Midahalo ya wagombea urais kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,411
114,363
Mwishoni mwa juma lililopita nilileta mada hapa jukwaani kuhusu Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Bw. Thabo Mbeki, alivyomkumbuka hayati Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Kwenye bandiko hilo, nami nikatoa maneno mawili matatu kumhusu Rais huyo mstaafu Mkapa, kwa jinsi nilivyomjua mimi, kiumbali.

Moja ya mambo niliyoyakumbuka ni ule mdahalo wa wagombea urais wa mwaka 1995 ambao ndo ulikuwa uchaguzi wa kwanza katika kurudi kwenye mfumo wa vyama vingi.

Nilisema hivi kuhusu ushiriki wa Rais Mkapa kwenye huo mdahalo:
B5935604-6560-49D6-AD5F-87BD14264E47.jpeg

Hilo bandiko linapatikana hapa.

Siku chache baadaye, mwenzetu Bw. Pascal Mayalla akaleta makala ya January Makamba, ya kumkumbuka marehemu rais huyo mstaafu.

Moja ya mambo ambayo Bw. Makamba aliyazungumzia, ulikuwa ni ule mdahalo wa wagombea urais wa mwaka 1995, mdahalo ambao nadhani ndiyo uliomtambulisha vizuri Rais Mkapa kwa umma wa Watanzania.

Katika kumbukumbu yangu, mimi nilisema Rais Mkapa alifanya vizuri sana kwenye huo mdahalo. Licha ya kwamba hakuna kipimo sahihi cha kupima na kuona yupi alishinda, kwa maoni yangu, Rais Mkapa alishinda mdahalo ule.

Na kwa maoni ya January Makamba, nadhani ni sahihi pia nikisema hata yeye January aliona kuwa Mkapa alishinda.

Yeye Bw. Makamba alisema hivi:

DFCDFC21-FC2A-415F-AFE7-896E3248D133.jpeg

Kusoma zaidi alichokiandika Bw. Makamba, bofya hapa.

Tokea mwaka huo wa ‘95, nadhani hatujawahi tena kuwa na mdahalo wa kitaifa wa wagombea urais.

Ningependa sana mwaka huu wa uchaguzi tuwe na mdahalo wa wagombea hiyo nafasi. Ila, sitashikilia pumzi yangu kusubiri hilo kutokea.

Lakini pia, nimeona si vibaya kuleta ombi/ wazo hili hapa.

Ombi ama wazo lenyewe ni kuipata video ya mdahalo wa ‘95.

Nimezunguka sana mtandaoni na huko YouTube, lakini nimeambulia patupu.

Pascal Mayalla wewe ni mwandishi wa habari wa muda mrefu. Naamini bado una uhusiano na watu waliomo kwenye vyumba vya habari vya vyombo vya habari hapa.

Sikumbuki vizuri ni stesheni zipi za runinga ambazo zilirusha matangazo ya ule mdahalo. CTN? ITV? DTV? Radio One labda?

Sasa Bw. Mayalla, unaweza kutumia uzoefu na nyenzo zako ulizonazo kututafutia video [au hata audio] ya huo mdahalo?

Mimi si muangaliaji sana wala si mfuatiliaji sana wa stesheni za runinga za hapa Tanzania. Ila kama kuna stesheni ambazo labda zina chaneli huko kwenye YouTube, zinaweza kuipandisha video ya huo mdahalo kwa faida ya umma.

Kama inawezekana, tusaidie Bw. Mayalla...

Shukran jazilan na ahlan wa sahlan.
 
Katika midahalo kuna vitu vingi sana vyenye umuhimu vya kuvijua na kujifunza toka kwa viongozi/wagombea wetu. Napendekeza pia ukufanyika

Mawazo yangu ni kwamba nahisi kama kuna wagombea/mgombea wanaweza/anaweza bado kujivika cheo cha urais kabla ya uchaguzi na akatoa zile lugha na sauti za mzazi kumkemea mtoto wake mkosefu

Baada ya kuzidiwa point
*"Wewe usinijibu hivyo mimi"*
Ndani ya mdahalo
 
Katika midahalo kuna vitu vingi sana vyenye umuhimu vya kuijua na kujifunza toka kwa viongozi/wagombea wetu. Napendekeza pia ukufanyika

Mawazo yangu ni kwamba nahisi km kuna wagombea/mgombea wanaweza/anaweza bado kujivika cheo cha urais kabla ya uchaguzi na akatoa zile lugha na sauti za mzazi kumkemea mtoto wake mkosefu

Baada ya kuzidiwa point
*"Wewe usinijibu hivyo mimi"*
Ndani ya mdahalo
Ikitokea hivyo ndio itakuwa vizuri sasa!
 
CCM huwa hatutaki midahalo ya wagombea Uraisi sababu wapiga kura wengi asilimia 80 wanaishi vijijini na wengi hawana TV Wala Radio Wala mitandao ya kijamii tofauti na Ulaya na Marekani hata hao wa mjini Ni wachache Wana TV na Radio na huingia mitandao ya kijamii

Na Ni useless sababu wengi wenye TV na waingia mitandao ya kijamii huwa hawaendi kupiga kura huwa wako tu majumbani wanafuatilia uchaguzi wakiwa kwenye sofa set zao!!

CCM tunaenda waliko wapiga kura ndio maana ofisi za CCM ziko kila Kijiji na kila mtaa na ziko active tofauti na vyama vingine
 
CCM huwa hatutaki midahalo ya wagombea Uraisi sababu wapiga kura wengi asilimia 80 wanaishi vijijini na wengi hawana TV Wala Radio Wala mitandao ya kijamii tofauti na ulaya na Marekani hata hao wa mjini Ni wachache Wana TV na Radio na huingia mitandao ya kijamii

Kwa lugha fupi hawajafikishiwa maendeleo!
 
Midahalo ajabu mtu mwingine utasikia Ohhh ifanyike kingereza kwa Nini isiwe kwa kifaransa? Lugha kuu zinazoongoza duniani Ni kingereza na kifaransa kwa Nini wengi wakomae kutaka kingereza tu?
 
Mwishoni mwa juma lililopita nilileta mada hapa jukwaani kuhusu Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Bw. Thabo Mbeki, alivyomkumbuka hayati Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Kwenye bandiko hilo, nami nikatoa maneno mawili matatu kumhusu Rais huyo mstaafu Mkapa, kwa jinsi nilivyomjua mimi, kiumbali.

Moja ya mambo niliyoyakumbuka ni ule mdahalo wa wagombea urais wa mwaka 1995 ambapo ndo ulikuwa uchaguzi wa kwanza katika kurudi kwenye mfumo wa vyama vingi.

Nilisema hivi kuhusu ushiriki wa Rais Mkapa kwenye huo mdahalo:
View attachment 1522615

Hilo bandiko linapatikana hapa.

Siku chache baadaye, mwenzetu Bw. Pascal Mayalla akaleta makala ya January Makamba, ya kumkumbuka marehemu rais huyo mstaafu.

Moja ya mambo ambayo Bw. Makamba aliyazungumzia, ulikuwa ni ule mdahalo wa wagombea urais wa mwaka 1995, mdahalo ambao nadhani ndiyo uliomtambulisha vizuri Rais Mkapa kwa umma wa Watanzania.

Katika kumbukumbu yangu, mimi nilisema Rais Mkapa alifanya vizuri sana kwenye huo mdahalo. Licha ya kwamba hakuna kipimo sahihi cha kupima na kuona yupi alishinda, kwa maoni yangu, Rais Mkapa alishinda mdahalo ule.

Na kwa maoni pia ya January Makamba, nadhani ni sahihi pia nikisema hata yeye January aliona kuwa Mkapa alishinda.

Yeye Bw. Makamba alisema hivi:

View attachment 1522626

Kusoma zaidi alichokiandika Bw. Makamba, bofya hapa.

Tokea mwaka huo wa ‘95, nadhani hatujawahi tena kuwa na mdahalo wa kitaifa wa wagombea urais.

Ningependa sana mwaka huu wa uchaguzi tuwe na mdahalo wa wagombea hiyo nafasi. Ila, sitashikilia pumzi yangu kusubiri hilo kutokea.

Lakini pia, nimeona si vibaya kuleta ombi/ wazo hili hapa.

Ombi ama wazo lenyewe ni kuipata video ya mdahalo wa ‘95.

Nimezunguka sana mtandaoni na huko YouTube, lakini nimeambulia patupu.

Pascal Mayalla wewe ni mwandishi wa habari wa muda mrefu. Naamini bado una uhusiano na watu waliomo kwenye vyumba vya habari vya vyombo vya habari hapa.

Sikumbuki vizuri ni stesheni zipi za runinga ambazo zilirusha matangazo ya ule mdahalo. CTN? ITV? DTV? Radio One labda?

Sasa Bw. Mayalla, unaweza kutumia uzoefu na nyenzo zako ulizonazo kututafutia video [au hata audio] ya huo mdahalo?

Mimi si muangaliaji sana wala si mfuatiliaji sana wa stesheni za runinga za hapa Tanzania. Ila kama kuna stesheni ambazo labda zina chaneli huko kwenye YouTube, zinaweza kuipandisha video ya huo mdahalo kwa faida ya umma.

Kama inawezekana, tusaidie Bw. Mayalla...

Shukran jazilan na ahlan wa sahlan.

Nyani Ngabu,
Hii hoja yako Ina mashiko.
Mie nashauri mdahalo uwe wa Kiingereza ili kuwapa viewers wote including foreigners kujua Tanzania inaweza kuongoza na mtu mwenye uelewa wa maswala kwa kiwango gani....!!!
1995 nilishuhudia mdahalo huo na kiukweli Marehemu Mkapa was the right candidate.

Mwaka huu wa 2020 nategemea kuona list ifuatayo kwenye Mdahalo huo:
 1. John Pombe Magufuli...CCM.
 2. Bernad Callius Membe....ACT.
 3. Tundu Antipas Lissu-CHADEMA.
 4. Ibrahim Haruna Lipumba- CUF.
Angalizo kwa waandaji :LUGHA NI UNG'ENG'E.
 
CCM huwa hatutaki midahalo ya wagombea Uraisi sababu wapiga kura wengi asilimia 80 wanaishi vijijini na wengi hawana TV Wala Radio Wala mitandao ya kijamii tofauti na ulaya na Marekani hata hao wa mjini Ni wachache Wana TV na Radio na huingia mitandao ya kijamii

Na Ni useless sababu wengi wenye TV na waingia mitandao ya kijamii huwa hawaendi kupiga kura huwa wako tu majumbani wanafuatilia uchaguzi wakiwa kwenye sofa set zao!!

CCM tunaenda waliko wapiga kura ndio maana ofisi za CCM ziko kila Kijiji na kila mtaa na ziko active tofauti na vyama vingine
Usitusemee sisi wa vijijini, mbona kuna umeme mpaka kijijini? Unafikri tunautumia kwa mambo gani?
 
Nyani Ngabu,
Hii hoja yako Ina mashiko.
Mie nashauri mdahalo uwe wa Kiingereza ili kuwapa viewers wote including foreigners kujua Tanzania inaweza kuongoza na mtu mwenye uelewa wa maswala kwa kiwango gani....!!!
1995 nilishuhudia mdahalo huo na kiukweli Marehemu Mkapa was the right candidate.

Mwaka huu wa 2020 nategemea kuona list ifuatayo kwenye Mdahalo huo:
 1. John Pombe Magufuli...CCM.
 2. Bernad Callius Membe....ACT.
 3. Tundu Antipas Lissu-CHADEMA.
 4. Ibrahim Haruna Lipumba- CUF.
Angalizo kwa waandaji :LUGHA NI UNG'ENG'E.
Mpaka hapo atakayeshika mkia ameshajulikana.
 
Membe mtoe hapo maana atamwunga mkono TAL! UNG'ENG'E haiwezekani sisi wengine siyo lugha yetu!
 
CCM huwa hatutaki midahalo ya wagombea Uraisi sababu wapiga kura wengi asilimia 80 wanaishi vijijini na wengi hawana TV Wala Radio Wala mitandao ya kijamii tofauti na ulaya na Marekani hata hao wa mjini Ni wachache Wana TV na Radio na huingia mitandao ya kijamii

Na Ni useless sababu wengi wenye TV na waingia mitandao ya kijamii huwa hawaendi kupiga kura huwa wako tu majumbani wanafuatilia uchaguzi wakiwa kwenye sofa set zao!!

CCM tunaenda waliko wapiga kura ndio maana ofisi za CCM ziko kila Kijiji na kila mtaa na ziko active tofauti na vyama vingine

Sababu hasa ya ccm kukimbia midahalo ni uwezo duni wa viongozi wao kwenye kujieleza kwa hoja. Kama kweli ccm inamini watu wengi wa vijijini hawapati taarifa kwa njia hizi, ni kwanini Magufuli kila kitu anafanya mubashara kwenye Media zote? Ukijaribu kuangalia kuhusu kuwepo Mubashara, Magufuli ndio kiongozi aliyekuwa mubashara kuliko kiongozi yoyote aliyewahi kuwa rais wa nchi hii. Na iwapo hatatokea kwenye mdahalo wa safari hii, ni kwa sababu hana uwezo wa mijadala, bali anaweza sehemu za kuhubiri na kuamrisha fullstop.
 
CCM huwa hatutaki midahalo ya wagombea Uraisi sababu wapiga kura wengi asilimia 80 wanaishi vijijini na wengi hawana TV Wala Radio Wala mitandao ya kijamii tofauti na ulaya na Marekani hata hao wa mjini Ni wachache Wana TV na Radio na huingia mitandao ya kijamii

Na Ni useless sababu wengi wenye TV na waingia mitandao ya kijamii huwa hawaendi kupiga kura huwa wako tu majumbani wanafuatilia uchaguzi wakiwa kwenye sofa set zao!!

CCM tunaenda waliko wapiga kura ndio maana ofisi za CCM ziko kila Kijiji na kila mtaa na ziko active tofauti na vyama vingine
What a lame excuse!🤦🏾‍♂️
 
Nyani Ngabu,
Hii hoja yako Ina mashiko.
Mie nashauri mdahalo uwe wa Kiingereza ili kuwapa viewers wote including foreigners kujua Tanzania inaweza kuongoza na mtu mwenye uelewa wa maswala kwa kiwango gani....!!!
1995 nilishuhudia mdahalo huo na kiukweli Marehemu Mkapa was the right candidate.

Mwaka huu wa 2020 nategemea kuona list ifuatayo kwenye Mdahalo huo:
 1. John Pombe Magufuli...CCM.
 2. Bernad Callius Membe....ACT.
 3. Tundu Antipas Lissu-CHADEMA.
 4. Ibrahim Haruna Lipumba- CUF.
Angalizo kwa waandaji :LUGHA NI UNG'ENG'E.
1995 ulikuwa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi tukiiga mataifa ya nje kila kitu Mkapa hakuwa na uzoefu
Nyani Ngabu,
Hii hoja yako Ina mashiko.
Mie nashauri mdahalo uwe wa Kiingereza ili kuwapa viewers wote including foreigners kujua Tanzania inaweza kuongoza na mtu mwenye uelewa wa maswala kwa kiwango gani....!!!
1995 nilishuhudia mdahalo huo na kiukweli Marehemu Mkapa was the right candidate.

Mwaka huu wa 2020 nategemea kuona list ifuatayo kwenye Mdahalo huo:
 1. John Pombe Magufuli...CCM.
 2. Bernad Callius Membe....ACT.
 3. Tundu Antipas Lissu-CHADEMA.
 4. Ibrahim Haruna Lipumba- CUF.
Angalizo kwa waandaji :LUGHA NI UNG'ENG'E.
Vyama vingine mkitaka fanyeni Ruksa CCM hatutashiriki

Mdahalo si lazima kila chama kishiriki kiwe CCM au chochote

Binafsi natoa ruksa vyama vyote vinavyotaka mdahalo ruksa nendeni mkafanye ila CCM hatutashiriki . Mdahalo Ni kitu Cha hiari sio amri kuwa utake usitake lazima ushiriki!!

Vyama vingine endeleleeni kuitisha huo mdahalo ila CCM mtutoe nyie ruksa endeleeni as long as mna pesa za kulipia media
 
Back
Top Bottom