Michezo inapochanganywa na siasa jimboni nyamagana ndo maendeleo?

kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,137
809
Asubuhi hii ya leo katika kipindi cha michezo kirushwacho na RFA,nmesikia bonanza la maveterani na vijana limeandaliwa katika jimbo la Nyamagana na Theme yake ni kuhamasisha wananchi kupiga kura na kwa amani. Maelezo ya mwanzo yamekuwa mazuri sana na nikashawishika kama mwana Mwanza kushiriki japo sikai jimbo la Nyamagana. kilichonishangaza ni pale mwishoni viongozi wa michezo na waandaaji wa bonanza hili walipopewa nafasi ya kuongea ndo hapo wakanichanganya na kupelekea nilete hoja hii hapa tuijadili. Wamesema wananyamagna wampigie kura Stanslaus Mabula kwa vile amekuwa nao bega kwa bega kushughulika na michezo toka hata hajawa diwani mpaka amekuwa Meya amekuwa na wanamichezo na kuwashauri wananyamgana wasimpigie kura Wenje kwa vile hajawahi kushughulikia michezo na alikuwa na dhamana na jimbo la Nyamagana!
Sasa binafsi nikaanza kushangaa,hivi wananyamagana wanaenda kuchagua kiongozi wa michezo au mbunge? Na kama tutakuwa na kauli za namna hii na zinapewa coverage kubwa na vyombo vyetu vya habari,ina maana wanamichezo wa Nyamagana ni wana CCM pekee? Nikaanza kujiuliza hivi Meya wa jiji letu kafanya nini zaidi ya Meya cup? Sikutaka sana kufikiria ni nini kafanya Meya huyu mpaka michezo ianze kuingizwa kwenye siasa!? Je hapa hatuweki mgawanyiko katika kukuza michezo yetu? Ninavyoifikiria mimi,wanamichezo wa Nyamagana ni mchanganyiko wa vyama mbali mbali na itikadi tofauti tofauti, viongozi wa michezo wasitumike kutaka kuingiza siasa katika michezo naamini kabisa hawakuzi michezo bali watazorotesha michezo! Bonanza lisitumike kutafutia kura mgombea,watatukatisha tamaa tusiokuwa na itikadi ya vyama,wengine tulitamani kwenda kushiriki bonanza kama theme ilivyoainisha lakini viongozi wameaanza kuonyesha dalili ya kufanyanyia kampeni mgombea ubunge!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom