Michango ya Ujenzi wa Uwanja wa Simba umefikia wapi?

Usajili wa michango ya yanga Kuchat kwenye group la WhatsApp umefikia wapi ili twende sawa.
 
Unasema?

Screenshot_20211029-110122 (1).png
 
Maamuzi ya Simba SC kutaka Kujenga Uwanja wake yalikuwa ni ya Kimihemko ( Kihasira ) zaidi na siyo ya Kiuhalisia.

Saikolojia ya Mashabiki wengi wa Tanzania ( hasa wa Simba na Yanga ) ni Kushangilia na Kubishana ila likija Suala la Michango hakuna utakachokipata zaidi ya Ahadi tu.

Mwisho kilichonishangaza zaidi ni Kitendo cha Mwekezaji Mo Dewji kusema katika Bajeti ya Ujenzi wa Uwanja wa Simba SC ya Tsh Bilioni 30 yeye atachangia Tsh Bilioni 2 tu na hizo Tsh Bilioni 28 zilizobaki akina GENTAMYCINE ambao hata Hela ya Kula tu Kwetu ni Changamoto ( Tatizo ) ndiyo tuchangie.

Kuna Usanii mwingi sana tu Simba SC.
Watu tulitoa hapa michango tena kisomi zaidi lkn tukaonekana tunataka kukwamisha juhudi.
Nimekupa Like kwa mara ya kwanza.
 
Kujenga uwanja sio jambo la kumaliza leo leo.

Hilo ni wazo na ujenzi ni swala la mchakato.

Kama sio leo au kesho mpango tayari upo katika Mpangokazi wa Simba Sports Club.
Hilo wazo tu ni moja ya hatua nzuri kuelekea kulifanyia kazi.

Kwanza uwanja tayari upo na ulianza kidokidogo hivyohivyo kwa wazo la kuwa na Uwanja japo wa mazoezi.

Mnaotaka Michango ikamilike leo na uwanja ujengwe kesho hayo ndiyo mawazo ya Mihemuko.
 
Kujenga uwanja ni mpango mzuri, lakini hili lilifanyika kimihemko ndiyo maana mpaka sasa hakuna kinachoendelea
 
Uwanja tutaanza kujenga kuanzia mwezi wa 5, pesa zote bil 30 zimepantikana na zaidi, tuko kwenye mchakato wa kumpata mkandarasi wa ujenzi!
 
Back
Top Bottom