Michanganyiko ya vyakula inayosaidia kupunguza uzito haraka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
1. Mchanganyiko wa maji, matango, ndimu au malimao (unaweza kutumia chochote kati ya hivyo), mdalasini, tangawizi, majani ya mint na ukipenda asali.

Kazi: Unasaidia kupunguza uzito sana. Ni njia nzuri ya kupunguza sumu mwilini (kufanya detox). TUMIA MUDA WOWOTE. Uaandaaji: - Maji lita 2 - Tango 1 kubwa. Likate vipande vya mviringo bila kumenya. - Tangawizi kipate kimoja cha kati kilichokatwa. - Mdalasini kijiti 1 - Majani ya mint vitawi 12 - Asali kijiko 1 kidogo ukipenda Changanya. Acha usiku mzima. Anza kunywa kuanzia asubuhi. Maji yakiisha tafuna vilivyomo na rudia tena kesho yake. Ukiendelea hivi matokeo ndani ya wiki moja utaanza kuona.

2. Mchanganyiko wa green tea na tangawizi Kwanini:
Mchanganyiko huu una kemikali za catechin na theanine. Hizi zinasaidia kuchangamsha mwili ili uchome mafuta mengi zaidi muda wote. TUMIA MUDA WOWOTE.

Uandaaji: Nunua green tea kutoka supermarket ya karibu. Pika kama chai ya kawaida ya rangi na ongeza kipande kiasi cha tangawizi iliyosagwa wakati chai inaaza kuchemka. Kunywa kadri utakavyo. Ni vema usitumie sukari.

3. Maji ya mdalasini na asali Kwanini:

Mdalasini unazuia kuongezeka kwa sukari kupita kiasi ndani ya mwili. Pia unazuia mafuta kulundikana chini ya ngozi na kusababisha uzito kuongezeka. Hii ni njia nzuri ya kupungua zaidi kama unafanya diet au mazoezi. MARA MOJA KWA SIKU INATOSHA.

Uandaaji: - Mdalasini uliopindwa nusu kijiko cha chai - Asali kijiko 1 cha chai - Maji kikombe 1 Chemsha maji. Weka mdalasini katika kikombe. Mwagia maji kwenye kikombe na ngojea yapoepoe. Ongeza asali. Enjoy.

4. Apple Cider Vinegar Kwanini:

Imeonekana kusaidia watu katika kupunguza mafuta mwilini. Matumizi: Vijiko viwili vya apple cider kwenye glasi moja ya maji. Kunywa kila asubuhi. MUDA WOWOTE MWINGINE HAMNA NENO.

5. Supu ya maharage aina 3 Kwanini:
Maharage yana protini, nyuzinyuzi na hayana mafuta. Ni chakula kinachoshibisha haraka na kwa muda mrefu bila kusababisha uzito kuongezeka. TUMIA MUDA WOWOTE.

Uaandaji: - Chukua viwango sawa vya maharage, njugu mawe na mbaazi na chemsha kwa masaa kadhaa mpaka uone maharage na mbaazi zimetengana. Weka karoti moja nzimanzima ili inyonye gesi wakati wa kuchemsha. - Hapa unaweza kutumia supu hiyohiyo uliyochemshia na kunywa baada ya kuongeza chumvi. Pia unaweza kuchuja maji na kuweka hayo maharage na vinginevyo katika supu ya nyama uliyoandaa pembeni na kuinywa.

6. Supu Jembe (Supu ya Kabeji) Kwanini:
Supu hii inasifika kwa kuwa na mbogamboga nyingi zinazopunguza uzito. Unavyoinywa zaidi ndivyo unavyopungua zaidi. TUMIA MUDA WOWOTE.

Uandaaji: - Kabeji moja kubwa. Ikatekate vizuri. Vipande visiwe vidogodogo sana. - Kitunguu maji kimoja kikubwa. Kitakekate kama kawaida. - Pilipili hoho moja kubwa. Ikatekate vizuri. - Kitunguu swaumu, kifundo kimoja.

Menya na pondaponda vizuri. - Nyanya nusu kilo. Katakata vipande vikubwakubwa. (Si lazima kama hupendelei) - Karoti nusu kilo. Zikatwekatwe saizi kubwa za kutafuna. - Maji lita 5. Kama una chombo kidogo, basi tumia maji lita 2 na nusu halafu gawanya kila kilichopo hapo juu kwa 2. - Chumvi na pilipili kiasi Kaanga mbogamboga na vitunguu kwenye mafuta (mafuta ya nazi ni mazuri zaidi) kidogo (usiweke kabeji na nyanya).

Hakikisha vitunguu vinaiva lakini havibadiliki rangi kabisa. Ongeza nyanya, kabeji na maji na chemsha mpaka mbogamboga zilainike. Hapa unaweza kuongeza viungo na chumvi na kukoroga. Acha itulie kwa dakika 5 kisha epua. Unaweza kutunza supu yako kwenye friji na kunywa kila unapojisikia. Au kama haupo nyumbani unaweza kuiweka kwenye thermos na kunywa popote uendapo.

7. Salad ya maparachichi Kwanini:

Maparachichi ni matunda muhimu sana kama unajaribu kupunguza uzito. Yana virutubisho vinavyopelekea kuchomwa mafuta mwilini zaidi. Pia unaweza kutumia fursa hii kuongeza mbogamboga na matunda mengine yanayosaidia katika kupunguza uzito. TUMIA MUDA WOWOTE.

Uandaaji: - Vipande 4 vya vitunguu vilivyokatwa kwa mviringo - Machungwa 2 - Maparachichi 2 - Vijiko 3 vya chai vya mafuta ya zeituni (olive oil) - Vijiko 2 vya chai vya majani ya mint - Kijiko 1 cha chai cha maji fresh ya ndimu - Kijiko robo cha chai cha chumvi Loweka vitunguu, ukali utoke.

Menya machungwa na ondoa kabisa ule weupe ibaki nyama tu. Katakata kwa vipande vya mviringo. Menya na katakata maparachichi upendavyo. Ongeza majani ya mint. Ongeza mafuta ya olive ukipenda kwa ajili ya kuongeza ladha. Mwagia maji ya ndimu. Enjoy.

8. Juisi ya ndimu na matikitimaji Kwanini:
Ndimu na matikitimaji vyote ni aina ya vyakula ambavyo vimekubalika kusaidia kupunguza uzito. Ndimu inatumika katika detox na pia inasaidia kuchoma mafuta zaidi. Matikitimaji yana maji mengi, mafuta sifuri na nyuzinyuzi sana hivyo yana uwezo wa kushibisha kwa muda mrefu na hivyo kumuepusha mtu kula vyakula vibaya. Pia nyuzinyuzi zinatumia nishati nyingi wakati wa umeng’enywaji na hivyo huchoma mafuta mengi mwilini. TUMIA MUDA WOWOTE.

Uandaaji: - Ndimu 1 (ikamuliwe) - Tikiti kipande 1 saizi ya kati (lililomenywa) - Majani ya mint kiasi (ukipenda) Changanya vyote hapo juu kwenye blenda na saga mpaka upate kinywaji chenye rangi nyekundu. Hapo unaweza kunywa moja kwa moja. USIONGEZE MAJI. USIONGEZE SUKARI.

9. Makande ya maharage (kwa kutumia mahindi yasiyokobolewa kabisa)

Kwanini: Huu ni mlo wenye protini kwa wingi, wanga wa kutosheleza, nyuzinyuzi pia. Utashiba kwa muda mrefu ukila hivi. Lakini kuwa makini usizidishe kiwango. Kikombe 1 tu cha makande haya kinatosha. TUMIA KAMA MBADALA WA VYAKULA VYA WANGA MZURI TU.

Uandaaji: Andaa kama kawaida. Ila kama unataka matokeo mazuri zaidi. Kula bila kuunga. Ukishachemsha, ongeza chumvi kidogo na ufurahie upunguaji wa kilo.

10. Samaki na Vitunguu swaumu Kwanini:

Samaki wana virutubisho vya Omega 3 na pia protini kwa wingi sana. Virutubisho hivyo vinasaidia kuchoma mafuta mwilini na protini inasaidia kujenga misuli mingi zaidi ndani ya mwili, misuli ambayo inachoma mafuta zaidi muda wote na kukufanya upungue zaidi. Vitunguu swaumu vinaongeza nguvu ya samaki zaidi. TUMIA MUDA WOWOTE.

Utumiaji: Ongeza vitunguu swaumu kadhaa katika kila mboga ya samaki upikayo. Kama unakula mkavu basi ambatanisha na vitunguu swaumu vibichi.

11. Pilipili hoho na Mayai Kwanini:
Mayai yana kemikali iitwayo choline inayoongeza uchangamfu (metabolism) ndani ya mwili na kuufanya mwili uchome mafuta zaidi hata ukiwa umepumzika. Pilipili hoho ina vitamin C kwa wingi ambayo husaidia kupunguza kemikali ya cortisol ambayo inahusishwa na stress na kulundikwa mafuta yanayosababisha unene. Ukiunganisha hivi viwili unapata chakula chenye nguvu kubwa ya kupunguza uzito. TUMIA MUDA WOWOTE.

Utumiaji: Kama unakaanga mayai, yakaange pamoja na pilipili hoho. Kama unayachemsha, basi kula na pilipili hoho iliyopikwa kidogo pembeni. Ni nzuri kwa afya yako na kwa kuondoa kilo za ziada haraka zaidi.

12. MaApple na Matikitimaji Kwanini:
Apple ni tunda lenye nyuzinyuzi sana. Nyuzinyuzi ni muhimu katika kupunguza uzito kwa sababu humwezesha mtu kushiba haraka na kwa muda mrefu zaidi. Pia yana msaada wa moja kwa moja katika kuondoa mafuta mwilini hasa tumboni. Matikiti nayo yana nyuzinyuzi sana na ndio maana ukiunganisha haya matunda mawili unapata mchanganyiko wenye nguvu kubwa ya kupigana na uzito uliopitiliza. TUMIA MUDA WOWOTE.

Utumiaji: Unaweza kukatakata matunda haya, kuyachanganya na kutumia kama salad. Pia unaweza kuyasaga pamoja bila kuongeza chochote kisha unywe kama juisi (usitoe mbegu za tikiti).

13. Viazi vitamu na Mtindi Kwanini: Viazi vitamu vimeitwa ‘vyakula vya wanga ambavyo haviwezi kukunenepesha’. Hii ni kwa sababu ukiachana na wanga kiasi, viazi hivi vina nyuzinyuzi nyingi inayosaidia katika kuchoma mafuta mengi mwilini. Ivyo hayasababishi uzito kuongezeka kirahisi kama vyanzo vingine vya wanga. Hivi ni chakula kizuri sana cha kukupatia nguvu wakati wa diet. Mtindi una protini nyingi ambayo hufanya mwili ushibe kwa muda mrefu. Protini pia inachoma nishati nyingi wakati wa umeng’enywaji hivyo inasaidia kuchoma mafuta mengi zaidi mwilini. TUMIA KAMA MBADALA WA WANGA MZURI TU. Utumiaji: Kula viazi vitamu vya kuchemsha na mtindi usio na madoido wowote. Kula asubuhi au mchana kwa kuwa unahitaji nguvu zaidi mwilini wakati huo.

14. Matango na Apple cider vinegar Kwanini: Matango yana maji kwa asilimia 95. Hivyo ni tunda zuri kula mara kwa mara bila kuongeza kilo. Ila wengi huwa wanaboreka nayo. Hapa ndipo apple cider vinegar inapoingia. Apple cider vinegar inaenda kusababisha mafuta mengi zaidi kuchomwa ndani ya mwili na hivyo kufanya uzito upungue kwa kasi zaidi. TUMIA MUDA WOWOTE.

Utumiaji: Chomvya tango kwenye apple cider vinegar kabla ya kulila. Fanya kadri uwezavyo. Wengi huweka vijiko 2 vya apple cider vinegar kwenye glasi ya maji kabla ya kuanza kuchomvya.

15. Aloevera gel Kwanini:

Aloevera inachangamsha mwili (boosting metabolism) na kuongeza utumiaji wa nishati mwilini, ambavyo vyote husababisha mafuta kuchomwa zaidi. Pia inaondoa sumu katika mfumo wa umeng’’enywaji chakula (digestive system). TUMIA MUDA WOWOTE.

Utumiaji: Zipo wanazouza kwa ajili ya kunywa. Forever Aloevera gel ni mfani mzuri. Tumia kwa angalu mwezi 1 uanze kuona matokeo vizuri.

16. Kula chakula kilichochemshwa au kupikwa kutumia mvuke tu. Kwanini: Hii ni njia zaidi nzuri ya kuepuka mafuta na mbwembwe nyingi katika chakula. Pia virutubisho vilivyomo katika vyakula vinatunzwa zaidi katika chakula kilichochemshwa tu kuliko katika hali nyingine.

Ufanyaje: Chemsha vyakula vyako vingi. Usisahau kunywa na supu zake kwa kuwa inakusaidia kushiba haraka, na kukupunguzia kilo zaidi.

17. Nyanya Kwanini: Nyanya zina nyuzinyuzi ambazo husaidia mfumo wa umeng’enywaji uende haraka zaidi. Hii inaweza kuzuia chakula kubadilishwa kuwa mafuta. Pia zina vitamin A, C na K zinazokufanya uwe na afya zaidi. TUMIA MUDA WOWOTE.

Utumiaji: Kula nyanya 2 ambazo hazijapikwa kwa siku ili uweze kupunguza uzito. Ila kama zinakusumbua au una vidonda vya tumbo, usitumie.
 
Yani hapo umeassume kuwa Mtu afanye hivyo na wakati huo aendelee na ratiba zake Za kula milo Yake Kama kawaida Au siyo?!
 
Yani hapo umeassume kuwa Mtu afanye hivyo na wakati huo aendelee na ratiba zake Za kula milo Yake Kama kawaida Au siyo?!
Sidhani kuwa ndo lengo lake kwa sababu unapoamua kupunguza uzito sharti na ratiba ya kula ibadilike..ulikua unakula sana wanga na sukari inabidi upunguze ama uache kabisa,vilevi soda nk
 
Mimi ninavyopenda kuwa heavy weight nawashangaa sana hapa. Labda kwa jinsia za kike na wazee ndio wanatakiwa kupunguza uzito. Ninampango wa kufikisha kilo 110 ndio nilidhike. Super heavyweight
 
Back
Top Bottom