Microsoft Outlook inakuletea "Personal Vault" hii ni nzuri kwako kwa sababu hii!

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
7,305
8,655
Kwa wale watumiaji wa Barua pepe Kutoka Microsoft yaani hotmail na outlook tunafahamu uwepo wa OneDrive, hii ni online cloud storage kama jinsi ilivyo Google Drive, tofauti yake na google drive ni kwamba hii inakupa 5GB initial storage wakati GDrive inakupa 15GB lakini *Though zote unaweza kuongeza storage kwa ku Purchase* ila tofauti kubwa na ya msingi imeletwa na Microsoft Kupita OneDrive Personal Vault, hii hapa inakuwa na security ya hali ya juu kuingia tu kwenye folder lake mpaka utumiwe code kwenye simu yako kisha uiingize.

Uzuri wa hii ni kwamba kila baada ya dk 20 ya kutokutumia huwa inajilock, na ukitaka kuingia humo mpaka uingize code!, kwahio kwa wale wapenzi wa kustore data online hii ni mbinu ambayo ipo very safe!

Unaweza kuhifadhi Risiti zako za biashara, namba za kadi muhimu, leseni na mengine mengi ya Muhimu!

Niwakumbushe tu, Flash yako inaweza kupotea, simu pia na hata computer, au hata files zikaliwa na virus.. usisahau kutunza information zako za muhimu Cloud Storage!

Karibu sana Microsoft One Drive!

Khan


1569675562586.png
 
Mbona hii sio mpya??au Luna kitu kimeongezeka..

Maana naitumia miaka sasa kuhifazi documents,pictures etc.
 
Mbona hii sio mpya??au Luna kitu kimeongezeka..

Maana naitumia miaka sasa kuhifazi documents,pictures etc.
ingia one drive kuna kitu kimeongezeka, kama uonavyo kwenye picha hapo juu
 
Back
Top Bottom