Michano/Hiphop/Freestyle

Tangu mwaka umetimba sijatia verse, sijui ni mambo mengi au ubize kufuatilia cash.../

Au vijimambo vya mpira na propanganda za injinia hersi, kutuaminisha chama kashatia wino na anacho subiria ni press.../
 
Mvumbo navaa silaha begani, narudi kupiga za utosi/

Hip Hop sanaa ya kughani, ilipo tupo hatukosi/

Madogo wanashangaa huyu nani, waambie ni MKUU WA KIKOSI/

Haina kukataa kwenye Medani, wakuu tutakufosi/

Hata wote mhamie kwa Kaburu, eti Amapiano ndio test/

Bado Mvumbo nitabaki huru, kama nimelipia Guest/

Waliodhani nimejiuzulu, kama Spika ya Kaseti/

Bado mikono mvululu, kama fisadi kwenye bajeti/
 
Hahaa hahaaa munafurahisha, machungu yangu sasa yameisha/
Vijana mistari mmeivisha, nimemeza kama dawa imeniponesha/
Sasa nawaachia manyoya, naenda zangu kujinoa/
 
Maisha si majaribio, ila ni kukaza ile mbaya/

Ila usiuze material, pesa haiji kwa umalaya/

Wenzako wanakwenda mbio, upo skani unavuta kaya/

So wakipata mafanikio, usiwatafute ubaya/

Hizi nyakati sio, we zisake tu hata ulaya/

Wagumu haina ufagio, hata uvute waya/

Kila kona vilio, mpaka wasomi wanagwaya/

Wanaimba mapambio, kwa Chief Ha...ya/
 
Nani mc mkali tuchanane
Nimpige chali chakali akaandamane
Nipo fit hatari tisubishane
Napiga magoli niite sadio mane
 
Barua ya wazi kwenda ikulu

Soma kichwa cha habari hapo juu kisha husika, naitwa Scars kwa vina hapa tu umefika..../

Sina lengo la kuomba kuteuliwa uspika, ila na maswali ambayo nilipenda uyajibu nipate uhakika.../

Soko limeungua sijui kama hukupata taarifa, maana hujatoa pole kwa machinga au sababu ya wingi wa pirika?.../

Usinitafsiri vibaya najua mi ni mdogo kwa rika, nisamehe maneno yangu yasiwe sababu ya wewe kukasirika.../

Mifumuko ya bei kwa bidhaa, ni kilio kipya huko kwa mitaa.../

Tuondolee na tozo kama utaona inafaa, wakulima wakipewa ruzuku tutaishinda njaa.../
 
Siku hizi game imestop wanasikika Amapiano/
Tuzo ni za Afro Pop wako wapi watu wa michano/
Ya nini kuwalaumu soap soap Wasafi kwenye chano/
Ilihali misingi ya kina Dilop limeachwa agano/
Fid ni mzazi ila siku hizi kapoa kidogo/
Na inasikitisha Kikosi kazi kunyewa na mtoto mdogo/
Mikogo na dharau/ madogo wanajisahau/
Zogo na nahau/ kisogo ni kwa wadau/
Ukikosa ndumu basi pombe/
Na ukikosa Ngumu basi Konde/
Game imebaki kwa Lunya na Maarifa/
Wakali wamefungiwa stoo/
Media beef zinawalipa/
Na wanapotezea Sauti ya jogoo/
Jay anaonyesha uwezo/
Ila wadau wanamkodolea Baba Levo/
Turufu sio Uwezo/ umaarufu wa dezo/
Pungufu weka kietezo/ mikufu na milegezo/
Ndio maana nilivunja mkataba/
Mvumbo nikaacha hizi mishe/
Maana walisema natema ngumu kama shaba/
Kidogo nilainishe/
 
Hizi sio hasira za mbuzi kurudi walikompiga/
Hizi ni maujuzi nina mood kama Jigga/
Wako wapi wapuuzi Mkurdi nimeshika Trigger/
Kwenye Movie niite Steven seagal/
Kwenye mikwara ndipo ninapo pambana/
Nina kipara na bado nachana/
Nipo imara zaidi ya juzi na jana/
Nipe tano nipe gwara niwaharibie wana/
Wanapata fever kuona Mvumbo Am back/
Siwezi kusikiliza michano yao ya kiwaki/
Waliojiona Jesus leo wanahamaki/
Kuona mawe yameiva kuni zimebaki/
 
Nina uwezo wa ajabu na mistari isiyokoma/
Mvumbo sio kitabu hivyo huwezi kunisoma/
Wameni bless mababu na nyama tukachoma/
So nina kila sababu ya kuleta hii noma/
Homa ya jiji/ popoma njoo uhiji/
Ngoma mkwiji/ ona hawaigi/
Hii mitikasi si kwa ajili ya watoto/
Nikitimba wananipa nafasi kama Zimamoto/
 
Unaingia unyonge, Jf mambo yanayojiri/
Peke yako msaka tonge, wote matajiri/
Hakuna kibonge, wote body zimeshamiri/
Madem ni shombe, na hawawezi kiswahili/
Wenzako wana Diploma, wewe ndio haujasoma/
Wana mijengo Dar Dodoma, wewe huna hata boma/
Ukichangia maada, utaambiwa bange unachoma/
Na ukihitaji msaada, utaitwa Popoma/
Kuna thread za mandinga, hakuna za mtembea kwa miguu/
So hutaonekana mjinga, ukinyanyua mikono juu/
Na kubaki msomaji, uwaachie wenye majina/
Maana nyuzi zako hazina wachangiaji, wanapita kimya kimya/
Andika ya maana, bado utatoka kapa/
Wenzako wamejazana, thread ya waonyesha papa/
Pm ukizama unakutana, na viingereza vya uwongo/
Wakati wenzako wanaelewana, na kupeana nyama ya udongo/
Wenzako wanatesa, ukimgusa Mama watasema bangi/
Utaambiwa tafuta pesa, au Sukuma Gang/
Ila usiache mbachao, wala kuwa mbogo/
Maana humu hata mwanao, atakuita bwana mdogo/

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Unaingia unyonge, Jf mambo yanayojiri/
Peke yako msaka tonge, wote matajiri/
Hakuna kibonge, wote body zimeshamiri/
Madem ni shombe, na hawawezi kiswahili/
Wenzako wana Diploma, wewe ndio haujasoma/
Wana mijengo Dar Dodoma, wewe huna hata boma/
Ukichangia maada, utaambiwa bange unachoma/
Na ukihitaji msaada, utaitwa Popoma/
Kuna thread za mandinga, hakuna za mtembea kwa miguu/
So hutaonekana mjinga, ukinyanyua mikono juu/
Na kubaki msomaji, uwaachie wenye majina/
Maana nyuzi zako hazina wachangiaji, wanapita kimya kimya/
Andika ya maana, bado utatoka kapa/
Wenzako wamejazana, thread ya waonyesha papa/
Pm ukizama unakutana, na viingereza vya uwongo/
Wakati wenzako wanaelewana, na kupeana nyama ya udongo/
Wenzako wanatesa, ukimgusa Mama watasema bangi/
Utaambiwa tafuta pesa, au Sukuma Gang/
Ila usiache mbachao, wala kuwa mbogo/
Maana humu hata mwanao, atakuita bwana mdogo/

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Kitambo sana hiz mambo ,kama vip goma liendelee
 
Jf wengine hawatoi namba, kama mawakala wa Nida/
Sio kama ni ushamba, USALAMA ndio shida/
Wengi Mod wanawabamba, hawaijui tafsida/
Ukiwafunga kamba, ni matusi kila mida/
Madem wanajielewa, na kichwani wapo smart/
Mvumbo nishapewa, ila sikuonyesha mapenzi ya dhati/
Jf elimu unaletewa, ambayo Shule huipati/
Jf ni ya kuombewa, isifike tamati/
Wengi imewatangaza, noti wakazichanga/
Kwa wasio kwenye mwangaza, hii ni mwanga/
Wengine wanakataza, hakuna Mungu kina Kiranga/
Wengine wana majina ya kushangaza, kama wamepewa kwa Mganga/
 
Leo napush mistari/ mkushi naonyesha uhodari/
Wazushi mi ni bahari/ hamgusi hata kwa morali/
Mvumbo ni m'bakiaji, kama alama za barabarani/
Dogo usidharau Bajaji, Ndege haikufikishi nyumbani/
Natawala dimba, msituni niite Tarzan/
Hawa Tembo Simba, wanajua mimi nani/
Watoto wadogo/ wanatoa boko tukiwapa kisogo/
Wanataka soko na hawana logo/ sa' natembeza mboko mdogo mdogo/
Mvumbo sauti ya Gheto/ dada usilete tumbo mimi nina beto/
Wananiogopa kama Meko/ Ukonga na Keko/
Mpaka mitaa ya Soweto/ haina mbeleko/
Demu wako anae sitasita, eti mpaka kesho/
Kwangu anakatika, kama umeme wa Tanesco/
 
Leo napush mistari/ mkushi naonyesha uhodari/
Wazushi mi ni bahari/ hamgusi hata kwa morali/
Mvumbo ni m'bakiaji, kama alama za barabarani/
Dogo usidharau Bajaji, Ndege haikufikishi nyumbani/
Natawala dimba, msituni niite Tarzan/
Hawa Tembo Simba, wanajua mimi nani/
Watoto wadogo/ wanatoa boko tukiwapa kisogo/
Wanataka soko na hawana logo/ sa' natembeza mboko mdogo mdogo/
Mvumbo sauti ya Gheto/ dada usilete tumbo mimi nina beto/
Wananiogopa kama Meko/ Ukonga na Keko/
Mpaka mitaa ya Soweto/ haina mbeleko/
Demu wako anae sitasita, eti mpaka kesho/
Kwangu anakatika, kama umeme wa Tanesco/
Daaah
 
Back
Top Bottom