Alvin A.
JF-Expert Member
- Oct 14, 2016
- 2,868
- 3,624
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 07, 2019 imemwachia huru aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura baada ya kukiri kujipatia fedha za kitanzania zaidi ya shilingi milioni 100 kwa njia isiyo halali na kukubali kuzirejesha.
Mapema mwaka huu 2019, Wambura alikamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka 17 ya uhujumu uchumi ikiwemo kutakatisha fedha zaidi ya shilingi milioni 100.
Wambura ameachiwa huru katika kesi yake namba tisa ya mwaka 2019 na Hakimu Mfawidhi Kelvin Mhina na kutakiwa kulipa fedha hizo, ambapo amekubali kulipa kwa awamu tano, na leo tayari amelipa shilingi milioni 20.
Zaidi, soma:

Michael Wambura afikishwa Mahakamani Kisutu na kusomewa makosa 17 ikiwemo utakatishaji fedha
Michael Wambura amefikishwa Mahakamani Kisutu Mda Huu, Na anashitakiwa Kwa Makosa 17 kwa maana Ana count 17 kwenye charge Yake, Count ya 16+17 ni Money Laundering ambayo ni unbailable. ===== Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Michael Wambura, amefikishwa...
www.jamiiforums.com