Nimesoma Mass Communication, natafuta kazi

A love

Member
May 17, 2021
93
119
Jamani napenda kuwashukuru wana JF wenzangu, kupitia nyinyi nimeweza kupata kazi japo ilikuwa ni ya muda mfupi lakini kwa nilichopata ninawashukuru sana tena sana.

Haya maisha inabidi tusaidiane, nimekuwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii lakini huku pamenifanya nijione nami ni mtu kati ya watu, nilidharaulika hata kwa familia, nilionekana mzigo lakini kupitia connections za humu niliweza kusimama.

Ninarudi tena kwenu, nilihitimu mass communication, kazi niliyoipata kupitia JF haikuwa ya kudumu, ninaomba kwa wenye connections huu uzi ni kwa ajili yetu, tusaidiane jamani kwa anayefanya kazi yoyote akomenti humu ,hata kusaidiana kimawazo tuu unaweza kumuokoa ndg yako ijapokuwa hamfahamiani.

Tupeane michongo ya kazi, mimi kwa sasa sina kabisa kazi, karibuni wakuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom