Midahalo ya udasa imefia wapi?

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Midahalo ya udasa imefia wapi?Toka enzi ya chama kimoja kulikuwa, na midahalo moto moto juu ya taifa, na utawala unaohusu mustakabali wa namna ya kujiongoza, lkn chashangaza toka serekali ya awamu ya tano iingie madarakani hakuna cha midahalo, wala makongamano, swali nini kimetokea kwenye utawa wa awamu ya tano?
 
Midahalo ya udasa imefia wapi?toka enzi ya chama kimoja kulikuwa,na midahalo moto moto juu ya taifa,na utawala unaohusu mustakabali wa namna ya kujiongoza,,lkn chashangaza toka serekali ya awamu ya tano iingie madarakani hakuna cha midahalo,wala makongamano,swali nini kimetokea kwenye utawa wa awamu ya tano?
Nilipoona kichwa cha habari nikajua unaijua vizuri historia ya UDASA na ilianza kujifia lini. Ila uliposema kwamba tangia awamu ya tano, nikaona hujui historia ya UDASA.
Ni kweli kabisa enzi za Chama kimoja UDASA ilikuwa ikianzisha na kusimamia midahalo ya kisomi ambayo ilikuwa na tija kubwa sana kwa nchi yetu. Enzi hizo ukisikia kuna Mdahalo wa UDASA basi ulikuwa ukitegemea uchambuzi na upembuzi yakinifu wa mada mbalimbali. Wataalam akina prof. Issa Shivji, Prof. Haroub Othuman (RIP), Prof. Marijorie Mbilinyi, Prof. Ishumi, Prof. Mushi, Prof. Shao, Prof. Kweka (RIP), Prof. Kwanywanyi, Prof. Chris Peter Maina, Dr. Lwaitama, etc walikuwa wakichambua mada kwa kina.
Baada ya ujio wa vyama vingi nikaanza kuona taratibu UDASA inanywea hii ni baada ya akina Dr. Mvungi na wataalam wengine wa sheria pale UDSM kujiunga na mambo ya siasa na kuacha kuwa neutral. Wasomi wakaanza kuwa wanasiasa, wakaacha uchambuzi wakaingia wenyewe kwenye siasa na kuanzia hapo wasomi wa UDSM wakakosa moral authority ya kuwa wachambuzi na badala yake wakawa wanaegemea vyama. UDASA ikafia hapo.

Wakati wa Mkapa kidogo UDASA ilikuwa na kanguvu fulani ka uchambuzi ila ndio ilikuwa inakata roho. Wakati wa JK ikazikwa kabisaaa. Hivyo basi UDASA haijafa kwenye awamu ya tano, ikijifia siku nyiiingi.

Hivi unategemea Prof. Mkumbo atakuwa neutral kweli itakapotakiwa kujadili suala la CHADEMA na ama ACT Wazalendo. Kuna wakati nilisikia ati Prof. Kitila Mkumbo ni Mwenyekiti wa UDASA.

UDASA club imebaki ni club ya kufanyia vikao vya harusi na kunywa michemsho.
 
Umenena kweli
 
..tatizo ni kiingereza.

..kuna mtu hapendi watu wazungumze kiingereza.
 
Dikteta ameua uthubutu na uwezo wa watu kufikiri na kutoa mawazo yao.

Hata kwa upande wa wanachuo. Revolution square pale sasa hivi wanachuo wanafanyia photo shoot kuangalia "make up" zao na milegezo yao.

Wanachuo hawana tofauti na mwanangu wa darasa la 3.

Nchi utopolo inaongozwa na mtu utopolo ili kuifikia future utopolo.
 
Ilikufa na mwanazuoni mahiri prof seith chachage

Continue to rest in peace the greatest professor
 
Kwa mfano nani wa kuendesha mdahalo pale Udasa? Wote wana vyama vyao na wengine wanasubiria kuteuliwa. Unataka wajadili wasiyoyapenda wakubwa wao wakose teuzi. Kimsingi teuzi za kisiasa vyuoni kwa mimi naona ni njia ya kunyamazisha wengine ili mbaki kusubiria kuteuliwa. Udasa ya sasa hivi haina tofauti na daruso
 
Back
Top Bottom