Michelangelo; Genius aliemchallenge vikali Leonardo Da Vinci kwenye kazi za Sanaa

Mkuu Una Kipawa Cha Uandishi Yaani Ni Analogous To Mange Kimambi ( No Offence), Huwezi Amini Sijaskip Neno Hata Moja Kwenye Article Yako. It Has A Grip! .

Pia, Inaelekea Wewe Ni Msomaji Wa Vitabu Sana. Sitaki Kuamini Kama Haujasoma "The Da Vinci Code".

Hao Watu Nimewafahamu Kwenye Hicho Kitabu Juu.

Ila Funny Enough Both Of Them Were Homosexuals.
wakikua wanaliwa wote hao na Pope..
 
Ingekuwa ulaya kidogo ingekuwa ngumu kutokana na gharama kubwa ila Ethiopia pale karibu sana yaani ukifika Kenya tu marsabit basi umefika Ethiopia.

Na hivi Karibuni marais wa pande mbili walikuwa wanataka kusign makubaliano ya kufanya iwe free visa country kwa Tanzania na Ethiopia.

Ethiopia wanaishi very ancient life ambayo sisi wengi hatukuiona na inafutika kwenye Dunia.. Its only in Ethiopia ambapo baadhi ya sehemu mgeni akifika anakaribishwa kwa kuoshwa miguu na binti mrembo wa familia.

Its ancient biblical stuffs.
Reallly????
 
unasema time traveller? Unajua time is stagnant? Unajua kama hakuna past, present wala future?

Ukitaka kuyajua haya kwa undani...kwanza ujue maana na mechanism ya déjà vu?

Ahahaha!! Ila tena nikimfuatilia zaidi mitkasi ya Da Vinci nashawishika kuamini time travellers exists.

Duh! Maisha yana siri kubwa sana haya.
mzee una hazina ya knowledge daah..
 
Mbona sanamu zao na michoro wamekosea!?the first world wasn't white hilo kosa la kwanza,la pili David hakua white but a dark skinned man,the same applies to Mary.
bro for ur information moja ya kaznkubwa ya wazungu ninkumis educate.. wanafanya maksud, hata masanam ya zaman wanayakata pua bt the truth ni hyo unayosema.. wanaforce ownerahip ya kila kitu from blackness.
 
Huyu hapa ndio Da Vinci.

Next nikipata time tutamjadili genius mmoja very interesting anaitwa Vincent Van Gogh yupo Kwenye top 5 genius artist of all time. Maisha yake yanasisimua sana. View attachment 802073
Spritual ,hiyo list nimeikubali, nilisoma mahali fulan history ya Pablo Picasso.

Hapo ni namba 5 lakin anaweza kuwa namba 1 in modern Word art

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio statue ya David yenyewe.View attachment 802083

Hii ni ile sanamu ya Davide original zipo 2 moja ni nakala inapatikana Accademy's Gallery(Galleria dell'Accademia) copy ipo nje pale panaitwa Piazza della Signoria.kwenye mji wa Firenze(florence).Hawa jamaa ukiacha kuchonga hayo masanamu walikuwa wapo vizuri kwa vitu vyote tunavyotumia leo hii vya kisasa,mtu kama Leonardo ukimsoma unaweza kusema hakuwa mtu wa kawaida huyu.


Inviato dal mio iPhone utilizzando Tapatalk
 
Good day
wakuu!

News is
Good

Baada ya kupona dhoruba la kunyimwa Uhuru wa kubanguana bongo....tuendelee kupeana vitu adimu na adhimu kwa afya ya ubongo..maandishi yenye kuprovoke thought and intellectual curiosity.. Leo nina mood ya kuzungumzia ishu za art kwenye kipindi cha Renaissance era ya manguli(Manyalali) wawili wa art Michelangelo na Da Vinci. Iko hivi;

Kama kuna kipindi ambacho sanaa ya Dunia ilibadilika kutoka kuwa ya primitive kwenda modern and classic art ilikuwa ni kwenye zama za "Renaissance" kuanzia karne ya 14 hadi 16C, hapa ndipo mafahari wawili washindani na wasiopendana walizaliwa lakini kama ilivyo asili ya washindani wawili mafundi wanapojikuta zama moja hakuna jingine zaidi ya kuoneshana uwezo kwenye field yao...rejea ishu ya 2pac na big notorious, Michael Jackson na Prince, Mondi na kiba e.t.c kwenye hii zama ya Renaissance walizawa mafahari wawili wa Sanaa ya uchoraji(painting, Sketch) uchongaji(Sculpture), mwanzoni mwa karne ya 14C..Leonardo Da Vinci na Michelangelo ambapo Da Vinci alimzidi bwana mdogo Michelangelo miaka 23. Wakiishi kwenye mji mmoja wa Florence pale Italy.

Hebu tujue kwanza Renaissance ni nini? Hiki kilikuwa ni kipindi cha mpito cha mabadiliko kuanzia karne ya 14 hadi ya 17C Dunia ikihama kutoka kwenye kufanya sanaa za kizamani kwenda kwenye Sanaa ya usasa modern and classical art kuanzia kwenye literature, architecture, poetry, engineering e.t.c kilichoanzia Italy na kusambaa ulaya na Dunia nzima. Kikichagizwa zaidi na manguli kadhaa akiwemo Leonardo Da Vinci, Michelangelo, Donatello, Raphael, Rambert e.t.c but walioitikisa Dunia na kuingiza technique and skills mpya kwenye sanaa tajwa hapo juu ni Da Vinci na Michelangelo.

Leonardo da Vinci yeye amekuwa maarufu zaidi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufanya vitu vingi na kuingia kwenye taaluma nyingi na zote kuzitendea haki kwa usahihi.. Kavumbua kifaru, kavumbua calculator, kagundua helicopter, hydrodynamic solar power, e.t.c huyu jamaa aliishi "ahead of his time" aliishi miaka 1000 mbele ya binadamu wengine aliweza kuiona future ikoje kabla ya wengine maana miaka 400 baada ya yeye kusema "kwamba Dunia lazma itakuwa muundo wa duara na sio Meza kama dini zilivyoaminisha kutokana na kani ya uvutano, Dr Isaac Newton akaja na theory iliyothibitisha kwa kusema kwamba “every weight tends to fall towards the centre by the shortest possible way”, and that the Earth must be spherical. Yeye tayari aliyasema hayo maneno ya Dr Isaac Newton miaka kama 400 iliyopita. Hakuishi maisha ya karne ya 14 aliishi maisha ya karne ya 19C. Alikuwa creative genius wa hali ya juu kuwahi kutokea kutokana na "versatility" yake ya kufit kwenye kila taaluma vizuri zaidi.

Sio rahisi kutafuta maneno sahihi yatakayo muelezea kwa usahihi huyu creative genius Leonardo Da Vinci na kumuelewa kwa uzuri wa kutosha maana ana fani lukuki alizovumbua na kuzitumikia kwenye zama zake akiwa kama architect, scientist, musician, engineer, painter, sculptor, inventor, mathematician e.t.c aliweza kuchora parachute la kwanza Duniani kabla halijatokea wala kutengenezwa na yeyote, helicopter ya kwanza Duniani, aeroplane ya kwanza Duniani, kifaru cha kijeshi, bunduki ya mashine gun, daraja la kunesa, boti ya kupiga pedeli, na gari la kutumia mafuta, kuchora michoro ya Sanaa za hadharani, alibuni vipodozi, alichonga vinyago, alikuwa mwanahisabati, alikuwa mtaalamu wa mimea, alikuwa mtaalamu wa sayansi ya mwili wa binadamu e.t.c

Kwenye Sanaa ya uchoraji ndiko alitisha zaidi kwa kubuni mbinu mpya za kimahesabu za kuchora picha ziitwazo "sfumato" ambapo alifanya calculation na kuchora vistari then alipitia humo humo kwenye vistari na kufanya mchoro uwe kama una roho hivi na uhai...iangalie kazi yake ya mchoro ya MonaLisa yule Dada anakuangalia kwenye kila angle utakayomuangalia hii haikuwahi kuwepo hapo awali Duniani mchoro kukutizama at every angle. Pia uwezo wa kuficha siri zake kwenye michoro yake kitaalamu wanaita "cryptographic " ulistaajabisha ulimwengu na kufanya Mapinduzi ya sanaa ya uchoraji yaanze rasmi karne ya 14. Monalisa ile picha ina mengi sana ya kuyazungumzia.

Hakuishia hapo akachora picha ya "Last supper" iliomwonesha yesu akiwa kwenye chakula cha mwisho na wanafunzi wake ili akafe msalabani...pale pembeni alikuwepo Magdalena ambae Da Vinci alikariri kwamba yesu alikuwa na mke aitwae Magdalena..ilizua mjadala mkubwa lakini nayo ilikuwa na siri lukuki alizoficha kwenye picha ambazo hakuzifafanua but style yake ya uchoraji ilibadilisha Dunia namna ya kupaint na Kusketch. Huyu jamaa tukianza kumzungumzia hatutamaliza Leo. Ana mengi ya kusisimua sana.

Da Vinci alikuwa muumini wa perfection yaani kufanya kazi kwa usahihi wa kiwango cha juu ndio maana kazi zake za Sanaa zaidi ya 100 alizitupa kwa kuamini hazina vigezo ingawaje walioziokota walishangazwa na maajabu ya ubora wa zile kazi zake za uchoraji. Na hata alipokuwa kitandani anataka kufa bado aliomba msamaha kwa Mungu na binadamu sababu kazi zake hazikufikia kiwango zilichotakiwa kufikia..namnukuu akisema "I have offended mankind and God because my works didn't have the quality it should have" wakati kiuhalisia kazi zake zilikuwa ahead of time yaani miaka 1000 mbele maana hata Leo hakuna picha inayoshangaza na kustaajabisha kiutalamu kama ya Mona Lisa. Kila Leo wataalamu wanavumbua vitu vipya ndani ya hiyo picha.

Yaani hii Dunia Kuna watu walitua duniani kwa kimya kimya na kuondoka kwa kishindo na bahati mbaya kizuri huwa hakidumu maishani wenzake kwa karne ya 14 waliishi zaidi ya miaka 100 yeye akafarikia akiwa na miaka 67 tu, akizaliwa 1452 na kufariki 1519.

Lakini tena miaka 23 baada ya Da Vinci kuzaliwa na kujijengea "brandy" kwenye taaluma mbalimbali Duniani na kuaminika na kuheshimika na viongozi wakubwa Duniani akazaliwa kijana mwingine machachari, hodari, mchapakazi, mahiri, mjeuri, mwenye kipaji cha juu zaidi kwenye uchoraji, uchongaji, engineer, poetry, architecture, na literature akiitwa Michelangelo di Lodovico Buonarroti Simoni lakini akifahamika zaidi kwa kifupi kama "Michelangelo" akikulia kwenye familia ya ndugu yake tu mchongaji wa mawe ya vinyago huyu bwana mdogo yeye hakuuona msingi wa sanaa kama ni uchoraji pekee yeye aliamini mhimili wa sanaa huko kwenye uchongaji na sio uchoraji kama alivyokuwa anaamini Leonardo Da Vinci. Hivyo akatofautiana nae kwenye epitome ya Renaissance art.

Na wengi wakahisi ni kama ni maneno ya mkosaji tu dogo hajui kuchora kama huyu legendary Da Vinci hivyo anataka kutafuta mwanya wa kuepuka uchoraji... Dogo Akawaprove wrong kwa kushinda kamisheni ya kuchora Vatican's Sistine chapel ceiling aliyopewa na Pope Julius || aliposumarize kitabu chote cha biblia cha Genesis(Mwanzo) kwa michoro murua sana pale juu kwenye ceiling yenye ukubwa wa kutisha kwa ustadi na uwezo wa hali ya juu akiwa mwenyewe bila yeyote mwingine kuweka mkono wake...akiwa kasimama kwenye ngazi na kukunja shingo akiangalia juu siku nzima huku akivumilia joto na ukali ya rangi za kuchorea. Pale kwenye madhabau akachora michoro inayoitwa "Last judgement" Hii kazi yake hadi Leo watalii wakiingia mule ndani ya kanisa huwa wakiangalia ile michoro ghafla mwili husisimka na vipele kama vile vya baridi vinaugubika mwili its totally "Goosebumps feelings" maana ni kama vile wanaona maisha ya another secret universe wanakwambia ile michoro yake ni pure definition ya artistic creative genius... Its the masterpiece work of art.

Kwa Michelangelo haikuwa kazi rahisi kuwafanya manyalali, matycoon yaani wale magenius wa art wa zama za Renaissance akina Raphael, Donatello, Da Vinci, Rambert e.t.c wakuvulie kofia kijana mdogo wa miaka 22 tu na kukutungia jina jipya la "|| Divino" ( The divine one) licha ya kwamba amewakuta kwenye game ilikuwa lazma afanye mara nne bora zaidi yao. Alifanya hivyo maana aliwakuta wachongaji kibao tu ila walikuwa hawajui kuonyesha ile anatomy of human body Kwenye jiwe wanalotaka kubadilisha na kuwa mtu...hapo ndipo kwa mara ya kwanza veins, bones, nails, eyebrow zilipopatikana kwenye statue za Michelangelo na kuishangaza Dunia... Wengi waliamini wenda sanamu zake zinaweza kuwa ni human flesh and spirit kutokana na uhalisia wa life-like human body.

