Michuzi amekuwa mpiga picha wa ikulu?

Mwangaza

Senior Member
Feb 26, 2008
198
64
Hii blog ya michuz kila siku inaweka habari za JK , JK , JK tuuu!! inaboa sasa..!!!
Mara JK , kafanya hivi, mara JK atembelewa na flani, mara JK kaenda huku, Mara birthday ya mke wa JK, mara JK katungiwa kitabu..kila siku JK.. JK ..JK ..JK!!
Sawa ni Rais lkn sio kila habari yake tunaitaka.
Au Michuzi ameshakuwa mpiga picha wa rais??
Au michuzi naye yupo UWT??
Au Michuzi anafanya kumpigia promo mzee kurudishia umaarufu wake ulioporomoka?? and then...??

USHAURI WA BURE:
Michuzi japokuwa tunajua brog ni mali yako binafsi, lkn jaribu kuweta habari za jamii zaid, hiz za JK wanaozitaka wanajua pakuzipata..wataenda kwenye site za Uhuru, daily news, mtanzania,ikulu na kwenye blogs,facebook na website zake (JK) kibao zilizofunguliwa na watu wake.
 
Michuzi ni mganga njaa tu hana jipya la kuieleza jamii alichobakisha ni kujikomba naye apate vitripu vya nje darasa hana asipojikomba atakula nini?
 
MICHUZI hana jipya,na iyo blog yake haina lolote ambalo jamii inaweza kufaidika nalo zaidi ya kujikombakomba tu kwa wakubwa.
 
USHAURI WA BURE:
Michuzi japokuwa tunajua brog ni mali yako binafsi, lkn jaribu kuweta habari za jamii zaid, hiz za JK wanaozitaka wanajua pakuzipata..wataenda kwenye site za Uhuru, daily news, mtanzania,ikulu na kwenye blogs,facebook na website zake (JK) kibao zilizofunguliwa na watu wake.

Mkuu mtendee haki japo kidogo.
Nilichowahi kusikia ni kuwa Michuzi ni mpiga picha wa TSN na kama ni taassisi ya serikali basi kupata mialiko hii ambayo mh. Rais anakuwepo ni kitu cha kawaida na watu wakikualika wanategemea utapost habari/picha zao huko usipofanay hivyo unaweza kuwakatisha tamaa wasikualike tena siku nyingine.

Binafsi sipendezwi na habari zote anazopost kwenye blog yake lakini naheshimu haki yake ya yeye kupost kile anachoona ni sahihi, maana hizi picha na stori za Jk zinaweza zisikufurahishe wewe lkn wako wengine zinaowafurahisha.

Kwa ushauri tu mwandikie email mpe ushauri wako utamsaidia kuboresha.....ukiona inakera sana na hasikiliziushauri wako basi achana na blog yake na kama wote wataacha yeye mwenyewe atashtuka sababu hata namba ya clicks kwa siku zitapungua, vinginevyo pamoja na madaifu yaliyopo kwenye hiyo blog michuzi anahitaji pongezi maana blog yake imekuwa ikisaidia sana wengine kupata taarifa mbalimbali.
 
Mimi huwa najiuliza kama michuzi blog ni notice board ya watu walioko nje kutundika matangazo yao ya wapi watakutana, kuna party wapi na kuturingishia sisi ambao hatupo huko...! Mara mkutano wa Watanzania Reading, Mkutano wa Watanzania Italy, mkutano wa watanzania Liberia...! Mara Flavor night Washington...! Sijawahi kuona matangazo ya mkutano wa kuchangia shule, hospitali au maji...!
 
Huyu Utingo nadhani jina hilo siyo la utani! Kama hawa kina Utingo ndiyo JF Senior Expert Members wa JF, basi Forum hii inaelekea kaburini. Shame!
 
Hii blog ya michuz kila siku inaweka habari za JK , JK , JK tuuu!! inaboa sasa..!!!
Mara JK , kafanya hivi, mara JK atembelewa na flani, mara JK kaenda huku, Mara birthday ya mke wa JK, mara JK katungiwa kitabu..kila siku JK.. JK ..JK ..JK!!
Sawa ni Rais lkn sio kila habari yake tunaitaka.
Au Michuzi ameshakuwa mpiga picha wa rais??
Au michuzi naye yupo UWT??
Au Michuzi anafanya kumpigia promo mzee kurudishia umaarufu wake ulioporomoka?? and then...??

USHAURI WA BURE:
Michuzi japokuwa tunajua brog ni mali yako binafsi, lkn jaribu kuweta habari za jamii zaid, hiz za JK wanaozitaka wanajua pakuzipata..wataenda kwenye site za Uhuru, daily news, mtanzania,ikulu na kwenye blogs,facebook na website zake (JK) kibao zilizofunguliwa na watu wake.

Blog ya michuzi ni blog binafsi na wala siyo ya serikali. Anayo haki ya kutomchukia JK na ya kuweka picha azitakazo, kama ambavyo wewe unayo haki ya kuacha kuitembelea kama kweli inaboa kiasi hiko.
 
Ni kibaraka tu huyo.... Kwanza habari zingine ambazo hazihusiani na IKULU anaziiba kwenye blog za watu mbali mbali na kupost kwake.... Ukitaka kuamini tembelea blog ya haki ngowi...ukiiishakuta post shortly utaikuta kwa Michuzi..bila ku quote source..
 
Kama JF ilivyo kibaraka kwa CDM?
 
Siku hizi comments kwenye blog yake zimeshuka sana. By the time JK anaachia ngazi 2015 sidhani kama hiyo blog itakuwa na any advert!
 
jaman wana JF, sie ni kupinga tu kila kitu. Comments karibu zote hapo watu wanapaka tuuuuuu! completely negativ minded...

Zingatia,
1.kwan unalazimishwa kutembelea?
2.Mbona kuna blogu nying sana jamani, kwann Michuz tu?
3.Nyinyi wenyewe mnatembelea kwa wingi, mnampa hits na mnapandisha chatini-huwa mnafuata anachopost, kwann hamuend kwenye blogu nyingine kama http://mafisaditanzania.blogspot.com/...?, michuzi hamuit mtu mle, mnaenda wenyewe. so ipotezeen kama vp.

Najua mnataka apost nini ili awakune..! tengezenni na nyinyi blogu zenu bana!

Hamna kazi?
 
Huyu jamaa ni mfanyakazi wa serikali na lazima amtumikie kafiri kusudi apate ujira wako..
 
Kwani mnalazimishwa kusoma blog yake?
Michuzi ni mwajiriwa wa serikali, lazima apulizie kibarua chake.....huenda siku moja akawa mpiga picha wa ikulu.
Mie ningekushauri wewe uliyeanzisha hii thread kuanzisha blog yako, nawe unaweza kuamua ni habari gani uiweke na kusomwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom