Midahalo ya kisiasa ya makatibu wakuu wa vyama itafanikisha kuongeza mshikamo wa kisiasa.

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Rais Samia Suluhu ameonesha nia ya dhati ya kutaka kufanya kazi na upinzani. Tunaamini Mhe.Rais atakapokutana na viongozi wa vya upinzani watajadiliana mengi hususani mambo yatakayokuza na kuimarisha ushirikiano na demokrasia. Kwa tathmini fupi niliyofanya nimegundua Rais wetu anapenda muafaka ufikiwe mezani kwa njia ya majadiliano.

Tunaenda kufungua kurasa mpya ya vuongozi wa vyama kukaa pamoja na kuzungumza lugha moja yaani siasa na demokrasia. Naamini imani ya Rais wetu itafanikiwa na muafaka wa pamoja kufikiwa bila msuguano wala mkwaruzano.

Swali la kujiuliza: Je, agenda hii yakukutana kwa viongozi itazima baada ya kukutana siku moja au itakuwa endelevu?

Kama itakuwa endelevu, napendekeza kuwepo na jukwaa kwa ajili ya makatibu wakuu (watendaji wakuu wa vyama) wote la kujadiliana hoja mbalimbali, kuchambua kasoro mbalimbali na kupendeza maoni mbalimabali na zaidi jukwaa hilo litumike kwa kila chama kuzielezea sera na falsafa zake kwa watanzania. Napendeza liwe jukwaa la watendaji wa vyama kwa sababu ya majukumu aliyonayo atakayekuwa mwenyekiti wa CCM Taifa.
 
Back
Top Bottom