Michael Richard Wambura aondolewa kwenye uchaguzi wa Simba SC

Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,421
1,387
Breaking news! Michael Richard Wambura aondolewa kwenye uchaguzi wa Simba.
stay tuned for more updates!

---------------------

Sababu ni kwamba alishawahi kuvuliwa uana chama na klabu hiyo na kwamujibu wa Damas Ndumbaro (Dkt) imebainika kwamba haikuwahi kufanyika kikao "halali" kilicho mrejeshea uana chama wake..sio maneno yangu bali ni ya M/Kiti kamati ya Uchaguzi Simba niliye mtaja hapo ..alipokua akiongea na wanahabari mapema leo!
 
Jamani huyu ana gundu gani lakini, si wamwache tu yaani we acha tu anaweza kufa kwa ugonjwa wa moyo. Ni kama yule meya wa Bukoba na Ubunge, alishawahi kupokwa hadi uraia kisa ubunge, Hata sarakasi zinazoendelea sasa hivi ni hilo tu
 
ushauri tu kwa kaka yangu WAMBURA hivi kwa elimu yako uliyonayo je ni lazima uwe kwenye michezo maana mi naona kama hiyo gemu imekuwa si njema sana kwako sasa kwanini usiachane tu na haya mambo ya michezo?
 
Nilijua kuwa jamaa ana damu ya kunguni na wale jamaa...

Behind haya ni lilee kundi la URAIS TFF. Na mmoja wa wale anagombea ujumbe kamati ya utendaji.
 
Ni sawa na kula nyama ya mtu,ukisha onja tu huwezi kuacha!!! We huoni hata Jamal Malinzi alivyokomalia TFF mpaka akapata urais kwa mbinde; sasa we jiulize huko kwenye michezo wanakokimbilia kuna nini?? Ni kwenda kuiba tu na sio kuendeleza michezo, by the time Malinzi anamaliza term yake hakuna lolote la maana atakalokuwa amelifanya kuendeleza soccer bongo lakini yeye atakuwa ameneemeka kwa fursa atakazojitengenezea!!!
 
Wambura hajui wala hana mahaba na michezo hata kidogo...
 
Wambura sasa apumzike tuu kugombea hata ubalozi wa nyumba kumi huenda wakamtosa pia
 
Ni Halbadri ya Mlandege ya Zanzibar alipoikosesha ushiriki wa Kombe la CAF wakati akiwa Katibu Mkuu FAT. Kisa? Tanzania kuchelewa kiwasilisha majina Makao Makuu Cairo. Ajabu? Jina la Simba lilitumwa kwa wakati, licha ya timu hizo kicheza ligi hiyohiyo ya Muungano wakati ule!
 
Wambura hajui wala hana mahaba na michezo hata kidogo...
Huwa naumia jinsi wambura anavyonyanyaswa. niliwahi kumsikiliza wakati wa rufaa yake ya TFF niliamini ni jembe la mpira ila kunawanaojua uwezo wake ndo maana wanamkaba mapema maana uwezo alionao akipewa nafasi kuna watu watasahau kuchaguliwa maana yeye yuko juu KIUELEWA.
 
Breaking news! Michael Richard Wambura aondolewa kwenye uchaguzi wa Simba.
stay tuned for more updates!
Wamefanya vzr kuondoa jina lake...........Jamaa angekuwa km malinzi kazi kupendelea kabila lake kwenye nafasi za uteuzi. NA WAMBURA NDO HIVOHIVO.
 
Hilo jamaa Wambura halina tofauti na Rage wukiwaona katika michezo ujue wamekuja kuua tu
 
Ana tatizo gani kwani mpaka wamuondoe?

Sababu ni kwamba alishawahi kuvuliwa uana chama na klabu hiyo na kwamujibu wa Damas Ndumbaro (Dkt) imebainika kwamba haikuwahi kufanyika kikao "halali" kilicho mrejeshea uana chama wake..sio maneno yangu bali ni ya M/Kiti kamati ya Uchaguzi Simba niliye mtaja hapo ..alipokua akiongea na wanahabari mapema leo!
 
Back
Top Bottom