Michezo ya utotoni!!!

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,585
5,758
Salaam wana JF
Wakati nikiwa mdogo nilipenda sana kucheza kombolela i.e Mchezo wa kujificha na kuanza kutafutana.
Nikiukumbuka huu mchezo natamani sana nirudi kuwa kama mtoto.
Je wewe utotoni ulipenda Mchezo gani?
 
mi nilikuewa napenda mchezo wa baba na mama,, halafu namchukua mama tunaenda kazini. Huko tuendako ni mafichoni, tunanjunji weee tukichoka tunarudi kuungana na wenzetu tunasema tumeshatoka kazini
 
mi nilikuewa napenda mchezo wa baba na mama,, halafu namchukua mama tunaenda kazini. Huko tuendako ni mafichoni, tunanjunji weee tukichoka tunarudi kuungana na wenzetu tunasema tumeshatoka kazini

teh teh teh hivi watoto wa siku hizi bado wanacheza mchezo huo??
 
Nikiona maeneo tuliyokuwa tunachezea huwa nashangaa pamebalidika sana...pamekuwa padogooo na hata sikuti watoto wakicheza ile michezo yetu... au watoto wa siku hizi ni wa dotcom??
 
Zamani tulikuwa tunatengeneza baiskeli za miti...yaani msimu wa baiskeli kila mtoto anatengeneza yake....
 
Hahahaa!! Michezo zamani bwana! enzi za KIBUNZI.Tulikua tunaimba: kibunzi,kibunzi chameeme chameeme kajambila ushuuzi...
 
Tulicheza mchezo wa pia 'enkuyo' tuliita mchezo huo. Tulishindana kuogelea kwenye mabawa ya mvua 'kalego' au kule mtoni 'kanyonyi'.
Nakumbuka 'etobito' inamnyonyoa ndege aina ya 'akaiba', ........ kulikuwa hakuna kukosea.
Kuna nani bingwa wa 'eilobo' kuvua kambare. We acha tu!
Ukistuka siku imeisha, mpira cha ndimu hujapiga lakini inabidi urudi nyumbani na kuni (enkwi).
Mbuzi na ng'ombe nao hawajarudishwsa nyumbani. Nilijua namna ya kujitayarisha ka ajili ya viboko.
Nitaongeza mingine, zamani ilikuwa raha sana.
 
Dah, enzi zileee..! Nakumbuka siku moja nilikua najificha kwa bahati mbaya nikakanyaga msumali wenye kutu... Ila michezo mingine ilkuwa hatari, Mf. PUTUKA..!
 
duuh michezo mingi mno kioo, kidali poo,kombolela,vichupa,mateka,rede ya wote,kuruka kamba,kibaba baba na kimama mama,vitambaa vya kuokota kwa fundi cherehani pia michezo ya zamani wasanii wanaiimba nowdays
 
Mi nakumbuka kucheza chandimu,tulikuwa hatufuati ile sheria ya watu 11 kila upande,ilikuwa ilimradi mlingane idadi.Ukifika umechelewa,huingii uwanjani mpaka upate pair yako ya timu pinzani,kwa kuwa hatukuwa na jersey,tulikuwa tunapeana zamu,sisi leo tunavaa mashati ninyi mtacheza bare chest.Mtu akishika mpira kwa mkono tunasema enzi(hands),inapigwa faulo.Tulikuwa tuna aina tatu za wachezaji,kipa anakaa golini,mabeki wanakaa mbele ya kipa na ma-forward wao ni daima mbele,nyuma mwiko hata timu ikizidiwa.Mpira sio dakika 90 tu,ni mpaka jua lizame,dah!I miss my childhood moments.
 
Katika michezo yoote ya utotoni,sitasahau MSINGI BOMOA,ukiinama tu unapewa teke la masaburi.Kujiunga na mchezo ilikuwa ni bure ila ukitaka kuacha ilikuwa ni lazima utoe hela(sh.20) kipindi kile. Basi kuna siku nilikuwa nina nawa uwani nikijiandaa kwenda shule,jamaa alinivizia akanipa bonge la teke mpaka nikadondokea kwenye dishi la maji.Siku-back down,na mimi kuna siku nilimvizia jikoni anamimina chai ndani ya vacuum flask,nilimpa bonge la teke la masaburi mpaka akadondoka na kupasua ile chupa ya chai na kuungua mikono.Haikuchukua dakika 10,akaja na mama yake ili anipige,kilichotokea ni mama kuniweka nyuma yake halafu kibabe akamuuliza;kwa hiyo unasemaje?yule mama akasepa na mwanae huku kanuna ile mbaya.
 
Yoote mmetaja, mi nakumbuka nlipokuwa naweka kijiti ktk nywele ili mama asahau pindi ninapoongea nae asikumbuke makosa nlofanya cku hyo. Haaah.
 
Ebwanae TIKIRI!!!Halafu kuna kuchonganishana kpigana bila sababu,Siku moja nilichonganishwa na kaka yangu nipigane na rafiki yangu,ebwana ee sitoisahau hiyo siku nilidundwa vibaya halafu bado dingi alinipa kipigo heavy!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom