Microsoft Word Ni Salama ?

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Katika dunia ya sasa watu wengi wamekuwa watumiaji wakubwa sana wa barua pepe kama njia zao kuu za mawasiliano na wateja wao au watu wao wengine ukiacha simu na uandikaji wa barua wa njia za kawaida .

Watu wamekuwa wanatumiana hizi barua pepe ( email kila kikicha na kila mara kwenda na kurudi , wengine wamekuwa wakitumiana vitu muhimu kama mikataba , na nyaraka zingine muhimu kwa njia hii haswa zilizotengenezwa kwa kutumia Microsoft word .)

Bila kujua baadhi ya version za hizi programu zinaweza kupeleka taarifa kuhusu wewe mwenyewe kwa mtu mwingine bila wewe kujua au bila ya wewe kuwa na taarifa na hii imetokea mara nyingi .

Hapa chini nitajadili jinsi programu kama word inavyoweza kutumiwa na mtu mwingine kupata taarifa kuhusu mtengenezaji wa nyaraka husika au computer iliyotumika kutengeneza nyaraka husika .

Unapofungua New Document na kuanza kutengeneza Nyaraka yako , mara nyingi taarifa kadhaa zinatoka katika windows na kuijiweka katika nyaraka hiyo bila ya wewe mtengenezaji kuruhusu kitu kama hichi kufanyika inakuwa katika properties .

Lakini huwa inategemea computer husika imesajiliwa kwa jina gani mfano mzuri angalia hapo chini



Ukitaka kupata kibox hichi unafungua Microsoft word halafu File – Properties , mfano kama ni email imetumwa kwako ukifanya jaribio hili utajua kwa uhakika Document hiyo ilitoka katika computer ya nani kwa sababu jina litajiandika hapo chini .

Wakati mwingine inategemea usajili wa computer hiyo wengine hupenda kutumia majina ya kampuni na kadhalika , ingawa haya majina unaweza kubadilisha kabla ya kutuma Document husika kwenda kwa mtu au watu husika .

Katika Programu ya Microsoft Word pia kuna kitu kinaitwa Word’s Revision Tracking hichi kitu kikiwashwa inasababisha Word kuweka kumbukumbu ya mabadiliyo yoyote yanayofanywa katika document husika , mfano kama document imetumwa kwa watu zaidi ya 10 na wote wakaiangalia na kufanyia mabadiliko ikirudishwa kwako itakuja na taarifa za nini walichofanya na kumbukumbu zingine kuhusu computer husika .



Ukitaka kupata Kitufe hicho unaenda katika Tools kisha Options halafu track changes hapo ndipo Settings za tracking unavyoweza kubadilisha ili mtu wa upande wa pili asiweze kukutrack .

HIZI NDIO NJIA NYEPESI ZA KUWEZA KUEPUKANA NA BAADHI YA KADHIA

1 ) Unapotuma na kupokea Document kumbuka ku toggle “highlight changes on screen” na “highlight changes on printed document”

2) Kama unataka kutuma kopy safi ya Microsoft word kumbuka kutumia Accept All

3) Kama unataka kufuta majina ya wote ambao walichangia kitu Fulani katika Document Husika fungua Document mpya na Paste kilichomo kisha Accepted , kisha weka On “track changes” halafu fungua “compare documents” kulinganisha Document ya kwanza na hiyo mpya ambayo haina taarifa za wahusika kama zinafanana au la

4 ) Kuna kitu kinaitwa “allow fast saves” Hii inatakiwa Iwe Off
5) Kama mtumiwa hatakiwi kubadilisha Chochote unatakiwa Uhamishie Document husika katika Mfumo wa PDF halafu Protect Changes , ingawa kama atataka kubadili chochote inabidi awe na programu inayoweza Kubadili kwenda Word au Document Zingine .

6 ) Wakati mwingine fikiria Kutumia programu za ziada za kampuni zingine ambazo zinaweza kuficha ID zako kabla ya kutuma Email au Document husika kwa watu mfano kuna Payne Consulting’s MetaData Assistant

7 ) Kuna tools kisha Protect Document

8 ) File halafu Permision ( hapo unaweza kuongezea baadhi ya vitu )

Hizo ni baadhi ya njia tu , ingawa kuna njia nyingi zaidi nyingine nyepesi na ngumu kwa sababu programu mpya zinatengenezwa kila kukicha na zingine zinazidi kuimarishwa zaidi kwahiyo nilivyotoa hapo sio mwisho wa kuweza kuwa na document salama .
 
Back
Top Bottom