Kazi ya sanaa sanamu ya "Pietà" ikiwa ni neno la kiitaliano lenye maana ya pity kwa kiingereza na (huruma) kwa kiswahili. ilichagiza hili jina la "divine one" kwa Michelangelo baada ya kuligeuza jiwe la baridi kubwa lisilo na uhai wala shepu kuwa mwili wa bikira Maria na Yesu ambapo Dunia ilishangaa kuona jiwe baridi likigeuzwa kuwa na life-like art na kijana mdogo wa miaka 22 tu..yaani ukiingalia unaiona sanamu ikiwa na muscle, vein and skin inayojivuta..huku ikishangaza kumuona yesu akiwa kwenye pozi la mtu aliekufa kabisa asieweza kuresist chochote..ukiutazama huu mwili wa yesu katika hii sanamu utaona totally a peacefulness death.

Ilikuwa ni ajabu sana kuona jiwe linachongwa na kutoa miili ya binadamu iliofichama ndani ya jiwe ukiwa unafanana kabisa na mwili wa binadamu kwa vitu vingi...it was pure magic.

Baada ya watu kushangazwa na ufanisi wa kwenye kazi ya Sanaa ya sanamu la Pietà alishinda kamisheni ya kuchonga sanamu ya mfalme Daudi iliyotakiwa kuwekwa kwenye mji wa Florence, Italy. Kazi Iliyowashinda magenius kibao akiwemo Leonardo Da Vinci mwenyewe na kukaa miaka lukuki ikiwa unfinished work of art hadi dogo alipozaliwa na kufikisha miaka 24 ndio akaitendea haki.. Dogo hakuangusha aliifanya ile kazi yeye mwenyewe kwa muda mrefu usiku na mchana na mwishowe akatengeneza masterpiece statue of art of all time...yaani Dunia iende na irudi hayupo atakaetengeneza sanamu yenye Ujumbe, ufundi na ushawishi mkubwa kwa Dunia ya sanaa ya uchongaji...hayupo! Wale wamakonde wachonge vinyago wawezavyo hadi mwisho wa Dunia hawawezi kubonyeza ile level za Michelangelo. Punde baada ya kuimaliza ile kazi ya kumchonga David akiwa kachafuka alitupa vitendea kazi vya kuchongea Akalia sana akawa anaiuliza ile sanamu kwa kitaliano “perchè non parli David” – why won’t you talk David?!

Yaani anaona kampa mwili David but kwanini David hajawa na roho ili wazungumze?

Pieta, David, moses, Sistine chapel ceiling, most genius artist walitamani waweze kutengeneza vitu vya heshima kama hivi katika maisha yao lakini ajabu Michelangelo yeye alivitengeneza vyote na vingine vingi zaidi akiwa na umri mdogo tu wa miaka 22.

Na hii inatukumbusha binadamu kujichunguza na kugundua kuna kitu gani cha thamani ndani yetu kama karama. Na kukitendea haki. Our talent and ability will never go in unnoticed way if we learn to tap into our genius level talents.

Ila licha ya yote hayo ya Michelangelo hawakuwahi kuwa urafiki na Da Vinci maana Da Vinci aliona kama dogo hana adabu, baada ya kupindua matokeo na heshima yake Duniani na kwenye jamii especially Kwenye Sanaa ya uchongaji. Na Da Vinci aliandika hii hata kwenye kitabu chake cha "Notebook" juu ya scenario moja akiwa pale Florence, Italy na watu mbalimbali wakimuuliza juu ya genius wa zamani aliefariki akiitwa Dante..sasa Da Vinci akamuona Michelangelo anapita pembeni akamuuita awasaidie juu ya wasifu na kazi za Dante dogo akajibu "Wewe si uwasaidie si unajifanya mtaalamu wa taaluma zote...ulieshindwa hata kuchonga sanamu ya farasi" then dogo akaondoka wala hakuchangia chochote. hii kauli ilimuudhi sana Leonardo Da Vinci na kuchochea zaidi uhasama wao.

Honestly, Dogo alikuwa anapenda kuwa mpweke na kuishi mwenyewe and introvert sana isipokuwa Da Vinci alikuwa social na mwenye link na connection kibao za marais na viongozi wakubwa Duniani na pia alikuwa na mkwanja zaidi ya Michelangelo ambae yeye alikuwa lone and sad asie na mkwanja sana wala marafiki wengi isipokuwa alikuwa na rafiki mmoja tu mkubwa Pope Julius 2.

Naam, huyo ndio Michelangelo licha ya mapungufu yake yote lakini aliefanikisha kutuonesha kwamba binadamu tuna udivinity flani ndani mwetu kwa kazi zake zitakazodumu milele maana ni mawe yale.

Naomba mnisaidie kumtag Da vinci wa humu JF. Anatakiwa kumfahamu mpinzani wake wa sanaa Tycoon Michelangelo.

Note; Picha zote ziko sehemu ya comments.

I enjoyed!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom