Miche ya Papai Malkia F1 imegoma kuota

Negemu

Senior Member
Dec 26, 2017
135
126
Niko kwenye majaribio ya kilimo cha papai,aina ya malkia F1, nilinunua packet moja ya mbegu, ambayo ina mbegu 80, hatua ya kwanza niliziloweka kwenye chombo chenye maji safi kwa muda wa suku 5 na kila suku nilikuwa nabadilisha maji, siku ya 6 nikahamishia hizo mbegu kwenye kitambaa cheupe kisafi kilicholoana nikazifunga kwa pamoja,na kuziweka juu ya sahani kwenye meza kwa siku 5, huku nikiloanisha kwa maji kidogo kila suku kwa muda wa siku 5,siku ya sita nikafungua kikakuta baadhi ya mbegu zimepasuka, nikahamishia kwenye viriba nilivyokuwa nimejaza udongo uliochanganyika na mbolea iliyooza,nilichimba shimo dogo kwa kutoboa na kijiti na kuweka mbegu mojamoja kwenye kila kiriba, nimekuwa nikimwagilia kila siku tangu tarehe 31/5/2019 mpaka leo tarehe 24 sijaona dalili yeyote ya kuota, sijui nilikosea wapi
IMG_20190624_100432.jpeg
IMG_20190523_183157.jpeg
IMG_20190624_100311.jpeg
 
Ulizidisha kuloweka masaa 12 yanatosha sana.niliziloweka nikaziweka kwenye kopo lenye pamba iliyolowa kidogo nikafunika,ndani ya siku tano ilichipua,nikahamishia kwenye shimo.now nakula tu matunda.
 
Ulizidisha kuloweka masaa 12 yanatosha sana.niliziloweka nikaziweka kwenye kopo lenye pamba iliyolowa kidogo nikafunika,ndani ya siku tano ilichipua,nikahamishia kwenye shimo.now nakula tu matunda.
Mkuu unaiweka kwa juu ya pamba au chini, maana nasikia pia zinashambuliwa na fangasi
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom