Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing yawa jukwaa la kuonyesha uvumbuzi wa teknolojia ya China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
Tovuti ya gazeti la Marekani “Los Angeles Times” tarehe 19 mwezi huu iliripoti kuwa vifaa vya kisasa vya kiteknolojia kwenye Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing vinawavutia watu wengi duniani, ikiwa ni pamoja na mgahawa unaotoa huduma wenyewe, roboti ya usimamizi kwenye hoteli na nyinginezo. Michezo hiyo imekuwa jukwaa la kuonyesha uvumbuzi wa teknolojia ya China.

Ripoti hiyo imesema, katika wiki kadhaa zilizopita mgahawa unaotoa huduma wenyewe uliopo kwenye kituo kikuu cha vyombo vya habari cha Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing umewavutia watu wengi duniani.

Watazamaji wa televisheni na watumiaji wa mitandao ya kijamii wote wanapenda kusoma habari kama hizo: kikapu kinatia maji ya moto ndani ya bakuli lenye chakula cha “wonton” zilizogandishwa, baada ya dakika chache tu, wonton zinazochemka na kuwekwa kwenye bakuli la plasitiki, kisha bakuli linapelekwa hadi kwa mteja kwa kutumia mkanda wa kuchukulia bila ya utendaji wowote wa binadamu. Baada ya taa kuwaka, chakula kitafikishwa mezani.

Kwenye mgahawa huo, kuna mpishi wa roboti, pia kuna mhudumu wa baa wa roboti. Wahudumu hao wa roboti wanatembea kwenye njia iliyoko juu ya wateja, chakula kinawekwa mezani kwa kutumia kamba.

Wasimamizi wa mgahawa huo wanasema huduma hiyo ya kisasa ya kutengeneza chakula ni kwa ajili ya kupunguza kusogeleana kati ya watu, ili kuzuia usambazaji wa virusi vya Corona.

Ripoti hiyo pia imesema roboti inatumika sana kwenye eneo la ndani la michezo hiyo ya Olimpiki. Ndani ya jumba la michezo na hoteli ya wanahabari, kuna roboti zinazotoa huduma, ambazo zinaweza kupanda lifti zenyewe. Baadhi ya roboti zinaweza kunyunyiza dawa ya kuua vijidudu, au zinaweza kuua vijidudu kwa kutumia mionzi ya ultraviolet. Baadhi ya wakati, zinaweza kutambua watu wasiovaa barakoa, na kuwakumbusha wavae.

Licha ya kutoa huduma kwa ajili ya kuzuia janga la Corona, teknolojia hizo za kisasa pia zinatumika kwenye sekta nyingine.

Wanahabari wanafanya kazi kuanzia asubuhi mapema hadi usiku wa manane, kwenye kituo kikuu cha vyombo vya habari kuna vibanda takriban 20 vya mapumziko kwa wanahabari hao. Wanahabari wanaweza kufungua mlango wa kibanda kwa kutumia QR Code, kisha kuweza kulala ndani ya chumba hicho chenye kitanda kimoja cha kisasa.

Mtu anaweza kukipandisha au kukishusha kitanda hicho, na mashuka yanayotumiwa mara moja tu na kutupwa yamo ndani ya kabati la ukutani.

274808196_4688462364598373_6818722479726627388_n.png


274694343_4688461944598415_8790796831198910120_n.png

274722889_4688462697931673_5317951241943267306_n.png
 
Hongera kwao Wavimba Macho,Kwani Speed wanayokwenda nayo kwenye teknolojia mpya ni kubwa sana.
 
Back
Top Bottom