Michellle Obama na Ma first lady wa Bongo, ni giza na mwanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Michellle Obama na Ma first lady wa Bongo, ni giza na mwanga

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Mgoyangi, Jan 21, 2009.

 1. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #1
  Jan 21, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Historia ya Obama na Mkewe Michele inaonesha jinsi ambavyo, mwanamke mke wa Rais, kabla ya wadhifa huo alivyokuwa bega kwa bega na mumewe hadi Urais. Hakujali kukaa mama wa nyumbani katika siku za mwanzo za mihangaiko baada ya kuacha uanasheria katika kampuni binafsi na kwenda kuwa mtumishi wa umma.

  Kapigania vilivyo na hata hotuba zake zilikuwa za hamasa na zinazoonesha kuwa alikuwa mpiganaji na aliyeelewa mumewe anataka nini.

  lakini la salaale hapa Bongo, Mzee BWM alikuwa mseminari asiyejua hata kuuza karanga, Mama wa kichaga akafungua hadi wakafungua Biashara wakiwa Ikulu.

  Pia mnakumbuka ya Mzee Ruksa na wakeze, mara Uingereza wakati fulani wakasema tunataka kumjua first lady mmoja siyo kubadili, mnakumbuka ile skandali ya kubadili badili Hotel ili kumuokoa mzee mzima ili first lady asijue maana kalikuwepo kabinti.

  Mnafahamu mama muungwana na Taarabu na siku hizi ana kipindi cha Watoto TBC, Je hizi ndizo kazi za First Lady?

  Lakini pia msisahahu Kamandoo kule Zenj baada ya kustaafu Ukamandoo wa tende na halua, mama wa kichaga akampiga buti maana alijua ngawira zimekwisha.

  Labda yule mama yetu wa Butiama pale naona Break. lakini hawa wengine wanashindana na waume zao kuonekana kwenye luninga.
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Umesikika ndugu!
  after all said and done.... labda uchagize zaidi mada yako ili tupate mwelekeo wa kuchangia.Unataka kusema nini hasa zaidi ya kuponda cha kwenu na kusifia vya wenzio?
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kama ni kampeni hata Mama Salma Kikwete alidiriki kupanda kwenye majukwaa mbalimbali kumsaidia mumewe kwenye kucampaign.

  Kuhusu kuendesha kipindi cha watoto TBC1, huo ni uamuzi wake na pengine mapenzi yake kwa watoto hasa ukizingatia taaluma yake ya ualimu.
   
 4. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #4
  Jan 21, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tunatofautiana, lakini inawezekana wengine shughuli wanazozifanya mafirst lady waliopita na waliopo katika nchi yetu na nyingine za kiafrika wanayaona ya kawaida.

  Majuzi First lady wa Zimbabwe kazaba mpiga picha Hong Kong na akatoroka kurudi Harare kabla kizaa zaa hakijakommaa, Mama kibaki alizaba mtu kibao Kenya kwa kumchanganya jina na nyumba ndogo ya Mzee huku bado sakata la posho kwa akina mama wake za wakubwa Kenya likitokota.

  Sasa cha maana hapa ni kuwa, hawa ma first lady wetu wana mchango gani katika maendeleo yetu, zaidi ya kuendelea na shughuli zenye maslahi yao
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Labda nijadili hii sehemu ya mwisho ya wasilisho lako.Kwa kifupi nitachangia kama ifuatavyo:

  1.Umeponda ma first ladies wa TZ, sasa umehamia Kwa WaKenya na Zimbabwe.Sijui ndugu kama uliwahi kuwasikia mafirst ladies kama Nana Rawlings wa Ghana na 31st December Movement au mama Janet Kagame au Janet Museveni? Unajua makubwa ambayo wanafanya/walifanyia nchi zao au unaponda tu?Hebu jaribu kufanya research kidoogo ujue kwamba kuna wanawake wa shoka pia katika bara la Afrika wenye kufanya mambo mazuri nje ya mipaka ya TZ kama hawa wa Tz wahajaku impress.... ukishafanya hivyo tutajadili zaidi.


  2. Suala la maslahi, hili ni somo by itself.Sidhani hiki kipindi kifupi sana cha kuangalia uchaguzi na hatimaye Obama kuibuka mshindi wa Urais marekani kimekupa ushahidi tosha kwamba alichokifanya Michelle kwa mfano katika kumsaidia mumewe hakikuwa na maslahi binafsi.. nadhani what she did was also "selfish in a way" kwamba amsaidie her dear and beloved hubby kuingia madarakani.Hatujaona kingine alichofanya kwa ajili ya wananchi, labda tusubiri tuone.As for Lucy Kibaki na Mrs Mugabe... it is so obvious kuwa somehow they were "provoked " waka act irresponsibly.Hayo tuyaachie hapo kwa sasa.

  Asante ndugu.
  WoS
   
 6. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Arrgggg hao wamama wa kwanza wamefanya nini bana taifani mwetu?? Mama mkapa fisadi namba 1 nani asiejua.....mama maria nae hakuna laa maana alilofanya....Huyu Salma nae sifuri nae anaanza kuanzia NGO(Nothing Goin On) kwa mghongo wa ikulu.....
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Unajua Yoyo for a long time first lady kama instution ni kama ilikuwa haipo mpaka BW Mkapa alipoingia madarakani na ofisi ya first lady ikaanza kupata sura ya public.Kama unajua vizuri, kuna First Ladies conference huwa inafanyika nadhani kila mwaka na kuna maazimio huwa yanatolewa katika nyanja mbalimbali,Nakumbuka wakati wa kipindi cha Mzee mwinyi mama Mwinyi aliporudi kutoka huo mkutano, kazi ilikuwa namna ya kutekeleza maazimio ya mkutano maana haikuwepo framework inayoeleweka ya kutekelezea mambo muhimu yaliyoazimiwa. Nadhani pamoja na mambo mengine ndiyo maana Mama Mkapa akaanzisha taasisi ya EOTF ili angalau kuweza kufanya mambo in a coordinated fashion/manner.Ofisi hii ilikuwa hata na mratibu aliyetoka serikalini na trustees pia.Tusilaumu tu kuwa ma first ladies hawajafanya kitu.Mkumbuke mama Mkapa pamoja na mapungufu ya taasis yake, alifanya mambo mengi - kumbuka Telefood ilivyokusanya fedha na kusaidia wanawake hasa wa vijijini kwenye kilimo na mambo mengine ,tukumbuke mapango wa WIPE - Women in Poverty Eradication ulivyotoa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali na kuratibu ushiriki wa wanawake kutoka kila pembe ya Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya biashara.Hii ni mifano michache.Sasa hivi Mama Salma nae kaanzisha WAMA - agenda yake kuu ni elimu kwa mtoto wa kike na pia UKIMWI.Tumpe muda kabla hatujamponda.

  Tuendelee kujadili ...
   
 8. K

  Kishazi JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Ila wazee, madam wetu wa sasa inabidi apigwe sana msasa. F ya kutoa speech bado inampa shida. Utakuta anaongea na executives utafikiri anahutubia chekechea students. Sasa tunasemaaaaaaa tuleteeeeeeeeeee.........!!! yaani kwa kweli mimi binafsi sivutiwi hata kidogo na speech za madam. Wakuu wa itifaki ikulu, hebu lifanyieni kazi hili swala, la sivyo tutatia aibu hapa.

  Kuna siku wakuu wa itifaki ikulu nao walimmaliza madam kabisa, ilikuwa ni siku mama Laura Bush alipokuja na mumewe bongo, madam anatoa speech kwa kiswahili (ileee kasumba kuwa tuenzi kiswahili) halafu hakuna wa kutranslate, yaani mama wa watu ilibakia aombe maji manake alikuwa haelewi chochote, zaidi ya kusikia "Bush, Bush, Laura" Sasa sijui madam naye alikuwa ametengenezewa speech au amekariri kiasi cha kushindwa hata kuweka vineno vya ufafanuzi (vya ki-english) ili mwenzie aelewe au la...!!!

  Mapungufu kwa first ladies yasiwe generalized saana, kwani hata huko mamtoni wanachemsha sema tu, wenzetu watu wa itifaki wanakuwa makini sana kuzima mapungufu ya first ladies hata wa marais wenyewe. Kwetu Afrika, first lady akiwa zoba kidogo tu, yaani mpaka watoto watajua kuwa madam kachemsha.
   
Loading...