Michango ya elimu Kagera: Ukweli au siasa,kuelekea 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Michango ya elimu Kagera: Ukweli au siasa,kuelekea 2010

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Sophist, Oct 11, 2009.

 1. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,083
  Likes Received: 1,729
  Trophy Points: 280
  Utafiti kutathmini thamani ya michango ya fedha (value for money) katika sekta ya Elimu: Michango ya kuendeleza Elimu Mkoa wa Kagera  Utangulizi:

  Utafiti huu unalenga kutathmini thamani ya michango ya fedha katika sekta ya Elimu. Una maana ya kubainisha kwamba kiasi cha fedha zilizochangwa kwa madhumuni ya kuendeleza sekta ya elimu kama zimetumika kama ilivyokusudiwa. Dhana ya kutathmini thamani ya michango ya fedha (value for money) kwa muktadha wa utafiti huu, inaainishwa kwamba “matumizi ya fedha za michango yawe na uwiano na ubora na makusudio ya bidhaa au huduma iliyokusudiwa”. Utafiti huu wa kutathmini michango unaweza kulinganishwa na kile kinachoitwa Public Expenditure Tracking (PETS) ambapo mafungu ya bajeti ya serikali yanafuatiliwa kuona kama yametumika kule kulikokusudiwa na kwa kuzingatia ubora wa huduma na miundombinu ambapo michango inaelekezwa.

  Tangu serikali ya Awamu ya Nne kuamua kujenga shule za sekondari za Kata, kumetokea wimbi la watu wa maeneo yao (kiwilaya au kimkoa) kutayarisha hafla na mikutano ya wahisani kuchangia ujenzi wa shule za sekondari za kata. Kitendo hicho kimedhihirisha kwamba wananchi wana shauku ya kuchangia maendeleo. Elimu inapewa kipaumbele katika fikra na mipango yao. Katika harambee zilizoendeshwa mjini Dar es salaam mabillioni ya fedha yamechangwa. Michango kwa Mkoa wa Kagera ilifikia kiasi cha shs.1.2 billioni mwaka 2007, ambacho ni kiasi kikubwa kilichowahi kuchangishwa nchini Tanzania.

  Nini tunataka kuchambua:

  Tunachotaka kuchambua na kutathmini ni kwa namna gani fedha zilizochangwa zimetumika katika kupanua na kuboresha elimu ya sekondari mkoani Kagera.

  Namna ya kukusanya habari:

  Habari zitakusanywa kwa:
  (i)kuwahoji watayarishaji wa Kagera Day, ambapo michango ilikusanywa (Dar es salaam, Bukoba)
  (ii)Kuchambua nyaraka ili kujua kiasi gani kilipatikana, kuahidiwa na kiasi gani cha mapato halisi kimewasilishwa.
  (iii)Ahadi za aina nyingine zisizo fedha
  (iv)Kutembelea shule zilizofaidika na michango na kujua vigezo gani vilitumika kuchagua shule hizo.
  (v)Kufikiwa malengo na ubora wa shule zilizojengwa
  (vi)Kuchambua muundo wa uongozi
  (vii)Kuchambua ushirikishwaji wa wadau katika menejimenti ya michango na utungaji wa vigezo vya kuteua miradi ya shule zipi inufaike na michango (ya fedha).
  (viii)Kuona kama mpango wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari za kata ni mpango endelevu au la.

  Watakaohojiwa

  (1)Watayarishaji wa Kagera Day (Kamati)
  (2)Mkuu wa Mkoa, Kagera
  (3)Wachangiaji na wadau wa Elimu Kagera
  (4)Walimu Wakuu wa Shule zilizonufaika na fedha zilizochangishwa
  (5)Maafsa elimu wa wilaya Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini na Muleba

  Maswali yatakayoulizwa yatakuwa kama ifuatavyo :-

  Watayarishaji: Wajumbe wa kamati ya Kagera Day (Kashasha, Mwijage)
  (i)Ilikuwaje mkafikiria kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu Kagera na siyo sekta nyingine.
  (ii)Mliundaje kamati yenu?
  (iii)Mliwasilianaje na uongozi wa mkoani Kagera kuhusiana na suala zima la kuendesha mchango?
  (iv)Kwa nini mlifanyia hafla ya kuchangisha Dar es salaam na siyo Bukoba?
  (v)Mwitikio wa wachangiaji ulikuwaje?
  (vi)Kiasi gani kilichangwa?
  (vii)Nani alikabidhiwa michango?
  (viii)Kuna udhibiti gani wa michango iliyokusanywa?
  (ix)Je, ukusanyaji michango ni tukio la mara moja au endelevu?

  Mkuu wa Mkoa

  (i)Wazo la kuchangia elimu mkoa wa Kagera liliibukaje?
  (ii)Kwa ini hafla ya michango ilifanyika Dar es salaam badala ya Bukoba
  (iii)Kiasi gani kilichangwa? Usalama wa michango ukoje?
  (iv)Kwa vipi wadau wanahusishwa katika kudhibiti michango na kuweka vigezo vya kugawa fedha zilizochangwa?
  (v)Kuna kamati ya kukusaidia juu ya kuweka vigezo vya kuteua miradi ya elimu ya kunufaika na michango Mkoani Kagera?
  (vi)Je, uchangiaji wa Elimu ni tukio la mara moja au tukio endelevu?

  Wachangiaji na wadau wa Elimu Kagera?

  (i)Kilichokusukuma kuchangia elimu Mkoa wa Kagera ni nini?
  (ii)Unaona au ungependa tukio la kuchangia elimu Mkoa wa Kagera liwe tukio la muda au endelevu?
  (iii)Ungependa wadau washirikishwe vipi kuhusiana na udhibiti, usalama na matumizi ya michango?

  Shule 10 zilizopewa misaada

  Walimu wakuu wa shule za sekondari zilizonufaika na fedha zilizochangishwa:

  (i)Nini matatizo katika shule unayosimamia?
  (ii)Shule yako iliishapata misaada kutokana na michango ya fedha za kupanua elimu ya sekondari Kagera?
  (iii)Mlitaarifiwa juu ya vianzio vya misaada?
  (iv)Mrishirikije kuhusiana na wapi shuleni paelekezwe misaada?
  (v)Je, unaridhika na matumizi ya misaada pale ilipoelekezwa shuleni kwako?
  (vi)Ungependa misaada zaidi itolewe na ielekezwe wapi?

  Maafsa wa Elimu Wilaya – Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini na Muleba

  (i)Ulihusikaje katika kuandaa hafla za kuchangia upanuzi wa sekta ya elimu ya sekondai wilayani na mkoani kwako?
  (ii)Je, wewe ni mwanakamati wa Kamati inayohusiana na uchangiaji wa upanuzi wa elimu wilayani; mkoani kwako?
  (iii)Ulihusika kuweka vigezo vya wapi pa kuelekeza misaada katika mashule yaliyo wilayani kwako?

  Nyaraka zitakazotumiwa :

  (i)Wanakamati Dar es salaam
  (ii)Waliohudhuria hafla ya kuchangisha Dar es salaam
  (iii)Magazeti yaliyoripoti hafla ilivyokuwa
  (iv)Nyaraka za benki
  (v)Nyaraka za shuleni zitakazohakikiwa

  Magazeti ambayo yataandika makala za uchambuzi: (kwa kiingereza na kiswahili)

  (1)Taifa Tanzania (Kiswahili)
  (2)Rai (Kiswahili)
  (3)Daily News (kiingereza)
  (4)The Citizen (Kiingereza)  Prince M. Bagenda
  Simu ya mkononi: 0789 – 050051
  E-mail: pmbagenda@yahoo.co.uk
   
Loading...