Microsoft Goldpartner

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,201
219
Miezi 2 iliyopita Microsoft ilianza kufuatilia maduka na watu wanaouza bidhaa zake ambazo hazikusajiliwa na wengine ambazo sio halali , wengi walikamatwa na maduka mengi yalilalizimika kufunga biashara zao kwa siku kadhaa kuogopa vyombo vya sheria visiingie katika maduka yao au katika office zao kwa ajili ya kukagua .

Kuna workshop kama New Age ambayo mimi niliwahi kufanya kazi lakini kwa sasa sifanyi kazi hapo . maduka maarufu kama Prince Samora Sunrise Kariakoo , kuna kampuni kama Power Computers ambayo ina uhusiano na Ideal Computers hawa wote walikutana na kash kash hii ingawa maduka mengine hapo hayakuonekana katika vyombo vya habari wale waliokuwa wanaripoti matukio haya wanajua na wahariri wao .

Kilichonifanya niwe na shauku leo ya kuuangalia tena suala hili , ni moja ya kampuni hizi Ideal Computers ambayo inauhusiano na Power Computers , inatakiwa ieleweke kwamba Power Computers walipovamiwa pale Dukani kwao Barabara ya Morogoro baadaye kidogo wakahama ule mtaa na kwenda sehemu ingine karibu na pale .

Leo nimeona Tangazo katika Gazeti la The Guardian kwamba Ideal Computers ni Gold Partner wa Microsoft na kweli ukienda katika baadhi ya office zao unakuta matangazo mengi sana ya Microsoft na kampuni zingine kwamba wana uhusiano na vyeti vya kufanya kazi vyema

Ukiangalia katika Microsoft kumeandikwa hivi Gold Certified Partners represent the highest level of competence and expertise with Microsoft technologies, and have the closest working relationship with Microsoft.


Sasa nauliza hiyo GOLDERN PARTNER SHIP imetokea wapi tena wakati miezi 2 iliyopita tu walikamatwa na bidhaa ambazo sio halali za Microsoft , wanataka kutuambia nini kama sio kudanganya ummah ? hii ni kampuni kubwa imeuza sana kamputa na bidhaa zingine kwa serikali na watu wengine bidhaa hizo sio halali wote hawa hawajaamua tu kwenda katika vyombo vya sheria kudai haki zao .

Umefikia wakati sasa wizara za serikali zinazohusiana na mambo haya ziingilie kati mpaka katika mambo , kama serikali imeshindwa kushugulikia haya au haina uwezo huo basi iweke wazi ili jitihada zingine zifanyike ili kuhakikisha haki inatendeka na watu kufurahia bidhaa hizi wakati wote wa maisha yao .

Kuna siku niliambiwa nisiwe naweka majina ya kampuni au watu wakati nawasilisha mada kama hizi kwa sababu za kibiashara , lakini mtu au kampuni au kikundi cha watu wanapoamua kukiuka miiko ya biashara hiyo basi haina haja tena ya kumficha tena atapelekewa ujumbe wake ajue anachofanya sio halali .

USIKU MWEMA
 
Back
Top Bottom