MICHEL LOTITO: Mfahamu jamaa aliyepata kula ndege ya abiria na kuimaliza yote

Mufti kuku The Infinity

JF-Expert Member
Sep 21, 2019
5,689
8,926
MICHAEL LOTITO : MTU PEKEE DUNIANI ALIYEKULA NDEGE YA ABIRIA (aeroplane)

Sijajua ni jina gani unaweza ukampa mtu huyu baada ya kusoma kisa chake, ila huko kwao Ufaransa wanamuita bwana mla vyote au mla kila kitu (Mr Eat All)

Najua sio mara ya kwanza kusikia mtu anayekula vitu vya ajabu hata hapa Tanzania tumeshawahi kuona kama sio kusikia kuhusu mtu anayekula misumari na kokoto ila sijawahi kusikia kama kuna mtu anaweza kula ndege kabisaa yooote, yaani ndege ya abiria yote ameitafuna akaimaliza.

Najua huwezi au ni ngumu kuamini kuhusu hili ila huo ndio ukweli jamaaa amekula ndege. Ndege ya abiria

Michel Lotito amezaliwa tar 15/6/1950 katika mji wa Grenoble nchini Ufaransa na alianza harakati zake hizo za kula vitu visivyo vya kawaida akiwa na miaka 16 tu.

Wataalamu walisema mtu huyo ana ugonjwa wa pica ambao ndio unamfanya kuwa na hamu ya kula vitu visivyo vya kawaida.

Lakini pia mfumo wake wa mmeng'enyo wa chakula una nguvu zisizo za kawaida kuna juice maalum inayosaidia kila binadamu katika mfumo wake wa chakula. Lakin juice yake ina nguvu saana kiasi ambacho akila vitu laini kama mayai ya kuchemsha na ndizi vinaweza kumfanya kuumwa.

Katika maisha yake alishawahi kula baiskeli, kula tv, kula vitoroli vya supermarket, na kubwa zaidi alishawahi kula ndege kabisaa aina ya Cessna 150. Bwana Fact

Alitumia miaka miwili kula ndege hiyo kuanzia 1978 hadi 1980

Katika kuanzia mwaka 1959 hadi 1997 inakadiriwa Michel Lotito anakadiriwa kula zaidi ya tani 9 za vyuma. Na namna anavyokula huvikata vipande kisha hunywa maji na mafuta ndio humeza vyuma hivyo.

Michel Lotito alifariki tar 25/6/2007, alifariki kwa ugonjwa wa kawaida tu.

Je, ungeombwa umpe jina mtu huyu ungempa jina gani?

s-338d2bedcad99be0cf9944a3928b0f69d00fd184.jpg

View attachment 1694005
View attachment 1694007
 
Ukitumia tu Biology ya form two topic ya Nutrition ni vigumu sana kuandika wala kukubali story ya aina hii.
Hata zile stories za mchele wa plastiki nilikuwa nazikataa katakata. Wote niliowataka waulete ule mchele waliukosa sanasana walinionesha clip za vichaneli uchwala vya YouTube.

Mwili wa binadamu hauwezi kufanya digestion ya takataka kama plastiki, vyuma, udongo au mbao. Hakuna digestive juice yoyote ya kufanya hivo.
 
Ukitumia tu Biology ya form two topic ya Nutrition ni vigumu sana kuandika wala kukubali story ya aina hii.
Hata zile stories za mchele wa plastiki nilikuwa nazikataa katakata. Wote niliowataka waulete ule mchele waliukosa sanasana walinionesha clip za vichaneli uchwala vya YouTube.

Mwili wa binadamu hauwezi kufanya digestion ya takataka kama plastiki, vyuma, udongo au mbao. Hakuna digestive juice yoyote ya kufanya hivo.
Udongo?? Nimeshuhudia watu kibao wakila udongo
 
Back
Top Bottom