Miche ya minanasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miche ya minanasi

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by mwalwisi, Apr 16, 2012.

 1. m

  mwalwisi Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakuu naomba kujua wapi ninaweza kupata mbegu ya minanasi, nina kajieneo mahali sina plan nako kwa mwaka huu hadi mwishoni mwa mwaka kesho. sasa sitaki kukaacha kakae bure ni wapi ninaweza kupata kama miche 40,000 au zaidi na kwa bei nafuu?

  Jone Mwalwisi

  Wapendwa
  Nashukuru kwa mchango wenu na maelekezo yaliyo bora, Mapendekezo mliyonipa nimeyatumia. Mbegu nyingi zilipatikana maeneo ya Bagamoyo na mimi nafanya shughuli za kilimo Mkuranga, hivyo basi ingawa bei ilionekana ipo chini kwa mbegu za Bagamoyo suala la usafiri liliadd gharama kubwa sana ukizingatia natumia usafiri wa kukodi. Hivyo nikaamua kutumia vyanzo vya mkuranga hukuhuku, nimepata mbegu kwa bei ya shilingi 100/- kwa mtoa mbegu kufikisha mwenyewe shambani. The only disadvantage ni kuwa sijapata mbegu nyingi za kutimiza lengo nililoweka, ila haijaniumiza sana kwani kwa vile ndio kwanza naanza acha nianze katika scale ndogo.

  Kwa mara nyingine tena asanteni sana
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ingekua 100 ningekwambia njoo uchukue lakini 40000??? Mingi sana.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwalwisi.

  Uko maeneo gani ?.Pwani,Dar na Tanga ni maeneo yanayostawi mananasi,yapo mananasi yanayostawi kanda ya ziwa Geita na eneo kubwa la kanda hiyo.

  Kama unaishi maeneo ya mkoa wa Pwani,Tanga na Dar nakushauri tembelea Kiwangwa ni eneo mashuhuri kwa kilimo cha nanasi na upatikanaji wa miche ya nanasi ni rahisi sana mche mmoja unauzwa kati ya tsh 30 - 50.Eka moja ya nanasi inaingia miche 10,000 - 12,000.Ni vyema ukaandaa eneo lako mapema kwasababu minanasi inaweza kupandwa hata kipindi cha kiangazi.
   
 4. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mpigie huyu 0714-298116 mche mmoja ni kati ya shs25 na 30
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Unapatikana sehemu gani ?.

   
 6. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Fukayose, BAGAMOYO
   
 7. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama upo maeneo ya Mkuranga ni PM. Zipo nyingi hapa Dundani na Mwanambaya
   
 8. m

  mwalwisi Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kaka nipo Dar nalimia Mkuranga katika vijiji vya mkiu na Mkuruwili, nahitaji mbegu kwa ajili ya mkuruwili
   
 9. m

  mwalwisi Member

  #9
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimeku PM mkuu
   
 10. m

  mwalwisi Member

  #10
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu mbona nimepiga namba hiyo jamaa kaniambia hausiki na mambo ya kilimo?
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu ebu check vizuri hizo number za simu uenda kuna number umekosea watu tuko kikazi zaidi.


   
 12. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Hivi nanasi tangu lipandwe hadi lizae linachukua muda gani?
   
 13. m

  mwalwisi Member

  #13
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Average time ni miezi 18
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Labda kama alitumia ya mtu. Mimi aliniuzia miche 280,000
   
 15. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  mkuu unaweza kutupa dondoo kidogo ktk hiyo miche ulifanikiwa kuvuna mananasi mangapi na kwa kiwango kipi (ubora)? if you dont mind na mapato kwa kukadiria
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Nimeipanda hii Januari. Ekari moja inatafuna miche 14,000 nami nimepanda ekari 20. Kuna suala la mbolea na upaliliaji pamoja na kushed jua wakati wa kiangazi. Hopefully ntavuna around July 2013. Nanasi moja kwa sasa ni TZS 300 likiwa shambani au unaweza kuuza eka moja 3,000,000
   
 17. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  mkuu safi sana, mimi huwa nayapanda kienyeji sehemu yoyote ambayo ina nafasi shambani huwa nayachanganya na mazao mengine kama mahindi, maharage, matikiti etc kwahiyo sielewi nalima hekari ngapi za mananasi na matikiti lakini mwishoni huwa naingiza fedha nzuri sana
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Mimi mkulima pia. Katika hiyo 14,000 bado kunabaki nafasi na nimepanda Kunde kwa ajili ya Nitrogenization ya udongo.
   
 19. b

  beko Senior Member

  #19
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  budget yako ni bei gani kwa mche? je shamba lako liko wapi? nina uwezo wa kukupatia mbegu hadi 100,000 ukitaka
   
 20. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  kumbe tupo wengi, hii njia inalipa sana mimi nimepanda mazao kama 8 hivi humo ndani kuna mbaazi, kunde(zikiwa mbichi ni fedha nzuri sana), karanga, ulezi na mtama kiasi. Somo la kilimo limenisaidia sana japo kipindi nalisoma nililiona kama kero kubwa kwangu
   
Loading...