Michuano ya Kombe la Dunia 2022 kuchezwa mwezi Novemba na Desemba badala ya Juni na Julai

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
MICHUANO YA KOMBE LA DUNIANI 2022 KUFANYIKA MWEZI NOVEMBA NA DESEMBA

Shirikisho la soka Duniani (FIFA) limeweka wazi kuwa michuano ya kombe la Dunia 2022 inayotarajiwa kichezwa nchini Qatar inatechezwa kati ya mwezi Novemba na Disemba.

Katika taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo leo mechi ya ufunguzi itapigwa kwenye uwanja wa Al Bayt wenye uwezo wa kubeba mashabiki takribani 60,000.

Sababu za michuano hiyo kupigwa kwenye kipindi hicho cha baridi ni kutokana na kuwepo kwa joto kali kwenye kipindi cha kawaida cha michuano hiyo yaani Mwezi Juni na Julai kwenye ukanda wa nchi za uarabuni.

Mechi ya fainali ya michuano hiyo ya kihistoria itachezwa Disemba 18,2020 kwenye uwanja wa Lusail unaoweza kubeba watu takribani 80,000.
 
Huu uamuzi maana yake ni kwamba, msimu wa 2022/2023 utaathirika kiratiba dunia nzima.

Ngoja tuanze kusikia matamko ya mashirikisho mbali mbali ya mpira wa miguu duniani kote.
 
Waarabu si wana hela?si waweke tu ma ac ya kumwaga kila Mahali
Kwanza mafuta bure umeme bure kwanini kutuharibia ratiba?
 
Back
Top Bottom