufanya midaharo? Hivi Kweli CCM ina nia ya kweli kuwakomboa watanzania kutoka mikononi mwa umasikini, maradhi, na ujinga ambavyo warithishwa kutoka TANU mwaka 1977 mpaka sasa bado haijapata hata kuonyesha nia ya kufanya hivyo kwa maana haijui kwa nini Tanzania ni masikini wakati imejaliwa kuwa na rasirimali za kila namna?

  Wanamapinduzi na watanzania wenzangu bila kujali itikadi zetu za vyama na imani za dini zetu na makabila yetu imefika wakati wa kutambua kuwa CCM siku zote wamelala na wanasubiri kuamshwa na vyama vya upinzani na hii imejidhihirisha mara nyingi hakuna ubishi. Kwa jinsi hii kwa kuwa vyama vya upinzani na hasa CHADEMA imeonyesha kuiamsha CCM kila mara lakini bado haionekani kuamka na sasa imekuwa ni chama cha kudandia hoja za wapinzani basi tukipumzishe kijipange upya kije na dira yake mpy a maana hata ile ya TANU ya mwaka 1954 mpaka sasa bado kimedhihirisha kushindwa kabisa. Nani asiyejua kuwa asilimia kubwa ya watanzania bado ni masikini? Nani asiyejua kuwa bado watanzania wengi wanasumbuliwa na maradhi? Nani asiyejua kuwa watanzania wengi wametolewa kafara kwenye shule za kata kama alivyosema Mheshimiwa Kikwete katika mahojiano yake na BBC?

  Watanzania wenzangu mimi ni mtanzania mhangaikaji kama wahangaikaji wengine hapa Tanzania, nani asiyejua kuwa serikali iliyopo bado inangangania kashati ulikokavaa kwa jasho lako? Hamjui hilo? Si rahisi kulijua, lakini nafafanua. Tunalipa pay as you earn, VAT LEVY, Property and Land Tax, Ewura nk. Hizo zote ni pesa ambazo unazifanyia kazi kwa jasho lako-ni shati lako. Kwa nini tunalipa hizo kodi? Simple: Huduma za jamii ziwe bora: Wangapi wananua vidumu vya maji hapa mjini Dar es Salaam about 10-15km from State house? Wangapi wanakosa huduma bora za matibabu wanazidi kujikamua kutibiwa hospitali binafsi? Wangapi wanakosa elimu bora wanakimbilia kuwapeleka watoto wao medium/Saint school? Wangapi wananunua nguzo za Tanesco na bado hawana umeme?

  YAPO MENGI KIKUBWA NI KUBADILISHA MFUMO ULIPO TUKAJA NA MFUMO MPYA.
  TULIPIGANIA UHURU TUKAUPATA KUTOKA MIKONONI MWA WAKOLONI KWA MIAKA 7 TU (1954-1961) TUNASHINDWA NINI KUPIGANA NA UMASIKINI, MARADHI NA MAGONJWA KWA MIAKA 49 (1961-2010)

  DHAMIRA (VISION) ZAMWL ZILIKUWA NI
  1. Kupigania uhuru wa Tanganyika na Afrika kwa ujumla (100% achieved)

  2. Kupigana na maradhi, umasikini na Ujinga (65% achieved)

  Nini Vision ya CCM? Anayejua anipe jibu


  CHAGUA CHADEMA HATA KAMA KIKWETE ATAPATA MADESA YA MDAHARO KABLA LAKINI UKWELI MTAUONA!
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
   
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Good point. Ila naomba ufanye marekebisho ya kiswahili kidogo. Ni Midahalo, sio Midaharo...
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nyingine ni "kuwafukarisha watanzania kadri iwezekanavyo ili iwe rahisi kuwanunua wakati wa uchaguzi".
   
 5. P

  Paul J Senior Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sijaona mwana CCM hapa akichangia na intention yangu kubwa ni kusikia kutoka chama tawala ili tuzidi kuwapima kimawazo, kifikra na kimtazamo, hata kama wanazidi kutawala kwa sababu ya ujinga, umasikini na maradhi ambavyo wamevipandikiza kwa watanzania waliowengi. Ninachoamini tofauti na imani yangu ya dini ni kwamba mtu mwenye akili timamau na asiyekuwa na maslahi binafsi na CCM hataichagua na akifanya hivyo kwa sababu nyingine hiyo basi atakuwa ni msaliti mkubwa na kama atakuwa na sababu yoyote ile ya kuichagua CCM atushirikishe kupitia jamii forums ili tusimuweke kwenye kundi ambalo sitadhubuti kulitaja hapa.
  Piga kura kuonyesha uzalendo wako kwa Tanzania na hasa kwa masikini na wajinga wa Tanzania, kama wewe tajiri kwa nafsi yako mushukuru Mungu lakini nyuma yako wako mamilioni ya watanzania wanaishi kwa kubahatisha. Pigeni kura makini tuache utani nchi na watu wake vinakosa mwelekeo because of POOR LEADERSHIP AND CORRUPT GOVERNMERT
   
Loading...