Microbiologists ni watu muhimu sana kwenye kufanya mapinduzi katika sekta ya kilimo

ormystatus

Member
Nov 3, 2019
89
176
Habari Jamvini! HAYA NI MAWAZO YANGU TU.

Ukiachana na uwepo wa zana za kisasa kama vile tractors pamoja na wataalamu wa kilimo kama vile agronomists na wataalamu wengine waliosomea mambo ya kilimo ili Tanzania tuweze kufanya mapinduzi katika sekta ya kilimo MICROBIOGISTS niwatu muhimu sana katika kufikia mapinduzi hayo.

MICROBIOLOGIST NI NANI?
Microbiologist ni mtu aliyesoma science of microbiology ambalo ni somo kuhusiana na viumbe wadogo kabisa wasioweza kuonekana kwa macho"microorganisms" kama vile virusi, bacteria na fangasi. Microbiology imegawanyika katika sehemu tofauti tofauti kama vile AGRICULTURAL MICROBIOLOGY, MEDICAL MICROBIOLOGY na INDUSTRIAL MICROBIOLOGY. Hata hivo kulingana na kichwa cha habari hapa tutazungumzia Agricultural microbiology.

AGRICULTURAL MICROBIOLOGY inahusisha microorganims wenye faida au hasara kw mmea aidha moja kwa moja au indirectly ambao mwisho wa siku wanawez kuongeza au kupunguza uzalishaji katika sekta ya kilimo.MICROBIOLOGISTS ni watu muhimu sana katika kuleta maendeleo makubwa kwnye sekta ya kilimo kwa sababu wanauwezo wa kufanya zoezi zima la uchunguzi wakiambatana au kutoambatana n wataalamu wengine wa kilimo kuhusiana n microorganisms wenye tija katika kilimo kisha kuwatenga microoganisms hao na kuwazalisha massively na kutumika endapo serikali yetu itawekeza vya kutosha katik sekta hii ya kilimo kwa kujenga vituo vya kutosha nchini vyenye maabara bora ambazo zitatumika kufanyia experiment , kuwa na wataalamu wa kutosha (asilimia kubwa Watanzania) watakaoconduct hizo practicals na kuziapply kwenye mashamba, kujenga angalau irrigation scheme kubwa na ya imara pamoja naza za kisasa, hii itasidia kuongeza uzalishaji ikimbatana na matumizi ya mbegu za kisasa,mbolea na madawa mengine/upatikanaji wa mazao mengi katika eneo dogo.

Kabla sijataja baadhi ya microorganisms wenye faida kwa mimea"mazao" na faida zao, kwanza microorganims hawa wamegawanyika katik makundi mawili ambayo ni

1:ENDOPHYTIC MICROORGANISMS (SYMBIONT MICROORGANISMS)
Hawa wanaishi kwenye tishu za mimea(sehemuya ndani ya mmea)

2:NON-SYMBIONT MICROORGANISM.
Hawa wanapatikana kwenye udongo.

WAFUATAO NI BAADHI YA MICROORGANISMS NA FAIDA ZAO KWA MIMEA"MAZAO". Kama vile Alizeti, mpung na mahindi

1:WANAOPATIKANA KWENYE TISHUZ MIMEA
•Methylobacterium, Azospirillum, Herbaspirillum, Burkholderia, Rhizobium spp.
Hawa ni endophytic bacteria wanaopromote ukuaji wa mpunga, hawasababishi magonjwa kwa mmea na wanaukinga mmea dhidi ya fangasi wenye madhara

•Enterobacter na Burkholderia
Hawa wanapromote ukuji wa alizeti

•Bacillus subtilis
Huyu anapunguza ukuaji wa microorganisms wenye madhara kwa mpunga, anausaidia mmea kuwa na ustahimilivu wakati wa hali ngumu kwa kuupa mmea vinasaba vinavoukinga mmea wakati wa stress mfano inaupa mti wa zao la mahindi ustahimilivu wakati ambao hamna maji yakutosha na pia anapromote ukuaji kwa alizeti

•Bacillus cereus
Anaukinga mpunga dhidi ugonjwa wa rice blust unaosababishwa na fangasi aitwae magnaporthe oryzae na pia Bacillus spp(Bacillus species) zinapunguza uvamizi wa microorganisms wenye madhara kwa zao la mpunga.

•Enterobacter, Azospirillum, Bacillus
Wanazalisha homoni ya auxin ambayo inasaidia mmea kukua

2:WANAOPATIKAN KWENYE UDONGO
•Azotobacter, cyanobacteria, Rhizobium spp
Hawa wanajulika kam biofertilizer kwa kimombo,wanapatikn kwenye surface ya mizizi , wanafanya nitrogen fixation ambayo ni muhimu sana kwa legumenous plants(mimea jamii ya kunde kikwetu)

•Pseudomanas
Hawa ni phosphate solubilizing bacteria

Nyongeza
•Baadhi ya species zinazalisha antibiotic

•Microorganims wenye faida kwa mmea wnaufanya udongoushikmane vizuri, kuuongezea idongo kiwango cha organic matter kwani wapo wanaoozesha mimea na wanyama waliokufa

KWA UJUMLA MICROOOGANISMS WANAUSAIDIA MMEA KUKUA KWA KUFANYAKAZI KU TATU AMBAZO NI,

1:Kuzalisha compounds kwa mmea

2:Kuongezea mmea kasi ya uchukuaji wa madini na lishe kutoka kwenye udongo.

3:Kupunguza au kuzuia kabisa magonjwa kwa mmea.

VIDOLE VINAUMA ASEE, niishie hapa.
#TANZANIA_KAMA_ISRAEL. Amiin

BAADHI YA SOURCES:
•Agricultural microbiology ‎Medtech; 3rd edition (January 1, 2020).

ResearchGate | Find and share research
 
Mkuu, ukichukua udongo kidogo wenye mboji, ukauweka kwenye maji yenye sukari guru, Kisha ukapitisha hewa labda kwa siku kama nne...

Ningependa kujua practice kama hiyo ni njema na inaweza kuongeza na inaweza kutumiwa kuongeza microorganisms kwenye shamba kwa kumwagia hiyo soln kwenye udongo.
 
Mkuu, ukichukua udongo kidogo wenye mboji, ukauweka kwenye maji yenye sukari guru, Kisha ukapitisha hewa labda kwa siku kama nne...
Ni kweli sugar solution inaweza kutumika kuzalishia soil microbes kwa sababu sukari haswahaswa ile simple sugar(glucose)ni chanzo cha carbon ambayo soil microbes wanatumia ili wapat chakula, lakini concetration kubwa ya sukari inazuia ukuaji kwa bacteria kwa sababu inasababisha osmosis (maji yanatoka kwa bacteria kwenda kwa sukari).

Ili kupata wale viumbe waliokusudiwa selective media inatakiwa zitumike ili ikue aina fulani tu ya viumbe na wengine wasikue.
 
Ni kweli sugar solution inaweza kutumika kuzalishia soil microbes kwa sababu sukari haswahaswa ile simple sugar(glucose)ni chanzo cha carbon ambayo soil microbes wanatumia ili wapat chakula selective media inatakiwa zitumike ili ikue aina fulani tu ya viumbe na wengine wasikue...
Vipi kuhusu nematode maana kwenye soil yoyote uwezakano wakukuta nematodes ni mkubwa sana
 
Vipi kuhusu nematode maana kwenye soil yoyote uwezakano wakukuta nematodes ni mkubwa sana
Ni kweli nemotodes(plant-parasitic nematodes) wanapatikana kwenye udongo na wanashambulia sna maeneo ya chini ya mmea kama vile mizizi, ukiachana tu matumii ya madawa yanayoua hawa nemotodes lakini pia bacteria wa genera Bacillus, Pseudomonas na Pasteuria wanaweza kutumika kufanya biological control kwa hawa nematodes kwani wanapatikana kwa kiasi kikubwa kwenye udongo na wanauwezo wa kuwauwa nematodes hawa kwa njia tofautitofauti kama vile-:

•kuzalisha sumu inayowathiri nematodes na kutokuw na madhara kwa mmea.

•kuzalisha antibiotics

•kuzalisha enzymes wenye madhara kwa hawa nematodes

•kushindania lishe na nematodes .
 
Back
Top Bottom