Michezo ya bonanza(Dubwika) imekuwa mingi mitaani watoto wanaathirika, serikali iangalie hilo

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
666
Mchezo ya Mchina, maarufu kama dubwika iko mingi sana mitaani kutokana na namna yetu ya maisha inawaathiri watoto kwa kiasi kikubwa

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Januari 23, 2019 iliamuru kutokuwa na matangazo ya kwenye redio na tv kwa michezo ya kubahatisha ambayo walilenga michezo ya biko na mingine ya kufanana na hiyo ili kuwalinda watoto lakini walisahahu michezo hii mingine ambayo ina athari sawa na michezo hiyo

Kutokana na michezo hii kutokuwa included kwenye udhibiti imefanya iwe inawekwa kila sehemu hata vijijini ambapo watu wamekuwa wakicheza michezo hiyo wengine wakiwa na uraibu kabisa wa michezo hiyo, si ajabu kumkuta mtoto ameacha kwenda shule akiendelea kucheza.

USHAURI
Kwa kuwa serikali ilizuia matangazo kwa sababu ya kuwakinga watoto dhidi ya athari za michezo hiyo, serikali iweke tamko lingine michezo hiyo ipatikane eneo moja tu la starehe i.e bar, club au casino ambako kote huko kuna udhibiti wa umri

NB: Mzigo usiwe kwa mwenye mchezo pekee kwamba asiruhusu watoto wacheze au muda wa kucheza, bali iwe ni eneo ambalo mchezo upo

Signed

OEDIPUS

1622548460078.png
 
Ndio uchumi wa kati huo ulioletwa na awamu ya 5.

Au nasema uongo ndg zanguuuuuuuuuu?
 
Bonanza ni kielelezo cha jinsi gani maisha ya mTz wa wastani hayana matumaini.

Ona hapa;

Hilo bonanza pesa ndefu kubwa inayoweza kutoa haizidi 200K yaani hapo tunaassume wewe ni una bahati kuliko mtu yeyote duniani kwakua ili ufikishe pesa kubwa kabisa inayoweza kutoa utahitaji kuweka hela ndefu huku ukidouble na kudouble.

So hili ishu pesa inayokupa ni 20K elfu mbili n.k.

Ila mTz wa kawaida anajua kabisa hili dude halina pesa ndefu ila haachi kucheza. Kwanini? Kwasababu hana kitu kingine cha kumpa matumaini. Kuna watu wachache wanacheza bila kua na stress za kula hao ni wawili katika kumi, nane ndiyo kama huyo mama hapo.

Nimechezesha hili dude na personally hata kucheza sijui.
 
Usalama wa taifa upo hatarini! Hii ni biashara haramu, ila imehalalishwa kwa maslahi ya wachache
 
Bonanza ni kielelezo cha jinsi gani maisha ya mTz wa wastani hayana matumaini.

Ona hapa;

Hilo bonanza pesa ndefu kubwa inayoweza kutoa haizidi 200K yaani hapo tunaassume wewe ni una bahati kuliko mtu yeyote duniani kwakua ili ufikishe pesa kubwa kabisa inayoweza kutoa utahitaji kuweka hela ndefu huku ukidouble na kudouble.

So hili ishu pesa inayokupa ni 20K elfu mbili n.k.

Ila mTz wa kawaida anajua kabisa hili dude halina pesa ndefu ila haachi kucheza. Kwanini? Kwasababu hana kitu kingine cha kumpa matumaini. Kuna watu wachache wanacheza bila kua na stress za kula hao ni wawili katika kumi, nane ndiyo kama huyo mama hapo.

Nimechezesha hili dude na personally hata kucheza sijui.
Nilishawahi kuwa na biashara ya PS2 lakini sikuwahi kucheza na hadi sasa hivi sijui kuicheza. Kweli ndugu tuli-focus kwenye hela tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom