Michango ya shughuli za maendeleo sasa ni kero. Watumishi tunakamuliwa

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,219
Jamani sijui kama huko mikoani mnaliona hili yaani sasa hivi Wakuu wa Mikoa (RC) wanachangisha taasisi na watumishi tena kibabe.

Mara mchango wa nyumba za walimu haijaisha mchango wa mashimo ya choo hajatulia team za mpira michango imetisha jamani.

Hasa taasisi binafsi jamani zinakoma yaani wanakamua kisa usipotoa huna ushirikiano nao, sasa kwanini wakamue watu na wasikamue taasisi? Ni lazima wakumbuke sisi ni watumishi kama wao hatuna cha ziada.

Mbaya asiyechangia anaonekana msaliti sasa jamani mishahara yetu ndio kama hiyo alafu pesa hizi hazina audit kweli ni nani atatusemea kwa viongozi wa kitaifa tumechoka mpaka furaha ya kazi hakuna.

Mh Rais na Tume ya Maadili tunaomba mlimulike hili na hasa wengi wanatumia style ya Rais kuchangisha akiwa ziarani sidhani kama ipo sawa yeye anafungu sisi tunatoa wapi mbona hamna huruma? Au hamuoni hali ya uchumi ilivyo sasa? Au mpaka watu walie?

Kama kuna mkoa huko, Mkuu wa Mkoa anachangisha mpaka sasa imekuwa ni tabu.
 
Taasisi zisizo za Umma na nyie mmeanza kulialia
Si mnasemaga tulioajiriwa na serikali tunakomeshwa na hatuna ujanja??
Nyie je?
 
Back
Top Bottom