Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,269
- 40,054
Nakumbuka nilipokuwa mdogo, shule ya msingi nilikwenda kumtembelea ndugu yangu mmoja, alikuwa anafanya kazi kijiji kimoja huko kanda ya ziwa, miaka hiyo.
Baada ya kufika kule kijijini, nikakutana na marafiki wa rika langu; wakawa wananitembeza mtaa kwa mtaa, ili niweze kufahamu mazingira ya huko kijijini.
Siku iliyofuata, tukapanga tuende tukawinde ndege; tukatafuta mapila yale ya kuvutika, pamoja na waya. Tukachukua vipande vidogo vitatu (3) vya miti; vile vipande, tukavigongelea chini vikatengeneza umbo la pembe tatu.
Vipande viwili tukavifunga mapila, na kile cha tatu kikawa ni kiegemeo cha mpira, ili tutakapofyatua mtego uweze kupiga ndege.
Baada ya kuweka mtego vizuri, tukamwagia pumba na tukaunganisha na kamba ndefu, ili ndege wakifika tuweze kufyatua mtego.
Baada ya lisaa kama limoja hivi, walikuja ndege wengi wakaanza kula pumba. Ndipo mmoja wetu, akasema sasa ni muda muafaka wa kufyatua mtego; baada ya kufyatua mtego, ndege kama saba hivi walipigwa, wakashindwa kupaa, na tukaenda kuwakamata.
Baada ya hapo, tukaanza kuseti tena mtego; wakati tunarudishia kijiti cha pili; kile cha kwanza kilifyatuka na kikaja kunipiga kwenye korodani moja; hapo niliona giza ghafla pamoja na maumivu makali, nikasema hapa roho ndio inaanza kuchomoka nini!
Nilijigeuza geuza huku nikisikilizia maumivu kwa muda mrefu kidogo; baada ya maumivu kupungua, nikawaambia marafiki zangu tuondoke, hapa sio mahali salama.
Katika ukuaji wangu, nikajua hapa uzazi ulishaharibika. Lakini, Mungu mkubwa, baada ya miaka kwenda hakukuwa na tatizo; na hatimaye nakimbilia kuja kulea wajukuu.
Ila michezo ya utotoni, ni hatari katika ukuaji wa mtoto.