Micah Richars na vitalu vya soka

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
15,497
22,337
Mchezaji mdogo na moja wa mabeki miamba wa timu ya Manchester City Micah Richards, amekiri kutaka kuchezea timu ya Arsenal siku moja.Mchezaji huyo ambae huchezea nafasi ya beki wa kushoto au kulia, amesema anaihusudu timu ya Arsenal tangu akiwa mdogo.

Mchezaji huyo wa kimataifa ambae pia ni beki wa pembeni wa timu ya taifa ya Uingereza, amesema amekuwa akiwa anawahusudu wachezaji mashuhuri wa Highbury Ian Wright na Patric Vieira.

Licha ya mahitaji ya huduma yake kutoka kwa timu za Chelsea, Liverpool na Manchester United tangu aingie katika timu ya taifa ya Uingereza,mchezaji huyo nyota wa Man City amedhihirisha matamanio yake ya kuweka saini mkataba na timu hio ya Arsene Wenger.

Ameliambia jarida hilo la Nuts kwamba,"nilikuwa shabiki mkubwa wa Ian Wright nilipokuwa mdogo hivo nishabikia Arsenal" alisema.

Aliendelea kwa kusema,"lakini kwa sasa nazingatia kuwiweka timu yangu ya Man City katika nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi na wachezaji tunao".

Mahojiano haya nimeyanukuu kutoka katika jarida la Nuts la hapa UK.

Timu ya Man City ni moja ya timu zinazokuza vipaji vya soka kwa vijana wadogo kabisa kwa hapa UK, zikiwa na shule maalum au "Academies" ambazo zimetoa wachezaji wa aina ya Micah Richards, Shaun Wright Philips, Michael Jonson,Joey Burton na wengine na matunda yake yanaonekana.

Timu zingine bila kusahau ni pamoja na Arsenal ambao nao wana shule ambayo inatoa vijana kama Justine Hoyte na David Bentley ambao kwa sasa ni wachezaji wa timu ya kwanza.

Sijui kama bila migogoro isiokwisha Tanzania kwa timu kuba za Yanga na Simba zingekuwa wapi kwa sasa katika medani ya soka Afrika.

Namkumbuka mzee Tambwe Leya ambae alisuka timu ya Yanga ya kutisha ya miaka ya tisini ya Mohamed Husein, Salvatory Edward,Bakari Malima na Sekilojo Chambua.

Waziri wa michezo wa sasa Tanzania sijui ana mipango gani ya kukuza michezo Tanzania. Inasikitisha kuona timu kama za Yanga na Simba bado zinategemea wafanyabiashara uchwara wanaokuja na kuondoka kila kukicha.

Mapendekezo yangu.

1. Waziri ateue timu ya wataalam waangalie namna ya kurekebisha mfumo wa soka na michezo mingine Tanzania, na wampe taarifa na mapendekezo yao.

2. Wachezaji wa zamani wa timu kama za Yanga na Simba wapewe nafasi za kwenda kusoma kufundisha soka katika nchi zilizoendelea na warudi nyumbani kuanzisha shule maalum za soka.

3. Huu sasa uwe ni wakati wa kubadilisha mfumo wa kutumia uwanja wa taifa kwa mechi zinazohusisha timu za Yanga na Simba. Mfumo huu ni wa wizi wa kimachomacho kwani timu hizo zina haki ya kuendeleza viwanja vyake kama pale Jangwani kwa Yanga na hatimae zijiendeshe zenyewe kwa revenue inayopatikana pale.

4. Serikali ipige marufuku na kuweka sheria kwamba kila timu iwe na wapenzi tu na sio wanachama. Ukiwa na watu wajiitao wanachama ndani ya timu hata kama hawachangii chochote huwa ni tatizo kwani huleta siasa badala ya pesa kama michango kwa kujiandikisha upenzi ambapo kama mimi nalipa £30 kwa Arsenal kama ada ya kila mwaka.

Jamani haya ni mambo ambayo ni madogo saana nashangaa Mzee Joel Bendera anafanya nini pale wizarani-"Wake up!"
 
Klabu kubwa za Yanga na Simba katika miaka fulani ziliwahi kuwa na timu zao ndogo zikiitwa timu B, ambapo kila mwaka wakati wa usajili waliweza kuwapandisha daraja wachezaji toka timu zao B. Sijui kama utaratibu huu bado upo ama la.. Lakini kupitia utaratibu huu timu hizo ziliweza kupata wachezaji wengi wenye vipaji na mapenzi ya dhati ya timu zao.

Vilabu vingi vya Tz bado ni vya ridhaa au haijulikani vipo kwenye ridhaa au ni vya kulipwa, kwani hakuna mfumo bayana uliowekwa katika uendeshaji wa vilabu vya soka hapa nchini. Mawazo wengi yameshatolewa kuwa vilabu hivyo viwe ni vya kulipwa kwani vina kila dalili ya kuwa hivyo. Sasa hapa ni kutangaza tu na tuone mabadiliko gani ambayo yataweza kutokea.

Suala la wachezaji wa zamani wa klabu kubwa kupewa nafasi ya kusomeshwa na kuja kuwa makocha ni la kibinafsi zaidi. Kuwa kocha kunatokana na mapenzi ya mtu. Wapo wachezaji ambao sasa ni makocha, ambao walijituma kwanza wenyewe, na baadae waliweza kuendelezwa ama na serikali au na timu wanazofundisha. Hili linafanyika.

Iwapo klabu zitakuwa ni za kulipwa hapana shaka wataweza kujitafutia viwanja vyao vya soka. Viwanja vingi vya soka hapa Tz ni vya serikali, halmashauri au ni vya CCM. Yanga wana uwanja wa Kaunda.. lakini uwanja huo hauna vipimo vya kuweza kucheza mechi za ligi ya aina yoyote. Klabu za mikoani zinatumia viwanja vya mikoa ambavyo vipo chini ya mamlaka zingine.
 
Nimekuelewa mkuu ila nilikuwa namaanisha kwamba wachezaji sio lazima wawe ni wa Simba na Yanga bali hata timu zingine wachagizwe waende kufanya mafunzo hata pale mlimani. Nafikiri pale mlimani kuna bwana Mziray ambae anaweza kusuka mipango mbalimbali ya kuendeleza soka.

Ukiangalia wachezaji kama Tony Adams,Roy Keane, Gareth Southgate na Glen Roeder ni wachezaji ambao wameamua kwa makocha kwa utashi wao hapa naungana na wewe.

Lakini kuna mfumo maalum wa kuwaangalia watu hawa kwamba wa -progress vipi na kazi zao.

Kwa hio Tanzania tunahitaji mfumo mpaya wa michezo ambao unakuwa endelevu kuanzia vitalu na hii ndio kazi ya waziri husika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom