Elections 2010 Michango ya CHADEMA Updates: Wiki ya Kwanza ya Harambee: 11,569,000...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Wito wa kuchangia mabadiliko umeanza vizuri kwani wiki ya kwanza ile iliyoishia tarehe 27 Septemba kiasi kilichochangwa na Watanzania kwa njia mbalimbali ni shilingi 11,569,000! Kwa kiwango kidogo kidogo ambacho kilikuwa kimependekezwa ni wazi kuwa watu wengi zaidi wamechangia. Nilitoa wito kuwa Chadema watupe updates za kila wiki ili tujue tunachangia kwa kiasi gani. Tuko kwenye challenge ya kufikia Shilingi milioni 100! Mchanganuo kidogo:

NMB/CRDB
11,000,000
MPESA 758 223344
402,000
MPESA 764 776673
152,000
ZAP 0789 555333
15,000


Natumaini wiki hii tutaendelea tena kufanya hivyo na once again natoa changamoto march my amount or beat it. Wiki hii nitatoa Shilingi 100,000 kuchangia mabadiliko tunayoyataka.

Unaniuliza kwanini? Kwa sababu naitikia wito huu:



WEWE JE?
 
Last edited by a moderator:
Asante Mzee Mwanakijiji. Nitakuunga mkono nitoe vile vile laki moja.

Ila hukuandika sahihi. Ukisema milioni 11,569,000 maana yake ni trilioni 11 na kitu. Aidha uondoe neno milioni au uandike milioni 11.569
 
Asante mzee. Naona zile za sms hazipo hapo. halaf kama CHADEMA wanaweza kuwajumuisha tigo kwenye hii njia ya sma, kwani siku hizi vijana wengi tuko huko...
 
Naelekea bank kuweka laki 2, Ingawa Tayari nimeshachangia huko nyuma lakini kwa mara nyingine tena wacha nijibane kuchengia mabadiliko

Kwa hali ilivyo Slaa ameshaingia ikulu, Tunahitaji michango ya kumalizia safari yake

PEEEEPOOOOOOZZZZZ.....
 
Thanks mwanak unajua hii njia ya Mpesa nilikuwa sijaigundua angalia salio kwa namba ya VODA nshachanga kwa kishindo.
Tena namba nimeisave ngoja nikipata Mkwanja fulani ivi lazima nichangie kama Laki ili kuweza nunua mafuta ya helcopter.
Mwambie Dr awe anatoa izo namba kwenye mikutano yake maana pale iringa walipitisha vikapu ndo tena mwishoni
 
mwanakijiji Wiki ni Kubwa tunaomba Tathmini ya Mchango itoke baada ya Siku Tatu
 
Tena nimeisave iyo number for sharing with my colleaques.
Tanzania itakombolewa na watanzania wenyewe
 
Shukrani Mwanakijiji kwa mchango mzuri.

Mchango wangu upo njiani unakuja leo huko wa laki moja tu.
 
Twendeni kufanya kufanya kweli... jamani hata kwenye mechi zetu enzi zile si wote tulikuwa wachezaji lakini baadhi walinunua machunga na machenza kuwapa moyo wachezaji.. be part of something bigger than yourself.. be part of history..!
 
Asante mzee. Naona zile za sms hazipo hapo. halaf kama CHADEMA wanaweza kuwajumuisha tigo kwenye hii njia ya sma, kwani siku hizi vijana wengi tuko huko...

Mimi nimejaribu mara nyingi kutuma SMS Tigo na Zain, lkn mara nyingi zina-fail! Sijui ni hujuma au matatizo ya network tu!
 
Mimi nawashukuru sana wadau kwa kuchangia mabadiliko,kwa kweli inatia moyo sana.Kitu ambacho nataka kuwaambia wadau ni kwamba mimi ni mtumishi wa umma moja kati ya Halmashauri Mkoani Mbeya,kuna wakati fulani CCM walipitisha fomu ya kuchangia kampeni,na michango hiyo haikuwa hiari,mkuu wa kazi akawa anawalazimisha watu kutoa fedha hizo.

Kwa kutumia njia ileile,mimi nimechukua fomu ya kuichangia CHADEMA kwa ajili ya kukodi vyombo vya mziki kwani DR.SLAA atakuwa wilayani kwetu kesho,watu walewale walioichangia CCM kwa lazima ambao wanataka mabadiliko wanaogopa kuichangia CHADEMA kwa madai kuwa vibarua vyao vitakuwa mashakani pindi itakapogundulika kuichangia Chadema.Kifupi CCM inabebwa na watendaji wa serikali.

Naomba Watanzania wenzangu mnaotaka mabadiliko,muliochoshwa na sarakasi za CCM tuendelee kuichangia CHADEMA,kwani harakati bila fedha ni kazi bure,kuwa sehemu ya mabadiliko.Asanteni.
 
Mimi nimejaribu mara nyingi kutuma SMS Tigo na Zain, lkn mara nyingi zina-fail! Sijui ni hujuma au matatizo ya network tu!
Peleka bank watazipokea mkuu. natumaini umesoma namba za akaunti hapo mwanzo wa thread hii
 






Tukiwa tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Tanzania ambao utafanyika October 31, 2010, Watanzania wazalendo wanachama na wapenzi wa Chadema mnaombwa kuchangia kwa dhati harakati za Chadema ili tuweze kuwafikia Wananchi wengi zaidi katika kila kona ya Tanzania tukitafuta ridhaa yenu ya kuweza kujenga nchi yetu; nchi yenye usawa, uzalendo, maadili na uwajibikaji katika miaka mitano ijayo.

Video Link:
http://www.youtube.com/watch?v=TvLRsAsgyWc

CHANGIA CHADEMA KUPITIA BANK:
CRDB BANK
CHADEMA - M4C
Account Number: 0J1080100600

National Microfinance Bank [NMB]
CHADEMA
Account Number: 2266600140

Unaweza kuweka pesa kupitia tawi lolote la Benki hizi Tanzania.


CHANGIA CHADEMA KUPITIA SMS (MESEJI):
Tuma neno:

"CHADEMA" kwenda namba 15710
"NAJIUNGA" kwenda namba 15710
"SLAA" kwenda namba 15710

Unaweza kutuma meseji mara nyingi kadri unavyoweza na kila ujumbe utagharimu TZS 350/= tu.
HII NI KWA MITANDAO YA ZAIN, TIGO NA VODACOM TU.


CHANGIA KUPITIA M-PESA:
Kwa watakaotaka kuchangia kwa M-Pesa wanaweza kutumia namba zifuatazo:

0758 223 344
0764 776 673


CHANGIA KUPITIA ZAP:
Kwa watakaotaka kuchangia kwa ZAP wanaweza kutumia namba hii:

0789 555 333

"Ndugu Zangu Watanzania, tunawaomba kwa dhati kabisa tushikamane, tushirikiane bila kujali itikadi zetu kuchangia harakati hizi, tunawashukuru sana. - Dr. Wilbroad Peter Slaa"

CHAGUA MABADILIKO YA KWELI. CHAGUA CHADEMA.

Kwa habari zaidi tembelea www.marafikislaa.blogspot.com
 
ebaaaaaaaaaa!!!!! kumekucha mkuu nitatoa laki kupitia nmb mobile, acha nilale njaa, nipate kuokolewa baada ya mkombozi wa kwanza jk nyerere kuchukuliwa kwenye mbele za haki
 
Kapu la mjanja, mjinga hatii mkono! wachaga sasa mna tapeliana wenyewe kwa wenyewe. Hivi hamja jifunza ya mwaka 1995? Kama namuona Mwenyekiti Mbowe meno yote nje mwaka huu anakula kwa ulaaaiiiniiiii!

Wale akina mwenzangu mie chezeni ngoma msio ijua, wakati mnastuka too late! wenye ngoma yao akina Augustino Moshi wanacheka tu!
 
Kapu la mjanja, mjinga hatii mkono! wachaga sasa mna tapeliana wenyewe kwa wenyewe. Hivi hamja jifunza ya mwaka 1995? Kama namuona Mwenyekiti Mbowe meno yote nje mwaka huu anakula kwa ulaaaiiiniiiii!

Wale akina mwenzangu mie chezeni ngoma msio ijua, wakati mnastuka too late! wenye ngoma yao akina Augustino Moshi wanacheka tu!

Pilipili usoila........................
 
Mimi nilituma kweneye sms....mbona sijaona mchanganuo km ni kiasi gani kilipatikana kupitia huko...........nisaidie tafadhari!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom