Bipolar
Member
- Apr 29, 2016
- 44
- 49
Tukumbushane michezo ya utotoni kwa wale wa miaka ya tisini kurudi nyuma.
Naanza na Kombolela, Dama, Ola (huu ulikuwa zaidi mchezo wa wasichana kujaza chupa mchanga na kukwepa mpira).
Mashuleni kulikuwa pia kukimbia asubuhi (mchaka mchaka) huku tukiimba "Idd Amini akifa mimi siwezi kulia nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba."
Vizazi vya siku hizi havijui hii michezo na ilisaidia sana, kujenga mahusiano na afya ya mwili. Siku hizi watoto wanashinda tu ndani na computer games hata unakuta hawajuani na mara nyingi wanaongezeka sana uzito jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.
Kuna kitu tumepoteza kama jamii. Tupia na wewe michezo unayoikumbuka...