Michelle Obama awakataza watoto wake kujichanganya na kina Beyonce | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Michelle Obama awakataza watoto wake kujichanganya na kina Beyonce

Discussion in 'International Forum' started by Pdidy, Feb 1, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Michelle Obama awakataza watoto wake kujichanganya na kina Beyonce


  Malia na Sasha wakiwa na mama yao Michelle Sunday, February 01, 2009 7:00 AM
  Mke wa rais wa Marekani Michelle Obama amewakataza watoto wake kujichanganya na 'masupastaa' wa Marekani katika njia ya kuwafanya watoto wake waishi maisha ya kawaida.
  Mara ya mwisho watoto hao kujichanganya na masupastaa wa Marekani ilikuwa wakati wa sherehe za kuapishwa kwa baba yao kuwa rais wa kwanza mweusi wa Marekani mwezi uliopita.

  Malia mwenye umri wa miaka 10 na Sasha mwenye umri wa miaka 7 walijivinjari na nyota kadhaa wa muziki na sinema wakati wa sherehe hizo.

  Watoto hao sasa hawatakutana na "A-list" wa Marekani kama kina Beyonce ambaye walitumia muda mwingi naye wakati wa kampeni.

  Watu wa karibu wa familia hiyo waliliambia Us Weekly kwamba mke wa Obama alikuwa anataka kuwafanya watoto wake waishi maisha ya kawaida baada ya kuanza maisha mapya Washington.

  Baada ya kuhamia Washington kutoka Chicago Michelle Obama anafanya jitihada za kuwafanya watoto wake waendelee na masomo yao vizuri katika mazingira mapya.

  "Michelle anatumia muda mwingi kuzungumza na binti zake kuhusiana na shule yao mpya na marafiki zao wapya katika shule hiyo" alisema rafiki mwingine wa familia hiyo.

  Us Weekly lilisema kuwa Michelle hana mpango wa kukodisha mtu wa kuwaangalia binti zake kwa kuwa bibi yao Marian Robinson, 71, ameishahamia ikulu kusaidia kuwaangalia wajukuu zake.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nafikiri ni uamuzi mzuri, lakini hatakiwi kuwabana sana eti kuwalazimisha waishi maisha ya kawaida, that should come naturally kadiri wao (mr & mrs Obama) watakavyo ishi maisha yao mapya!
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri sana kufanya hivyo. Japo maisha yao hayawezi kuwa ya kawaida moja kwa moja ila wataishi maisha ambayo si ya makuu. Wajione kuwa ni watoto kama watoto wengine only tu kuwa baba yao amekuwa Rais wa Marekani na ni Rais wa Wamarekani wote na si wachache wao wa matawi ya juu. Hata mimi napenda sana watoto wangu kujichanganya na watoto wa clusters/strata mbalimbali, ila tu wawapende na kuwaheshimu wenye uwezo mdogo kimaisha. Na hii huanza tangu watoto wakiwa wadogo. Unaweza kuwafunza hata kuwapa wototo wasio na uwezo nguo zao which have grown out of and toys. Pia birthday zao jaribu kualika hata watoto walio jirani uswahilini (hapa msiniambie Dar hata kama ni kule Masaki au Msasani hakuna uswahili jirani). Kuna familia mojo ilitia kiwingi kijana wao asioe binti kwa kuwa binti eti hajatoka familia tajiri (harusi ilikuwa delayed for 3 years). Nilimpenda sana yule kijana aliweka msimamo wake na December 2008 alioa lile chaguo lake. Yote haya yanatokea Tz, katika familia zetu za Mbezi Beach!!!! Michelle is doing fine. Ila kwa kutizama tu harakaharaka, Michele ni mama na si msanii katika malezi, likewise to Pres Barack Obama. Na Marekani ili uwe Rais kuna masuala mengi wanatizama na family matters is crucial. Wenye ujuzi zaidi watujuze hapa.
   
 4. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Una maana gani na kuwabana sana na kwamba that should come naturally? Bila ya muelekezo mzuri natural ya Marekani ni celebrity kwa celebrit na nafikiri hilo ndio Mitchelle anajaribu kuliepuka.
   
 5. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kuhamia tu whitehouse, status ya vijana hawa umeshabadilika kabisa...na hii huwezi tena kuiondoa in their remaining life, washakuwa maarufu....so asiwabane, eti kwa mfano kama walikuwa wanaenda shule kwa pikipiki wakiwa Illinois, then na hapo white house watumie usafiri huo huo wakati kuna Helcopter(mfano) etc!
   
 6. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  bora awakataze tu, watoto miaka 7 na 10 watajichanganyaje na wadada walio kwenye twenty something?? hata kama kina Beyonce wangekuwa watu wa kawaida tu bado hawapaswi "kujichanganya" na watoto wadogo unless kuna umuhimu
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Unajua tatizo si kuwa celebrity au vipi, tatizo ni kufuata maadili mabaya ya baadhi yao. Kuwa mkubwa hakuna maana kuwa na haki na kudeserve kufanya mambo yasiyo na faida na nafikiri Mitchelle analenga katika hili na sio kuwabana wasifanye kile kizuri kinachofanywa na watoto wa vwakubwa. Hebu angalia hao kina Boyence na wengine matatizo wanayofanya katika jamii, wao wakifanya yanaishia kwao binafsi lakini kama tendo litafanywa na mtoto wa kiongozi basi litamuharimu zaidi mzee. Hivyo Mitchelle ana lemgo la kuona kuwa hadi hapo watakapokuwa wakubwa na kuwa res[ponsible kwa matendo yao,anawaongoza katika njia anayoihisi yeye itaweza kuwasaidia baadae na kwa sasa kuwawekea heshima wazee wao.
   
 8. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Age difference nayo ina matter, sasa leo hii Beyonce akahang out na watoto wa miaka 10 na 7 si mambo ya ajabu hayo.
   
Loading...